Na Janeth Raphael -MichuziTv
SERIKALI kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) imeendelea kuweka mkazo katika utekelezaji wa miradi ya umeme inayolenga kuhakikisha wawekezaji katika sekta mbalimbali, ikiwemo madini, viwanda, kilimo cha kisasa na ufugaji, wanapata nishati ya uhakika kwa ajili ya kuongeza uzalishaji na kuchochea ukuaji wa uchumi.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Nishati, Salome Makamba, wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa utekelezaji wa mradi wa kusafirisha umeme wa msongo wa kilovoti 220 pamoja na kituo cha kupokea na kupoza umeme cha kilovoti 220/33 kwa ajili ya Geita Gold Mining (GGM), iliyofanyika jijini Dodoma.
Makamba amesema Serikali inalenga kufanya upatikanaji wa nishati ya uhakika kuwa miongoni mwa vivutio vikubwa vya uwekezaji nchini, kwa kuhakikisha miundombinu ya umeme inaendana na mahitaji ya uchumi na kasi ya uwekezaji.
Amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kuwekeza katika miundombinu ya nishati ili umeme uwe kichocheo cha uzalishaji na kivutio kwa wawekezaji zaidi kuja nchini.
“Mwekezaji anapokuja Tanzania, nishati iwe kichocheo na kivutio kikubwa cha uwekezaji na uzalishaji wake,” amesema Makamba.
Amesema Serikali pia imechukua hatua za kuimarisha uwezo wa TANESCO kifedha na kiutendaji ili shirika hilo liweze kuendelea kutekeleza miradi mikubwa ya nishati. Kwa mujibu wa Makamba, Wizara ya Fedha imeidhinisha TANESCO kukopa Sh bilioni 229.3 kutoka benki za ndani kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati yenye lengo la kuongeza mapato na kujenga uwezo wa shirika kuendelea kuwekeza.
Amesema uwekezaji huo unalenga kuhakikisha miradi ya umeme inaleta manufaa kwa pande zote, ambapo Serikali inawekeza katika miundombinu, mwekezaji anaongeza uzalishaji, TANESCO inaongeza mapato na Taifa linapata manufaa ya kiuchumi.
Makamba amesema mradi wa GGM ni mfano wa utekelezaji wa falsafa hiyo, kwa kuwa Serikali inawekeza katika miundombinu ya umeme huku mwekezaji akitarajiwa kuongeza uzalishaji, jambo litakalosaidia kuongeza mapato ya TANESCO na Serikali pamoja na kuchochea shughuli nyingine za kiuchumi.
Amesema uwekezaji katika nishati hauhusiani tu na kuwasha taa au kuendesha mashine, bali una nafasi kubwa katika kuongeza uzalishaji, kupunguza gharama za uzalishaji, kuongeza ajira, mapato ya Serikali, thamani ya rasilimali za nchi na kuvutia wawekezaji wengine.
“Tunapozungumzia uwekezaji katika nishati, tunazungumzia zaidi ya kuwasha taa au kuendesha mashine. Tunazungumzia kuongeza uzalishaji, kupunguza gharama za uzalishaji, kuongeza ajira, kuongeza mapato ya Serikali, kuongeza thamani ya rasilimali zetu na kuvutia wawekezaji wengine kuja kuwekeza nchini,” amesema.
Makamba amesema kila njia ya umeme inayojengwa, kila kituo kinachokamilishwa na kila mwekezaji anayeunganishwa kwenye Gridi ya Taifa ni sehemu ya kujenga uchumi imara, endelevu na wenye ushindani.
Amesema Wizara ya Nishati itaendelea kusimamia utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050 inayotambua nishati kuwa miongoni mwa vichocheo muhimu vya ukuaji wa uchumi na maendeleo ya nchi.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Geita, Hashim Komba, ameishukuru Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa inayoendelea katika kuimarisha sekta ya nishati, akisema nishati ni eneo muhimu linalochochea maendeleo ya sekta nyingine za uzalishaji.
Komba amesema mkoani Geita kazi ya kusambaza umeme inaendelea, huku akipongeza TANESCO kwa namna inavyoendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kugusa moja kwa moja sekta ya madini ambayo ni miongoni mwa sekta muhimu katika mkoa huo.
Amesema ongezeko la shughuli za utafiti wa madini limechochea kuongezeka kwa maeneo ya uchimbaji, hali inayosababisha mahitaji makubwa ya nishati ya uhakika kwa wachimbaji wakubwa, wa kati na wadogo.
Komba amesema mradi wa kupeleka umeme GGM haupaswi kuangaliwa kwa upande wa kusaidia mgodi pekee, bali pia kwa namna unavyoweza kuchochea uwekezaji na kuongeza mapato ya Serikali, pamoja na kuwezesha wachimbaji wadogo kupata umeme wa kutosha katika maeneo yao ya shughuli.
Amesema mkoa huo utaendelea kushirikiana na TANESCO kutoa elimu kwa wachimbaji wadogo kuhusu namna wanavyoweza kutumia fursa ya umeme katika maeneo yao ya uchimbaji, hususan kupitia Maonesho ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika kila mwaka mkoani Geita.
Kwa mwaka huu, amesema Geita inatarajia kufanya maonesho hayo kwa mara ya tisa, huku akiahidi kuwa Serikali ya Mkoa itashirikiana na TANESCO kuhakikisha wachimbaji wadogo wanaelewa vizuri fursa zinazotokana na upatikanaji wa umeme katika maeneo yao.
Komba pia amesema Serikali ya Mkoa wa Geita imejipanga kushirikiana na mkandarasi wa mradi huo kuhakikisha utekelezaji wake unakwenda kwa wakati na kwamba changamoto zozote zinazoweza kuchelewesha mradi zitashughulikiwa kwa haraka.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Lazaro Twange, amesema uwekezaji nchini unaendelea kukua, hususan katika sekta ya madini ambayo inahitaji nishati ya uhakika kutokana na matumizi ya teknolojia na mashine za kisasa.
Twange amesema upatikanaji wa umeme wa uhakika utawawezesha wachimbaji wakubwa, wa kati na wadogo kuongeza ufanisi wa shughuli zao, kutumia teknolojia za kisasa na kuongeza uzalishaji.
Amesema TANESCO itaendelea kutekeleza miradi ya umeme kwa kuzingatia mahitaji ya wawekezaji na sekta mbalimbali za uzalishaji, ili kuhakikisha nishati inakuwa kichocheo cha shughuli za kiuchumi nchini.
Mradi wa kusafirisha umeme wa msongo wa kilovoti 220 pamoja na kituo cha kupokea na kupoza umeme cha kilovoti 220/33 kwa ajili ya GGM unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 18 iliyopangwa.
Serikali imeeleza kuwa uwekezaji katika miundombinu ya umeme ni sehemu muhimu ya kuongeza uzalishaji, mapato ya TANESCO, ajira na uwekezaji, huku ukichangia kwa ujumla katika ukuaji na maendeleo ya uchumi wa Taifa.

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...