Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Mhe. Ado Shaibu, imeridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, huku ikisisitiza kukamilishwa kwa miradi hiyo kwa wakati na kwa kuzingatia viwango vya ubora.

Leo, Oktoba 24,2026, Kamati hiyo imetembelea na kukagua miradi mbalimbali ya kimkakati, ikiwemo ujenzi wa barabara ya Mtwivila machinjio ya kisasa Ngelewala na Soko la kihesa kwa lengo la kufuatilia maendeleo ya utekelezaji wake.

Akizungumza baada ya ukaguzi, Mhe. Ado Shaibu amesema ameridhishwa na kasi ya utekelezaji na kutoa maelekezo kwa Halmashauri kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa wakati na inakidhi viwango vinavyotakiwa.

Ziara hiyo imehudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Kheri James; Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Mhe. Benjamin Sitta, Katibu Tawala wa Mkoa, Bi. Doris Kalasa; Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Bi. Zaina Mlawa; Mstahiki Meya wa Manispaa, Mhe. Ibrahim Ngwada; Katibu Tawala Wilaya, Ndg. Bernard Urassa, Wajumbe wa Kamati ya LAAC, pamoja na wakuu wa idara na vitengo wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa na wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...