Na Victor Masangu, Bagamoyo

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Pwani imekutana na wadau wa Forodha, wakiwemo wafanyabiashara wanaojihusisha na uingizaji na usafirishaji wa mafuta ya kupikia kupitia Bandari ya Bagamoyo, kwa lengo la kusikiliza changamoto zao na kujadili namna ya kuzipatia ufumbuzi.

Kikao hicho kilichofanyika katika Ofisi za TRA Wilaya ya Bagamoyo ni sehemu ya juhudi za mamlaka hiyo kuimarisha ushirikiano na wadau wa Forodha, kuboresha mawasiliano na kuweka mazingira rafiki kwa shughuli halali za biashara.

Akizungumza katika kikao hicho, Meneja wa TRA Mkoa wa Pwani, Peter Jackson, amesema mamlaka hiyo itaendelea kusimamia sheria na taratibu za Forodha huku ikiweka mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara wanaozingatia sheria.

Amesema udhibiti wa bidhaa za magendo unafanyika kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Serikali, huku akisisitiza umuhimu wa kutoa elimu ya kodi na Forodha kwa wafanyabiashara ili kuongeza uelewa na uzingatiaji wa sheria.

Kwa upande wao, baadhi ya wafanyabiashara wameishukuru TRA Mkoa wa Pwani kwa kuwapa nafasi ya kuwasilisha changamoto zao na kujadiliana njia za kuzitatua.

Wamesema mazungumzo hayo yameimarisha mawasiliano na ushirikiano kati yao na TRA, huku wakitoa matumaini ya kuendelezwa kwa mikutano hiyo ili changamoto zinazojitokeza katika shughuli zao za biashara zipatiwe ufumbuzi kwa wakati.





Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...