Benki ya Exim Tanzania kupitia programu ya Exim Cares, imefanya zoezi la uhamasishaji kuhusu saratani ya matiti lililowapa fursa wafanyakazi na wanajamii inayowazunguka kupata elimu na huduma ya uchunguzi wa saratani ya matiti bila malipo katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam.
Zoezi hilo ni sehemu ya maadhimisho ya Mwezi wa Uhamasishaji kuhusu Saratani ya Matiti, unaoadhimishwa kila Oktoba, kwa lengo la kuongeza uelewa kuhusu ugonjwa huo na kuhimiza utambuzi wa mapema.
Kupitia wataalamu kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road, washiriki walipata elimu kuhusu dalili na mabadiliko yanayoweza kuashiria saratani ya matiti, umuhimu wa tathmini ya kitabibu na hatua za kuchukua wanapobaini mabadiliko yasiyo ya kawaida, huku juhudi zikilenga pia kupunguza hofu na dhana potofu zinazoweza kuchelewesha upatikanaji wa huduma za afya.
Kwa mwaka 2026, Mwezi wa Uhamasishaji kuhusu Saratani ya Matiti unaambatana na kaulimbiu “Kila simulizi ni ya kipekee, kila hatua ina thamani”, inayosisitiza umuhimu wa taarifa sahihi, huduma zinazofaa na msaada kwa watu walioathiriwa na ugonjwa huo.
Hatua hiyo inakuja wakati saratani ya matiti ikiendelea kuwa changamoto ya afya duniani na nchini Tanzania. Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Utafiti wa Saratani (IARC), katika makadirio yake ya mwaka 2024, visa vipya takribani milioni 2.43 vya saratani ya matiti vilitokea duniani. Nchini Tanzania, wanawake takribani 3,024 walikadiriwa kugundulika na ugonjwa huo, huku vifo 1,492 vikikadiriwa kutokana na saratani ya matiti katika mwaka huo.
Aidha, kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), kiwango cha kuishi kwa angalau miaka mitano baada ya kugundulika na saratani ya matiti kilikadiriwa kuwa asilimia 77.8 duniani, ikilinganishwa na asilimia 39.1 katika Kanda ya Afrika ya WHO, kwa wanawake waliogundulika kati ya mwaka 2017 na 2021. Takwimu hizi zinasisitiza umuhimu wa utambuzi wa mapema na upatikanaji wa huduma za uchunguzi na matibabu kwa wakati ili kuboresha matokeo ya matibabu na kupunguza vifo.
Akizungumzia ushiriki wa benki katika juhudi hizo, Meneja Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim Tanzania, Kauthar D’souza, alisema afya na ustawi wa wafanyakazi wa benki na jamii kwa ujumla ni sehemu muhimu ya mchango wa benki kupitia mpango wa Exim Cares.
“Afya ya jamii inahitaji ushirikiano na hatua za pamoja. Kupitia Exim Cares, tunaunga mkono juhudi zinazowasaidia wafanyakazi wetu na jamii kupata taarifa sahihi kuhusu afya na kuelewa umuhimu wa kuchukua hatua kwa wakati. Tunaamini kuwa kuongeza uelewa kuhusu saratani ya matiti ni sehemu muhimu ya kuhimiza utunzaji wa afya na upatikanaji wa huduma zinazofaa,” alisema D’souza.
''Kwa mujibu wa WHO, takribani asilimia 80 ya saratani ya matiti hutokea kwa wanawake wasio na vihatarishi maalumu vinavyojulikana isipokuwa kuwa mwanamke na kuongezeka kwa umri. Hivyo, kutokuwa na historia ya saratani ya matiti katika familia hakumaanishi kuwa mtu hawezi kupata ugonjwa huo, jambo linalosisitiza umuhimu wa kufahamu mabadiliko ya mwili na kutafuta ushauri wa kitaalamu inapohitajika'', aliongeza.
Kwa upande wake, Dactari Maguha Stephano, mwakilishi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road alisema kuwa kuelimisha jamii na kuhamasisha watu kutafuta huduma za afya mapema ni sehemu muhimu ya juhudi za kukabiliana na saratani ya matiti.
