Na Vero Ignatus, Michuzi Tv Arusha
Tanzania imeendelea kuchukua hatua za kuimarisha usalama wa nyuklia na mionzi kuelekea Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027, ikiwemo matumizi ya vifaa vya kugundua mionzi katika maeneo muhimu na mipakani, pamoja na kuwajengea uwezo maofisa walio mstari wa mbele katika kubaini na kukabiliana na matukio yanayoweza kuhusisha vyanzo vya mionzi.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), Profesa Najat Kassim Mohammed, amesema Tanzania kwa kushirikiana na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) imeanza kuimarisha maandalizi ya usalama wa nyuklia kuelekea AFCON 2027. Amesema Tanzania ni kiongozi na kinara katika kuhakikisha usalama wa nyuklia na mionzi unazingatiwa katika maandalizi ya mashindano hayo.
Profesa Najat amesema Serikali imewekeza katika wataalamu, vifaa na kujenga uwezo wa kitaifa, huku akisisitiza kuwa ukubwa na hadhi ya AFCON 2027 vinahitaji maandalizi ya kina na ushirikiano wa taasisi mbalimbali. Amesema warsha hiyo inayofanyika Agosti 31 hadi Septemba 4, 2026, imewakutanisha wataalamu na maofisa kutoka JWTZ, Jeshi la Polisi, vyombo vya usalama, mamlaka za forodha na uhamiaji pamoja na wasimamizi wa viwanja vya michezo.
Amesema washiriki wa warsha hiyo watapata mafunzo ya nadharia na vitendo kuhusu utambuzi wa mionzi, tathmini ya tahadhari, upekuzi na matumizi ya vifaa vya kugundua mionzi, ikiwemo Personal Radiation Detectors (PRDs) na Radioisotope Identification Devices (RIDs)
_Mazoezi hayo pia yatahusisha uchunguzi wa kimionzi katika mazingira ya uwanja wa michezo na maeneo ya watazamaji ili kuongeza utayari kuelekea AFCON 2027.
Kwa upande wake, Kiongozi wa Timu ya Wataalamu kutoka IAEA, Lacina Saro, amepongeza Tanzania kwa kuanza mapema maandalizi ya usalama wa nyuklia kuelekea AFCON 2027.
Amesema kuchaguliwa kwa Tanzania kuwa miongoni mwa wenyeji wa mashindano hayo ni jambo la kujivunia, lakini pia kunaambatana na wajibu wa kuhakikisha usalama unaandaliwa mapema, unafanyiwa majaribio na kutekelezwa kwa ufanisi. Ameongeza kuwa IAEA itaendelea kutoa miongozo, mafunzo na msaada wa kiufundi kwa Tanzania.
Naye Mkurugenzi wa Teknolojia na Huduma za Ufundi wa TAEC, Dkt. Remigius Kawala, amesema Tanzania ipo katika nafasi nzuri kutokana na uwekezaji wa Serikali katika wataalamu na vifaa vya usalama wa nyuklia na mionzi. Amesema zaidi ya asilimia 70 ya wataalamu wa TAEC wamebobea katika maeneo yanayohusiana na matumizi ya nguvu za atomu, nyuklia na mionzi, huku Tanzania ikiwa na vifaa vya kutosha vya kutekeleza majukumu ya kiusalama.
Dkt. Kawala amesema Tanzania imeomba msaada wa vifaa kwa kiwango cha chini ya asilimia 20 katika maandalizi ya AFCON 2027, jambo linaloonesha kuwa sehemu kubwa ya mahitaji inaweza kutekelezwa kwa kutumia uwezo na rasilimali zilizopo nchini. Amesema wataalamu wapatao 40 wanashiriki katika maandalizi hayo, huku Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi wenyeji wa AFCON 2027 pamoja na Kenya na Uganda, ikiwa na lengo la kuhakikisha mashindano yanafanyika katika mazingira salama.
Washiriki wa warsha hiyo watapata mafunzo ya nadharia na vitendo kuhusu utambuzi wa mionzi, tathmini ya tahadhari, upekuzi na matumizi ya vifaa vya kugundua mionzi, ikiwemo Personal Radiation Detectors (PRDs) na Radioisotope Identification Devices (RIDs). Mazoezi hayo pia yatahusisha uchunguzi wa kimionzi katika mazingira ya uwanja wa michezo.

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...