Jitihada za kutumia uandishi wa habari kuchochea ukuaji wa uchumi na kuunga mkono maendeleo nchini zimepewa kipaumbele katika kongamano la wadau wa habari lililoandaliwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA Tanzania) jijini Mwanza.
Kongamano hilo lililofanyika Oktoba 12, 2026, chini ya kaulimbiu "Uhuru wa Vyombo vya Habari Kiuchumi", liliwashirikisha wanachama 60 wa MISA kutoka Kanda ya Ziwa, Magharibi na Kati, pamoja na wadau kutoka taasisi za umma na sekta binafsi.Kama muendelezo wa kongamano hilo, wanachama hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa MISA Tanzania, Edwin Soko, wamefanya ziara ya kutembelea miradi ya kimkakati Oktoba 13, 2026, ikiwemo Daraja la John Pombe Magufuli (Kigongo-Busisi) na mradi wa ujenzi wa meli ya kisasa ya MV New Mwanza katika Bandari ya Mwanza.
Akizungumza wakati wa ziara, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa TASHICO, Abdulrahman Ally, amesema MV New Mwanza ni kichocheo muhimu cha uchumi kwani itaboresha usafiri wa abiria na mizigo na kuchochea biashara katika Ukanda wa Ziwa na nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Naye Mwenyekiti wa MISA Tanzania, Edwin Soko, amesema ziara hiyo inalenga kuwawezesha waandishi kujionea uwekezaji wa Serikali ili waweze kuhabarisha umma kwa taarifa sahihi.
Amesema waandishi wana wajibu wa kuwa mabalozi wa maendeleo kwa kuelimisha wananchi kuhusu mchango wa miradi hiyo katika kuboresha maisha na kukuza uchumi wa Taifa.


.jpeg)
.jpeg)



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...