Na Seif Mangwangi, Michuzi TV, Arusha
UJIO wa wajumbe wa Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Jijini Arusha umeibua fursa kwa wafanyabiashara na wasanii wa bidhaa za asili kutumia mkutano huo kutangaza utamaduni, sanaa na ubunifu wa Tanzania katika soko la kimataifa.
Mfanyabiashara wa bidhaa za asili, Jamila Akram, amesema kuwa uwepo wa wageni kutoka mataifa mbalimbali duniani ni fursa muhimu kwa Tanzania kuonyesha utajiri wake wa kiutamaduni kupitia bidhaa zinazozalishwa na Watanzania.
Amesema bidhaa za asili zinazopatikana Arusha zinabeba historia, utamaduni na ubunifu wa jamii mbalimbali nchini, hivyo wageni wanaofika kwa ajili ya mkutano huo wanapaswa kupata nafasi ya kuziona na kuzifahamu zaidi.
Kwa mujibu wa Mlinga, bidhaa hizo ni pamoja na mavazi, mashati, bidhaa za ngozi, kazi za mikono pamoja na bidhaa nyingine zinazotengenezwa kwa kutumia malighafi zinazopatikana nchini.
Amesema kupitia wageni hao, bidhaa za Tanzania zinaweza ni mwonekano mpana zaidi kimataifa, hasa pale wanapozinunua na kwenda nazo katika nchi zao kama kumbukumbu ya safari yao nchini.
“Tunawaona wageni wengi kutoka nchi mbalimbali na hii ni fursa kubwa ya kuwaonyesha kwamba Tanzania ina utamaduni na bidhaa nzuri.Wakienda nazo kwao, ni kama wamebeba sehemu ya Tanzania,” amesema Jamila.
Amesema wafanyabiashara wanapaswa kutumia fursa hiyo kwa kuhakikisha bidhaa zao zina ubora, ubunifu na zinawakilisha vyema utamaduni wa Tanzania ili kuwavutia wageni wa kimataifa.
Jamila amewataka wageni wanaoshiriki mkutano huo kutenga muda wa kutembelea maeneo mbalimbali yanayouza bidhaa za asili Jijini Arusha ili kujionea kwa karibu kazi zinazofanywa na wafanyabiashara na wasanii wa Tanzania.
Amesema Arusha ina nafasi kubwa katika kukuza utalii na biashara za bidhaa za asili kutokana na kuwa moja ya miji inayopokea wageni wengi wa kimataifa wanaokuja nchini kwa shughuli mbalimbali.
“Tunawakaribisha wageni wote waje waone bidhaa zetu. Tunataka watoke Tanzania wakiwa na kitu kinachowakumbusha utamaduni wetu na ubunifu wa Watanzania,” amesema.
Amesema matumizi ya bidhaa za asili na kazi za mikono yanapaswa kuendelea kupewa kipaumbele kwa kuwa yanawasaidia wasanii na wafanyabiashara wadogo kupata kipato na kuendeleza ujuzi wao.
Aidha, amesema matukio makubwa ya kimataifa kama Mkutano wa IPU yanaweza kusaidia kuwafungulia wafanyabiashara milango ya kupata masoko mapya nje ya Tanzania kupitia wageni wanaotembelea nchi.



.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...