Na Victor Masangu,Kibaha

Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe.Silvestry Koka katika kuweka mikakati ya kuboresha sekta ya elimu na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi amekuja na kampeni kabambe aliyoipa jina la Tokomeza zero punguza divisheni 4.

Mh.Koka ametoa kauli hiyo wakati wa mahafali ya nne ya kuhitimu wanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari picha ya ndege iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha.

Aidha Koka amebainisha kwamba lengo lake atashirikiana bega kwa bega na wazazi na walezi katika kuweks misingi imara ambayo itasaidia wanafunzi kuweza kuongeza kasi ya ufaulu.

"Mimi kama mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini katika kukuza sekta ya elimu nimeona kuja na kampeni maalumu ambayo itakwenda kwa jina la Tokomeza zero punguza divisheni four.,"amebainisha Mhe.Koka.

Aidha Koka akijibu risala iliyosomwa na mwalimu mkuu shule hiyo ameahidi kutoa mashine ya kutoa nakala ( Photocopy mashine) pamoja na mashine ya printer lengo ikiwa ni kukuza sekta ya elimu na kuongeza kasi ya ufaulu kwa wanafunzi.

Pia amesema ataendelea kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha na wadau wa maendeleo katika kuendeleza masomo ya sayansi kwa wanafunzi kwa kuboresha vifaa mbali mbali katika maabara katika shule hiyo ya sekondari picha ya ndege.

Katika hatua nyingine Mbunge huyo amechangia kiasi cha shilingi laki tano ambazo zitaweza kusaidia katika mahitaji mbali mbali ya shule hiyo.

Naye Mwalimu mkuu wa shule hiyo Omary Mtaka amemshukuru kwa dhati Mbunge huyo kwa kuweza kusapoti kwa hali na kuchochea maendeleo katika shule hiyo.

Jumla ya wanafunzi wapatao 188 wameweza kuhitimu kidato cha nne katika shule ya sekondari picha ya ndege iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...