“Ni muhimu jamii kupata taarifa sahihi kuhusu saratani ya matiti na kutoruhusu hofu au dhana potofu kuwazuia kutafuta huduma za afya. Watu wanapaswa kufahamu mabadiliko ya miili yao na kutafuta ushauri wa kitaalamu wanapobaini mabadiliko yasiyo ya kawaida, kama vile uvimbe kwenye titi au kwapani, au mabadiliko kwenye ngozi ya titi au chuchu. Tathmini ya kitabibu kwa wakati husaidia kuharakisha utambuzi na hatua zinazofaa,” alisema.
Exim Cares ni programu ya uwajibikaji kwa jamii ya Benki ya Exim Tanzania inayolenga kuboresha maisha kupitia juhudi katika sekta za afya, elimu, mazingira, ubunifu na elimu ya fedha. Katika sekta ya afya, benki imekuwa ikiunga mkono kampeni za uchangiaji damu kwa kushirikiana na Huduma ya Taifa ya Damu Salama (NBTS), kuimarisha huduma za afya hospitalini kupitia msaada wa vifaa tiba na kuboresha mazingira kwaajili ya wagonjwa wenye changamoto ya afya ya akili. Juhudi hizi zinaonesha dhamira ya benki katika kuendeleza afya na ustawi wa jamii.
Benki ya Exim Tanzania inawahimiza wafanyakazi wake na jamii kwa ujumla kufanya utunzaji wa afya kuwa sehemu ya maisha ya kila siku, kupata ushauri wa kitaalamu kuhusu uchunguzi unaofaa na kutochelewa kutafuta huduma za afya wanapobaini mabadiliko yasiyo ya kawaida.
Meneja Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim Tanzania, Kauthar D’souza, akiwa katika hatua moja wapo ya uchunguzi wa saratani ya matiti wakati wa zoezi la uhamasishaji lililoandaliwa na benki hiyo kupitia programu ya Exim Cares kwa kutumia wataalamu kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road, jijini Dar es Salaam, tarehe 23 Oktoba 2026. Zoezi hilo liliwapa wafanyakazi wa benki na wanajamii inayowazunguka kupata elimu na huduma ya uchunguzi bila malipo, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Mwezi wa Uhamasishaji kuhusu Saratani ya Matiti, unaoadhimishwa kila Oktoba, kwa lengo la kuhamasisha utambuzi wa mapema na matumizi ya taarifa sahihi za afya
.jpeg)


.jpeg)
.jpeg)
Kwa mwaka 2026, Mwezi wa Uhamasishaji kuhusu Saratani ya Matiti unaambatana na kaulimbiu “Kila simulizi ni ya kipekee, kila hatua ina thamani”, inayosisitiza umuhimu wa taarifa sahihi, huduma zinazofaa na msaada kwa watu walioathiriwa na ugonjwa huo.
Hatua hiyo inakuja wakati saratani ya matiti ikiendelea kuwa changamoto ya afya duniani na nchini Tanzania. Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Utafiti wa Saratani (IARC), katika makadirio yake ya mwaka 2024, visa vipya takribani milioni 2.43 vya saratani ya matiti vilitokea duniani. Nchini Tanzania, wanawake takribani 3,024 walikadiriwa kugundulika na ugonjwa huo, huku vifo 1,492 vikikadiriwa kutokana na saratani ya matiti katika mwaka huo.
Aidha, kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), kiwango cha kuishi kwa angalau miaka mitano baada ya kugundulika na saratani ya matiti kilikadiriwa kuwa asilimia 77.8 duniani, ikilinganishwa na asilimia 39.1 katika Kanda ya Afrika ya WHO, kwa wanawake waliogundulika kati ya mwaka 2017 na 2021. Takwimu hizi zinasisitiza umuhimu wa utambuzi wa mapema na upatikanaji wa huduma za uchunguzi na matibabu kwa wakati ili kuboresha matokeo ya matibabu na kupunguza vifo.
