Na Mwandishi Wetu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt. Leonard Akwilapo, amewaonya wananchi wanaovamia maeneo kwa nguvu na kuunda vikosi vya ulinzi kwa ajili ya kulinda maeneo hayo, akisema Serikali haitavumilia vitendo hivyo na kwamba hatua kali za kisheria zitachukuliwa.
Dkt. Akwilapo ametoa onyo hilo leo Sept 17, 2026 wakati akizungumza na wananchi katika Kliniki ya Ardhi iliyofanyika Kata ya Zingiziwa, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Amesema, wananchi hawapaswi kujichukulia sheria mkononi kwa kuvamia maeneo yanayomilikiwa na watu wengine na kuanzisha vikosi vya ulinzi kwa lengo la kuyadhibiti kwa nguvu.
“Serikali haitavumilia vitendo vya watu kujichukulia sheria kwa kuvamia maeneo ya wananchi wengine na kuunda vikosi vya ulinzi kwa lengo la kulinda maeneo hayo kwa nguvu,” amesema Dkt. Akwilapo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Bw. Elihuruma Mabelya, amesema hadi sasa jumla ya hati miliki 545 zimetolewa kwa wananchi kupitia Kliniki hiyo ya Ardhi.
Mabelya ameeleza kuwa, timu ya wataalamu itaendelea kuwepo katika eneo hilo ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma za ardhi kwa urahisi na kwa wakati, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Wizara.
Baadhi ya wananchi, kupitia Diwani wa Kata hiyo, wameipongeza Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kusogeza huduma za ardhi karibu na maeneo yao.
Wameielezea hatua hiyo kuwa imewapunguzia adha ya kusafiri umbali mrefu pamoja na gharama kubwa walizokuwa wakitumia ili kufuata huduma hizo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt. Leonard Akwilapo, akizungumza na wananchi waliojitokeza katika Kliniki ya Ardhi iliyofanyika Kata ya Zingiziwa, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, leo Septemba 17, 2026.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt. Leonard Akwilapo, akizungumza na wananchi waliojitokeza katika Kliniki ya Ardhi iliyofanyika Kata ya Zingiziwa, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, leo Septemba 17, 2026.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt. Leonard Akwilapo, akikabidhi hati kwa baadhi ya wananchi waliokamilisha taratibu za umiliki wa ardhi na waliojitokeza katika Kliniki ya Ardhi iliyofanyika Kata ya Zingiziwa, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, leo Septemba 17, 2026.

Sehemu ya wananchi waliojitokeza katika Kliniki ya Ardhi iliyofanyika Kata ya Zingiziwa, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, leo Septemba 17, 2026.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...