Kamati ya Mipango Miji ya Halmashauri ya Mji Mafinga imefanya ziara ya ukaguzi katika eneo la Makalala, lililopo Kata ya Wambi, kwa lengo la kukagua eneo lililotengwa kwa ajili ya maziko ya waumini wa Kanisa Katoliki.
Ziara hiyo imeongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga, Mhe. Regnant Kivinge, akiambatana na Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango Miji, Mhe. Richard Mduda, Kaimu Mkurugenzi pamoja na wajumbe wa kamati hiyo.
Akiwasilisha taarifa ya ukaguzi wa eneo hilo, Mkuu wa Idara ya Ardhi na Mipango Miji wa Halmashauri ya Mji Mafinga, Ndugu Luis Ndumbaro, amesema kuwa uongozi wa Kanisa Katoliki umetenga eneo lenye ukubwa wa ekari saba kwa ajili ya maziko ya waumini wake.Aidha, ameeleza kuwa eneo hilo litaunganishwa na barabara ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za maziko kwa wananchi.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango Miji, Mhe. Richard Mduda, ameushukuru uongozi wa Kanisa Katoliki kwa kutenga eneo hilo kwa ajili ya kuwahudumia wananchi. Vilevile, amesisitiza umuhimu wa eneo hilo kufanyiwa usafi na kutunzwa vizuri ili kuhakikisha linakuwa katika hali nzuri na salama kwa matumizi yaliyokusudiwa. Pia, amependekeza shughuli za uzalishaji wa mkaa katika eneo hilo zifanyike kwa kuzingatia taratibu za uhifadhi wa mazingira.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga, Mhe. Regnant Kivinge, ameushukuru uongozi wa Kanisa Katoliki kwa kutoa eneo hilo kwa ajili ya maziko. Aidha, amependekeza kutokuwepo kwa masharti na kuwanyima fursa waumini wa dini mbalimbali kupata huduma za maziko katika eneo hilo, kwa kuzingatia makubaliano na taratibu zitakazowekwa na mamlaka husika.
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...