Na Jane Mwakyoma
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amewataka vijana nchini kutosubiri fursa mpya za kiuchumi, bali kutumia rasilimali zinazowazunguka kujiajiri, kuongeza kipato na kuchangia maendeleo ya Taifa, huku akisisitiza umuhimu wa kuzalisha bidhaa bora zenye ushindani sokoni.
Prof. Mkenda alitoa wito huo jana alipomwakilisha Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, katika ufunguzi wa maonesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa yaliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Ndua, Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, mkoani Rukwa.
Alisema maadhimisho hayo yanatoa nafasi kwa vijana kutoka vijijini, mijini na visiwani, wakiwemo wenye na wasio na ulemavu pamoja na wenye viwango tofauti vya elimu, kukutana, kubadilishana mawazo na kujifunza namna ya kutumia rasilimali zilizopo katika maeneo yao kujiletea maendeleo.
Prof. Mkenda alitaja kilimo, uvuvi, biashara na uchumi wa buluu kuwa miongoni mwa sekta zenye fursa za kiuchumi kwa vijana, akiwataka kujifunza ujuzi wa biashara, kutambua mahitaji ya soko na kutumia teknolojia za kidijitali kupata taarifa za fursa na kupanua masoko ya bidhaa zao.
Profesa Mkenda alisema kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2022 , Tanzania ilikuwa na vijana 21,312,411 wenya umri wa miaka 15 hadi 35 sawa na asilimia 34.5 ya watu wote nchini alisisitiza kuwa vijana ni rasilimali muhimu katika maendeleo ya Taifa.
Alisema kiwango cha ukosefu wa ajira. kimepungua kutoka asilimia 8.3 mwaka 2024 hadi asilimia 7.5 mwaka 2025, lakini bado kuna haja ya kuongeza ajira na kuwawezesha vijana kujiajiri na kukuza biashara zao.
Aidha alisema serikali imeongeza kiwango cha fedha zinazotengwa na halmashauri kwa ajiri ya mikopo na uwezeshaji wanawake,vijana na watu wenye ulemavu kutoka asilimia 10 hadi asilimia 15 katika mwaka wa fedha 2026/27.
Aidha aliwataka vijana kutumia ubunifu, maarifa na ujuzi walionao kuchangamkia fursa za kiuchumi zinazopatikana katika maeneo yao kujikwamua kiuchumi,kujiajiri na kuchangia maendeleo ya Taifa.
Prof. Mkenda alizitaka Taasisi za serikali,mashirika binafsi,watendaji wa kata wanaohusika na maendeleo ya vijana kuhakikisha Taarifa za fursa zinawafikia walengwa kwa wakati na usahii,huku mafunzo yakitolewa ili kuwawezesha kutumia mifumo ya Kidijitali na majukwaa ya uwezeshaji kiuchumi.
Awali akiongea na vijana hao waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana Joel Nanauka alisema serikali itaendelea kuwawezesha vijana kwa kuwapatia elimu kuhusu viwanda,kuongeza thamani bidhaa wanazozalisha na namna ya kupata masoko ya bidhaa zao.
Alisema maadhimisho hayo yanaweka mkazo katika wajibu wa vijana kutambua fursa na kutumia ujuzi walionao sambamba na wajibu wa serikali na Taasisi za uwezeshaji kuhakikisha mitaji,mafunzo na masoko yanapatikana kwa wakati ili kuchochea ajira na ukuaji wa uchumi.
Aidha alisema kaulimbiu ya maazimisho ya wiki la vijana kitaifa"Mazingira Tofauti,Fursa sawa kwa vijana" imezingatia wakati uliopo katika ukuaji wa Teknolojia duniani.
Pia alimshukuru Rais wa awamu ya sita,Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuweka mazingira rafiki kwa vijana yanayowawezesha kupata fursa za kiuchumi na kushiriki katika maendeleo ya Taifa.
Kwa upande wao vijana walisema ni wakati wa kutambua fursa za maendeleo katika mazigira wanayoishi kuliko kusubili ajira katika sekta mbalimbli na huku wakiiomba serikali kuendelea kuongea lugha moja na Taasisi za kibenki kuhakikisha wanatoa mikopo kwa vijana kwa liba nafuu ili kila kijana wa kitanzania kupata mkopo kwa mashariti nafuu.
"Vijana kinachotukwamisha ni mitaji,tunaiomba serikali wakae na mabenki walegeze mashariti siyo kila kijana anamali isiyohamishika wengine ndiyo kwanza ametoka kumaliza shule,tunaomba mabenki watoe mikopo kwa vijana kwa mashariti nafuu" walisema.

.jpeg)

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...