Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya kimataifa ya teknolojia ya fedha, Verto kwa kushirikiana na Visa, imezindua kadi
maalumu ya biashara inayojumuisha sarafu nyingi kuwezesha malipo ya kimataifa.
Kadi hiyo inalenga kusaidia wafanyabiashara barani Afrika kupunguza gharama za ubadilishaji wa fedha za kigeni, kuboresha usimamizi wa matumizi ya fedha na kuongeza ufanisi wa shughuli zao katika masoko ya kimataifa.
Kadi hiyo ya Verto inawawezesha wafanyabiashara kutumia fedha moja kwa moja kutoka kwenye akaunti zao bila kulazimika kuhamisha fedha kati ya akaunti ama kubadilisha fedha kabla ya kufanya malipo.
Kupitia kadi hiyo wafanyabiashara wanaweza kuzifikia sarafu 11 moja kwa moja huku wakipata fursa ya kutumia zaidi ya sarafu nyingine 160 kupitia mtandao wa kimataifa wa malipo wa Visa.Aidha,huduma hiyo haitatoza nyongeza ya gharama za ubadilishaji wa fedha za kigeni katika sarafu kuu 10.
Akizungumza kuhusu uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi Mwenza wa Verto, Ola
Oyetayo, alisema huduma hiyo inalenga kukabiliana na pengo kubwa la miundombinu ya kifedha linalozikabili biashara za barani Afrika zinazofanyika kimataifa.
“Biashara za Afrika zimekua na kuvuka mipaka kwa kasi kikubwa kuliko miundombinu ya kifedha
inayozihudumia. Kwa sasa, changamoto si upatikanaji wa masoko, bali ni namna fedha zinavyohamishwa.
“Kampuni nyingi bado zinapoteza fedha kutokana na gharama zisizo za lazima
katika ubadilishaji wa fedha, ucheleweshaji wa malipo na taratibu za kibenki zilizogawanyika, ambazo huathiri moja kwa moja faida na ukuaji wa biashara.
“Kadi ya Verto imeundwa kuwapa wafanyabiashara udhibiti mkubwa zaidi wa matumizi ya kimataifa, huku ikipunguza baadhi ya vikwazo ambavyo kwa muda mrefu vimeambatana na biashara za hizo kimataifa,” alisema.
Kadi ya Verto inakubalika katika zaidi ya maduka na biashara milioni 150 duniani kote, popote ambapo kadi zote za Visa zinakubalika, ikiwemo kwa wafanyabiashara wanaohitaji mifumo ya malipo ya kadi za mkopo.
Hali hiyo inaziwezesha biashara kupata fursa ya kufanya malipo kwa wafanyabiashara wa kimataifa kwa kutumia kadi moja iliyounganishwa na akaunti zao za Verto.
Kadi hiyo pia inaruhusu biashara kugharamia miamala moja kwa moja kutoka kwenye pochi zao za sarafu za Verto, hatua inayosaidia kupunguza ubadilishaji wa fedha usio wa lazima na kuboresha ufuatiliaji pamoja na udhibiti wa matumizi ya fedha kimataifa.
Jukwaa hilo linajumuisha pia mifumo ya kudhibiti matumizi, utoaji wa kadi papo hapo na usalama wa miamala ulioimarishwa.

“Usimamizi wa sarafu nyingi haupaswi kuwa kikwazo cha ukuaji kwa biashara zinazolenga kupanua shughuli zao kimataifa,” alisema Shahebaz Khan, Makamu wa Rais Mwandamizi na Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Uhamishaji Fedha wa Visa.
“Ushirikiano wetu na Verto unasaidia kurahisisha namna biashara zinavyowalipa wasambazaji, kusimamia gharama na kufanya miamala kimataifa huku zikipata usalama na ukubalifu mpana wa kimataifa wanaoutegemea kutoka Visa,” alisema.
Wakati biashara za Afrika Mashariki zikizidi kupanua shughuli zao katika masoko mapya, uwezo wa kuhamisha na kusimamia fedha kwa ufanisi kuvuka mipaka unazidi kuwa suala la muhimu.
Kuanzia kuwalipa wasambazaji wa kimataifa na kusimamia usajili wa huduma hadi kugharamia shughuli za uendeshaji katika masoko mbalimbali, biashara zinahitaji mifumo ya malipo inayoweza kwenda sambamba na shughuli zao zinazozidi kukua kimataifa.
Uzinduzi huo ni sehemu ya mpango mpana wa Verto wa kupanua miundombinu yake ya usimamizi wa fedha na malipo ya kimataifa kwa lengo la kusaidia biashara katika masoko mapya zinapopanua shughuli zao kuvuka mipaka na kusaka fursa mpya kimataifa.
Kuhusu Verto Verto ni kampuni ya kimataifa ya teknolojia ya fedha inayolenga biashara kwa biashara (B2B) ikiwezesha biashara za ukubwa wowote kupata huduma za malipo yanayovuka mipaka, ubadilishaji wa fedha za kigeni na huduma za kibenki zenye viwango vya biashara kubwa.
Kupitia miundombinu ya kiteknolojia iliyoundwa mahsusi na mifumo ya malipo, biashara zinaweza kutuma na kupokea fedha papo hapo katika nchi zaidi ya 190 na kubadilisha fedha hizo katika sarafu 48.
Kwa sasa, Verto inahudumia biashara zaidi ya 5,000 duniani kote, kuanzia kampuni ndogo na za kati hadi mashirika makubwa ya kimataifa. Biashara hizo hufanya miamala yenye kufikia zaidi ya dola za Marekani bilioni 25 kwa mwaka.
Kuhusu Visa Visa ni kampuni inayoongoza duniani katika malipo ya kidijiti inayowezesha miamala kati ya watumiaji, wauzaji, taasisi za kifedha na mashirika ya serikali katika nchi zaidi ya 200.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...