Na Said Mwishehe

HIYOOO LINI HIYOOOO? HIyo leo hiyooo!Hayo yalikuwa sehemu ya misemo iiyokuwa ikitumiwa na wakiambiaji wa mbio za pole maarufu Jogging walipokuwa wakipita katika mitaa mbalimbali ya Jiji ya Dar es Salaam leo Oktoba 11,2026.

Mbio hizo za pole zilizopewa jina la City to City zimeshirikisha washiriki zaidi ya 6500 kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam pamoja na mikoa mbalimbali ikiwemo ya Lindi,Mtwara,Morogoro na Dodoma.

Shirikisho la Joging Ilala(IJA)ambalo linahusisha jongongi zote za Wilaya ya Ilala chini ya mlezi wao Mkuu wa Wilaya hiyo Edward Mpogolo ndio ilikuwa mwenyeji na kauli mbiu yao inasema hivi AMANI NA AFCON SALAMA.

Washiriki walikuwa na vaibu la kufa mtu na walianza mbio hizo Viwanja Vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mpogolo,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Saaam Elihuruma Mabyela pamoja na Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Charangwa Selemani.

Mbio hizo zilizokuwa na burudani kutoka kwa washiriki hao ziligeuka kuwa kivutio kwa waliokuwa kando Kando ya barabara ambayo ilitumika kutoka Mnazi Mmoja kuelekea Upanga katika Hospitali ya Agha Khan na kisha barabara inayopita katika ufukwe wa Bahari ya Hindi na baadae Posta Mpya katika Mtaa wa Azikiwe na kisha Samora na kurejea Mnazi mmoja.

Kulikuwa kumenoga sana hasa kutokana na nyimbo zilizokuwa zinaimbwa na wana-Joga ndio zilifanya hakuna aliyechoka.Washiriki kutoka Mtwara wenyewe waliamua kuwa na ngoma kabisa na jinsi wanavyojua kuzipiga …acha kabisa.Ile nyimbo ya Libasee Motooo leo ilipogwa live.

Na ule ushindi wa Simba dhidi ya mtani wake Yanga ndio kabisa wale wenye mahaba na Simba wakawa wamefurahi mnooo.Ilala leo kulinoga ,wingi wa washiriki ulifanya kuwe na msusuru mrefu wa wakiambiaji.

Wakiwa katika Uwanja wa Mnazi mmoja baada ya washiriki kumaliza mbio na kufanya mazoezi ya kupasha misuli ndipo sasa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Elihuruma Mabelya na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo walipozungumza na washiriki hao kwanza kwa kuwapongeza kwa ushiriki wao.

Lakini ujumbe mkubwa wa Mabelya na Mpogolo kwa wana joging hao ni kuhakikisha sasa wanaanza kutumia klabu za joging kuzungumza na kupanga jinsi ya kujiinua kiuchumi kuelekea Dira ya 2050 ambayo inaeleza ifikapo mwaka 2050 kila Mtanzania awe na kipato cha dola 1000 kwa siku.

Hivyo wana joging wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na wana Joga wote ni wakati wa kupanga namna ya kutumia fursa zinazotolewa na Serikali ikiwemo mikopo kuchangamkia fursa hizo ili nao kuwa sehemu ya wanuifaka.

Pia wamehimizwa kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele katika kulinda amani yetu ambayo ni Tunu ya Taifa la Tanzania na kwamba utulivu wa nchi ndio unaowezesha kila Mtanzania kushiriki katika Ujenzi wa Taifa letu nzuri la Tanzania chini ya uongozi mahiri wa Rais wetu Dk.Samia Suluhu Hassan.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...