Na Said Mwishehe,Michuzi TV


WASHIRIKI wa Kongamano la kimataifa la Vyama vya Ushirika vya Akiba na Mikopo Barani Afrika(SACCA) wamesema kongamano hilo limekufa fursa muhimu ya kuwaongezea maarifa viongozi wa vyama hivyo.

Wakizungumza leo Oktoba 13,2026 wakati wa kongamano hilo linaloendelea katika Ukumbi wa mikitano wa Kimatata Julius Nyerere jijini Dar es Salaam washiriki hao wamesema kupitia kongamano kuna mada mbalimbali znazotolewa ambazo kwa sehemu kubwa zinawajengea uelewa na maarifa kuhusu usimamizi bora wa vyama vya ushirika.

Akizungumza kuhusu kongamano hilo ambalo limeshirikisha washriki zaidi ya 600 , Mwenyekiti wa Chama cha Akiba na Mikopo (SACCOS) cha Kinole kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Hasira Zahoro ambaye ni miongoni mwa washiriki amesema limekuwa fursa katika kuwaongezea viongozi wa vyama hivyo maarifa ya uongozi na usimamizi bora.

“Katika kongamano hili kumekuwa na mijadala mbalimbali inayotolewa na wawezeshaji waliobobea katika vyama vya ushirika na hivyo imetusaidia viongozi kubaini mapungufu yaliyopo na namna ya kuyatatua ili kufikia malengo yaliyowekwa hasa kwenye kuboresha mifumo ya uongozi na usimamizi wa watendaji.

Ameongeza kupitia mafunzo yanayohusu uongozi na kuimarisha mifumo ya uongozi, amepata maarifa mapya kuhusu umuhimu wa kufanya tathmini kabla ya kuchukua hatua, kutambua mahitaji ya taasisi na kuweka mikakati inayolenga kutatua changamoto zilizopo.

Pia amesema mijadala hiyo imewajengea uwezo wa kutathmini utendaji wa wafanyakazi, kuendesha mchakato wa ajira, kubaini changamoto za kiutendaji na kutafuta suluhisho, pamoja na kuweka mazingira yatakayowafanya watendaji kuwa na imani na taasisi wanazozifanyia kazi.

Zahoro amesema SACCOS ya Kinole ina wanachama wengi ambao ni wakulima na wajasiriamali wakiwemo vijana, hivyo kuboresha uongozi na usimamizi wa chama hicho kutasaidia kuimarisha utoaji wa huduma na kuchochea maendeleo ya wanachama.

Ametumia hiyo kutoa shukrani kwa taasisi za SCALT, TCDC pamoja na Serikali kwa kuwezesha kufanyika kwa kongamano hilo huku akisisitiza kila chama kitakachoshiriki kongamano hilo kupitia mwakilishi wake kitapata maarifa yatakayosaidia kuboresha shughuli za vyama vya ushirika.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...