Kamati ya Uchumi, Afya na Elimu ya Halmashauri ya Mji Mafinga ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri,Kaimu Mkurugenzi pamoja na Wakuu wa Idara wa Halmashauri imefanya Ziara katika Kata ya Wambi na kupongeza Maendeleo ya Ujenzi wa Kituo cha Afya cha Wambi.
Akiwasilisha ripoti ya Ujenzi wa Kituo hicho cha Afya, Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi Ndugu Eusebius Ngatunga amesema wamepokea Fedha za Ujenzi Kutoka Serikali kuu Tsh.Milioni Mia Tatu na hatua ya ujenzi inakaribia kukamilika kwa wakati ili kuwawezesha Wakazi wa Kata ya Wambi kupata huduma ya Afya.
Akizungumza katika Ziara hiyo Diwani wa Kata ya Wambi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi,Afya na Elimu Mhe.Frank Kalinga amesema anampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwatengea Fedha za Mradi kwa sababu ujenzi ukikamilika utasaidia kutatua changamoto za Afya kwa Wananchi wa Kata ya Wambi.
Naye kiongozi wa Ziara hiyo ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mhe.Regnant Kivinge amepongeza jitihada za Wananchi na kamati ya Ujenzi kwa ushirikiano na amewasihi waendelee kusimamia Mradi huo kwa weledi ili waweze kufikia Malengo.
Aidha,Diwani wa Viti Maalumu wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mhe.Dainess Msolwa amewapongeza Wananchi wa Kata ya Wambi kwa kutenga muda wao kusaidia shughuli za ujenzi pamoja na kushirikiana vyema na kamati ya Ujenzi kwa lengo la kukamilisha Jengo kwa wakati.
Sambamba na hayo,Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Ndugu Peter Ngussa amepongeza jitihada za ujenzi pia amewasisitiza kamati ya ujenzi ifikapo January 2027 ujenzi wa Kituo hicho uwe umekamilika ili huduma za awali za Afya zianze kutolewa kwa Wananchi wa Kata ya Wambi.


.jpeg)



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...