NA MWANDISHI WETU
CHUO Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), kupitia Mradi wa Tathmini ya Mapato ya Kaboni kama Njia Endelevu ya Uwezeshaji Kifedha katika Uhifadhi na Usimamizi wa Misitu ya Jamii Tanzania, kimewajengea uwezo maafisa na wananchi kutoka maeneo yenye misitu ya hifadhi za vijiji, pamoja na vijiji ambavyo tayari vinashiriki katika biashara ya kaboni na kunufaika na mapato yatokanayo na biashara hiyo.
Mafunzo hayo yamelenga kuwapa washiriki uelewa kuhusu vigezo, taratibu na fursa zilizopo katika biashara ya kaboni, huku yakisisitiza umuhimu wa usimamizi bora wa mapato yanayotokana na biashara hiyo kwa manufaa ya jamii na uhifadhi endelevu wa misitu.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, mmoja wa wananchi kutoka vijiji ambavyo bado havijaanza kunufaika na mapato ya kaboni, Mwanangao Msanya, kutoka Mvomero mkoani Morogoro, alisema wamekuwa wakihifadhi misitu ya vijiji kwa muda mrefu, lakini mafunzo hayo yamewapa uelewa mpya kuhusu vigezo na taratibu za kuingia na kunufaika na biashara ya kaboni.
“Tumekuwa tukihifadhi misitu ya kijiji kwa muda, lakini kupitia mafunzo haya tumepata uelewa kuhusu namna ya kushiriki katika biashara ya kaboni na mambo muhimu tunayopaswa kuzingatia ili wananchi wanufaike,” alisema.
Afisa Misitu Mwandamizi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Siima Bakengesa, akifungua warsha hiyo iliyowakutanisha wadau kutoka taasisi za Serikali, asasi zisizo za kiserikali na wananchi kutoka Wilaya za Tanganyika, Mbulu, Mvomero, Mwanga na Korogwe, alisema mafunzo hayo ni muhimu katika kuimarisha uhifadhi wa bioanuwai na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kupitia usimamizi shirikishi wa misitu ya vijiji.
Kwa upande wake, Mtafiti Kiongozi wa Mradi huo, Dkt. Kajenje Nkukurah, alisema SUA inaamini mafunzo hayo yatawezesha vijiji ambavyo bado havijaingia katika biashara ya kaboni kufanya maamuzi sahihi kuhusu ushiriki wao, pamoja na kuimarisha utawala na usimamizi wa mapato katika ngazi ya vijiji.
Alisema mradi huo pia unalenga kuwajengea uwezo wananchi wa vijiji vyenye misitu inayoshiriki katika biashara ya kaboni ili waweze kuendelea kunufaika kiuchumi, huku mapato yatokanayo na biashara hiyo yakitumika katika usimamizi endelevu wa misitu ya hifadhi za vijiji na kuchochea maendeleo ya jamii.
Akitoa ushuhuda wakati wa kuwasilisha sauti za jamii, Afisa Misitu wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, Bruno Mwaisaka, alisema wilaya hiyo imepokea zaidi ya Sh bilioni 34 kutokana na biashara ya kaboni.
Alisema fedha hizo zimechangia kuboresha ustawi wa jamii kupitia ujenzi wa shule na vituo vya afya, pamoja na kutoa ajira za muda kwa wananchi, huku zikiendelea kuongeza ari ya jamii kushiriki katika uhifadhi na usimamizi wa misitu.
Mradi wa Tathmini ya Mapato ya Kaboni kama Njia Endelevu ya Uwezeshaji Kifedha katika Uhifadhi na Usimamizi wa Misitu ya Jamii Tanzania ni wa miaka mitatu na unatekelezwa na SUA kama taasisi inayoongoza, kwa kushirikiana na NCMC na Chuo Kikuu cha Bangor cha Uingereza.
Mradi huo unafadhiliwa na Defra kupitia GCBC, DAI, ISPF pamoja na Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Serikali ya Uingereza.

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...