Na Seif Mangwangi, Michuzi Tv Arusha
Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, amesema mkutano wa Umoja huo unaofanyika jijini Arusha ni fursa kubwa kwa Tanzania kujitangaza kimataifa kupitia diplomasia ya kibunge, utalii na namna nchi inavyoshirikisha makundi mbalimbali katika uongozi na meza za maamuzi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo 1Oktoba 2026, Jijini Arusha alipotua kwaajili ya maandalizi ya mkutano huo unaoanza Oktoba 5 mwaka huu, Dkt. Tulia amesema mkutano huo unaowakutanisha wabunge na viongozi kutoka zaidi ya nchi 180 duniani.
Dkt Tulia amesema mkutano huo umeifanya Tanzania kuwa sehemu muhimu ya mijadala ya kimataifa, huku wajumbe hao wakipata nafasi ya kujifunza kuhusu Tanzania na Watanzania nao kupata fursa ya kujifunza kutoka kwa mataifa mbalimbali.
Amesema uwepo wa zaidi ya wageni 2,000 nchini ni fursa ambayo Tanzania inapaswa kuitumia kuwaonyesha wageni hao uwezo wa nchi katika kuandaa mikutano mikubwa ya kimataifa, pamoja na ukarimu wa Watanzania.
Kwa mujibu wa Dkt. Tulia, mkutano huo pia umeipa Tanzania nafasi ya kuonyesha namna inavyoshirikisha wanawake katika uongozi, akibainisha kuwa nchi inaongozwa na mwanamke, jambo ambalo ni sehemu ya uzoefu ambao dunia inaweza kujifunza kutoka Tanzania.
Amesema pamoja na wanawake, Tanzania imekuwa ikitoa nafasi kwa vijana na watu wenye ulemavu kushiriki katika michakato ya maamuzi, akisisitiza umuhimu wa kuhakikisha makundi mbalimbali yanapata nafasi katika uongozi.
Dkt. Tulia amesema Tanzania inapaswa kutumia uwepo wa wajumbe hao kuhakikisha wanarejea tena nchini baada ya mkutano, si kwa ajili ya mikutano pekee, bali pia kwa shughuli za utalii, biashara na maeneo mengine ya uwekezaji.
Amesema kuchaguliwa kwa Arusha kuwa mwenyeji wa mkutano huo kumeipa Tanzania nafasi ya kuwawezesha wageni kuona kwa macho yao vivutio vya utalii ambavyo awali walikuwa wakivisikia kupitia simulizi.
“Tunataka warejee tena, si kwa ajili ya mikutano pekee, bali pia kwa ajili ya utalii na shughuli nyingine,” amesema Dkt. Tulia.
Ameeleza kuwa mkutano huo pia ni sehemu ya kuimarisha diplomasia ya kibunge ya Tanzania, huku wajumbe kutoka mataifa mbalimbali wakipata nafasi ya kufahamu namna Tanzania inavyoendesha shughuli zake za kibunge na kushughulikia masuala ya kitaifa na kimataifa.
Katika hatua nyingine, Dkt. Tulia amesema Tanzania imechangia mabadiliko mbalimbali ya kanuni na taratibu za uendeshaji wa Umoja wa Mabunge Duniani katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake.
Amesema mabadiliko hayo yamewezesha Umoja huo kupata nafasi pana zaidi ya kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili dunia, tofauti na ilivyokuwa awali ambapo wakati mwingine wajumbe walilazimika kuchagua suala moja pekee kati ya masuala kadhaa yaliyokuwa yakihitaji kujadiliwa.
Dkt. Tulia ametolea mfano majanga yanayosababishwa na mabadiliko ya tabianchi katika maeneo mbalimbali duniani, akisema mfumo ulioboreshwa sasa unaruhusu mijadala kuhusu changamoto hizo kufanyika kwa upana bila kulazimika kuacha suala moja ili kujadili jingine.
Amesema mabadiliko hayo pia yameongeza nafasi ya kujadili masuala ya amani na usalama yanayoendelea katika maeneo mbalimbali duniani, ikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Sudan, Ukraine, Iran na maeneo mengine.
Kwa mujibu wa Dkt. Tulia, Tanzania inaona umuhimu wa mijadala hiyo kwa kuwa migogoro na changamoto za kiusalama katika baadhi ya maeneo zinaweza kuwa na athari kwa nchi nyingine na jamii ya kimataifa kwa ujumla.
Aidha, amesema Tanzania imechangia katika kukuza ushiriki wa wanawake ndani ya mabunge duniani, akieleza kuwa baadhi ya nchi ambazo awali hazikuwa na wanawake katika mabunge yao zimeanza kufanya mabadiliko baada ya juhudi za kuhamasisha ushiriki wao.
Dkt. Tulia amesema katika mkutano huo, ambao unatarajiwa kuwa na zaidi ya wageni 2,000, umewekwa utaratibu wa kuhakikisha wanawake na vijana wanashiriki, akieleza kuwa hatua hiyo inalenga kuhakikisha mijadala ya Umoja wa Mabunge Duniani inawakilisha makundi mbalimbali ya jamii.

.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...