Na Jane Mwakyoma, Rukwa

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Rukwa, Silafu Maufi, amewataka wajumbe wa Baraza la Wazee wa chama hicho mkoani humo kuendelea kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, kinachotarajiwa kufanyika mkoani Rukwa Oktoba 14, mwaka huu.

Maufi ametoa rai hiyo leo wakati alipokutana na kuzungumza na wajumbe wa Baraza hilo kuhusu maandalizi ya mapokezi na kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, akisisitiza umuhimu wa wazee kushiriki kikamilifu katika maandalizi na kuhamasisha jamii kujitokeza katika shughuli hiyo ya kitaifa.

Aidha, amesema kilele hicho kitaambatana na Wiki ya Vijana, ambapo vijana kutoka mikoa mbalimbali nchini wataonesha shughuli za maendeleo wanazozifanya. Maonesho hayo yanatarajiwa kufunguliwa Oktoba 8, mwaka huu.

Kwa upande wao, wajumbe wa Baraza la Wazee la CCM Mkoa wa Rukwa wameahidi kutoa ushirikiano katika kufanikisha shughuli zote za mapokezi ya Mwenge wa Uhuru na kilele chake, pamoja na kuendelea kuelimisha makundi mbalimbali ya jamii kuhusu umuhimu wa Mwenge wa Uhuru kitaifa.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...