Na.Ashura Mohamed - Arusha

Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya amesema ndoto ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 haitafanikiwa kwa hotuba na maandiko,bali kwa usalama,Ubora na thamani ya fedha katika kila mradi wa ujenzi unaotekelezwa.

Mhandisi Kasekenya amesema hayo alipokuwa akifungua rasmi Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Sita wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) - AQ'26, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) ambapo alimwakilisha waziri wa Ujenzi Masanja Kadogosa.

Mkutano huo unafanyika kwa mada isemayo kujenga Tanzania Tunayoitaka Kuelekea 2050, Kuimarisha Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa kwa Mazingira Endelevu ya Ujenzi.

"Tanzania ya Mwaka 2050 haitajengwa Mwaka 2050. Inajengwa leo kupitia maamuzi tunayofanya, wataalamu tunaowaandaa, teknolojia tunazotumia na miradi tunayoitekeleza," alisema Kasekenya.

Aidha alipongeza AQRB kwa kusajili miradi 1,947 na kufanya ukaguzi wa miradi 6,274 katika mikoa 26 ya Tanzania Bara kwa mwaka wa fedha 2025/26, lakini akasisitiza kuwa usalama wa majengo si hiari.

"Usalama wa majengo si jambo la hiari; ni wajibu wa kisheria, kitaaluma na kimaadili. Natoa wito kwa taasisi za Serikali, Halmashauri na wawekezaji kuhakikisha miradi inasajiliwa na kusimamiwa na wataalamu wenye usajili halali," alisisitiza.

Kasekenya alisema Tanzania haiwezi kufikia Dira 2050 kwa kutegemea mbinu za zamani. Aliitaka sekta ya ujenzi kutumia Akili Unde (AI), mifumo ya kidijitali na Building Information Modelling (BIM) kwa vitendo.

Kwa Upande wake Kaimu Msajili wa (AQRB) Dkt.Daniel Matondo katika mwaka wa fedha 2025/2026 bodi imeendelea kuimarisha usajili na ukaguzi wa miradi ya ujenzi ili kuhakikisha kuwa uzingatiaji wa sheria na viwango vga ubora kwa usalama wa wananchi.

Aidha kuhusu ajira kwa vijana kupitia Programu ya Mafunzo kwa Vitendo kwa Wahitimu (AQIP) ambapo wahitimu 1,866, ambapo 1,163 waliwezeshwa na Serikali na 703 kupitia sekta binafsi.

Mkutano huo umehudhuriwa na wabunifu wa majengo,wakadiriaji majenzi,wahandisi,wataalamu na wadau wote wa sekta ya ujenzi ambapo itakapofika mwaka 2027 AQRB itaadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwake









Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...