•Asema maandalizi yamekamilika, washiriki zaidi ya 2,000 kuhudhuria kutoka mabunge 183

Na Vero Ignatus, Michuzi TV – Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, CPA Amos Gabriel Makalla, amemhakikishia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Balozi Anda Cristina Filip, kuwa Mkoa wa Arusha umekamilisha maandalizi ya kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani, unaotarajiwa kuanza Oktoba 5, 2026, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC).

Akizungumza leo, Alhamisi, Oktoba 1, 2026, alipokutana na Balozi Anda ofisini kwake jijini Arusha, RC Makalla amesema mkoa umejiandaa kwa muda mrefu kuhakikisha mkutano huo unafanyika kwa mafanikio ambapo Mkutano huo ni wa kihistoria kwa Tanzania kwa kuwa ni mara ya kwanza kuandaa mkutano huo wa kimataifa.

RC Makalla amesema kuwa usalama wa washiriki ni kipaumbele, akisisitiza taasisi mbalimbali zimeunganisha nguvu kuhakikisha maandalizi yote muhimu yanakamilika kwa wakati ambapo mkutano huo unatarajiwa kutoa fursa kwa wajumbe kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya kibunge na kuimarisha ushirikiano kati ya mabunge ya nchi wanachama.

Balozi Anda pia ameeleza matumaini yake kuwa mkutano huo utafanikiwa na washiriki watapata nafasi ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii nchini, hatua inayoweza kuwapa fursa ya kuifahamu Tanzania na vivutio vyake.

Kufanyika kwa mkutano huo jijini Arusha kunaipa Tanzania fursa ya kuandaa jukwaa muhimu la kidiplomasia na kibunge linalowakutanisha viongozi kutoka mataifa mbalimbali.

Kwa Arusha, maandalizi hayo yanaweka mkoa katika nafasi ya kupokea wageni wa kimataifa, huku mafanikio ya mkutano yakitarajiwa kutegemea ushirikiano wa taasisi husika, usalama na utekelezaji wa ratiba ya shughuli zilizopangwa.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...