
KAMPUNI ya ubashiri ya Meridianbet imeendelea kutekeleza dhamira yake ya kurudisha kwa jamii kupitia mpango wake wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR), kwa kukabidhi vifaa vya usafi wa mazingira kwa Mama Lishe na Baba Lishe katika Kata ya Mbezi Juu, jijini Dar es Salaam.
Zoezi hilo limefanyika kwa kushirikiana na Diwani wa Kata ya Mbezi Juu, Anna Lukindo, likiwa na lengo la kuhamasisha usafi wa mazingira, utunzaji wa taka na kuimarisha mazingira bora na salama kwa wafanyabiashara wa chakula pamoja na wananchi wanaowahudumia kila siku.
Kupitia msaada huo, Meridianbet inalenga kuwasaidia Mama Lishe na Baba Lishe kuwa na maeneo safi ya kufanyia biashara zao kwa kuweka taka katika sehemu maalumu badala ya kuzitupa ovyo, hatua inayoweza kuchangia kupunguza uchafuzi wa mazingira na kuboresha afya ya jamii.
Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya MERIDIANBET au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Akizungumzia msaada huo, Nancy Ingram kutoka Meridianbet amesisitiza umuhimu wa kushirikiana na viongozi wa maeneo husika pamoja na makundi mbalimbali ya kijamii katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi na kuendeleza mazingira bora kwa wote.
Kwa upande wake, ushirikiano na Diwani wa Kata ya Mbezi Juu, Anna Lukindo, unaonesha umuhimu wa kuunganisha nguvu za sekta binafsi na uongozi wa serikali za mitaa katika kuhamasisha maendeleo ya jamii na utekelezaji wa mipango yenye manufaa kwa wananchi.
Meridianbet inaamini kuwa usafi wa mazingira ni jukumu la kila mmoja. Hivyo, kampuni inatoa wito kwa Mama Lishe, Baba Lishe na wananchi kwa ujumla kutumia vifaa hivyo ipasavyo, kutunza mazingira yanayowazunguka na kuendeleza utamaduni wa kuweka taka katika maeneo maalumu.
Kupitia mipango yake ya CSR, Meridianbet inaendelea kuonesha dhamira yake ya kuwa sehemu ya jamii na kuchangia maendeleo endelevu kwa kuunga mkono juhudi zinazolenga kuboresha ustawi wa wananchi.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...