Akizungumzia ushiriki wa benki katika juhudi hizo, Meneja Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim Tanzania, Kauthar D’souza, alisema afya na ustawi wa wafanyakazi wa benki na jamii kwa ujumla ni sehemu muhimu ya mchango wa benki kupitia mpango wa Exim Cares.
“Afya ya jamii inahitaji ushirikiano na hatua za pamoja. Kupitia Exim Cares, tunaunga mkono juhudi zinazowasaidia wafanyakazi wetu na jamii kupata taarifa sahihi kuhusu afya na kuelewa umuhimu wa kuchukua hatua kwa wakati. Tunaamini kuwa kuongeza uelewa kuhusu saratani ya matiti ni sehemu muhimu ya kuhimiza utunzaji wa afya na upatikanaji wa huduma zinazofaa,” alisema D’souza.
''Kwa mujibu wa WHO, takribani asilimia 80 ya saratani ya matiti hutokea kwa wanawake wasio na vihatarishi maalumu vinavyojulikana isipokuwa kuwa mwanamke na kuongezeka kwa umri. Hivyo, kutokuwa na historia ya saratani ya matiti katika familia hakumaanishi kuwa mtu hawezi kupata ugonjwa huo, jambo linalosisitiza umuhimu wa kufahamu mabadiliko ya mwili na kutafuta ushauri wa kitaalamu inapohitajika'', aliongeza.
Kwa upande wake, Dactari Maguha Stephano, mwakilishi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road alisema kuwa kuelimisha jamii na kuhamasisha watu kutafuta huduma za afya mapema ni sehemu muhimu ya juhudi za kukabiliana na saratani ya matiti.
“Ni muhimu jamii kupata taarifa sahihi kuhusu saratani ya matiti na kutoruhusu hofu au dhana potofu kuwazuia kutafuta huduma za afya. Watu wanapaswa kufahamu mabadiliko ya miili yao na kutafuta ushauri wa kitaalamu wanapobaini mabadiliko yasiyo ya kawaida, kama vile uvimbe kwenye titi au kwapani, au mabadiliko kwenye ngozi ya titi au chuchu. Tathmini ya kitabibu kwa wakati husaidia kuharakisha utambuzi na hatua zinazofaa,” alisema.
Exim Cares ni programu ya uwajibikaji kwa jamii ya Benki ya Exim Tanzania inayolenga kuboresha maisha kupitia juhudi katika sekta za afya, elimu, mazingira, ubunifu na elimu ya fedha. Katika sekta ya afya, benki imekuwa ikiunga mkono kampeni za uchangiaji damu kwa kushirikiana na Huduma ya Taifa ya Damu Salama (NBTS), kuimarisha huduma za afya hospitalini kupitia msaada wa vifaa tiba na kuboresha mazingira kwaajili ya wagonjwa wenye changamoto ya afya ya akili. Juhudi hizi zinaonesha dhamira ya benki katika kuendeleza afya na ustawi wa jamii.
Benki ya Exim Tanzania inawahimiza wafanyakazi wake na jamii kwa ujumla kufanya utunzaji wa afya kuwa sehemu ya maisha ya kila siku, kupata ushauri wa kitaalamu kuhusu uchunguzi unaofaa na kutochelewa kutafuta huduma za afya wanapobaini mabadiliko yasiyo ya kawaida.
Meneja Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim Tanzania, Kauthar D’souza, akiwa katika hatua moja wapo ya uchunguzi wa saratani ya matiti wakati wa zoezi la uhamasishaji lililoandaliwa na benki hiyo kupitia programu ya Exim Cares kwa kutumia wataalamu kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road, jijini Dar es Salaam, tarehe 23 Oktoba 2026. Zoezi hilo liliwapa wafanyakazi wa benki na wanajamii inayowazunguka kupata elimu na huduma ya uchunguzi bila malipo, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Mwezi wa Uhamasishaji kuhusu Saratani ya Matiti, unaoadhimishwa kila Oktoba, kwa lengo la kuhamasisha utambuzi wa mapema na matumizi ya taarifa sahihi za afya.jpeg)


.jpeg)
.jpeg)


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...