Benki ya NMB imeondoa ada za miamala kupitia mfumo wake mpya wa NMB Direct kwa siku 90, kuanzia Oktoba 5 hadi Desemba 31, 2026, hatua inayohusisha malipo ya pamoja, uhamishaji wa fedha ndani na nje ya nchi pamoja na malipo ya bili.
Hatua hiyo ni sehemu ya maboresho matatu yaliyotambulishwa wakati wa Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026, yakiwamo kuanzishwa kwa dawati maalumu la kuwahudumia wateja wenye ulemavu na huduma ya Self-Reversal kupitia NMB Mkononi App na USSD.Mkuu wa Kitengo cha Benki kwa Wateja Binafsi wa NMB, Filbert Mponzi, alisema dawati hilo litatoa msaada maalumu kwa wateja wenye ulemavu wa kusikia, kuona na viungo, huku wenye ulemavu wa kusikia wakiwezeshwa kupata huduma kwa video inayotumia lugha ya alama.
Kupitia Self-Reversal, wateja wataweza kuanzisha wenyewe maombi ya kurejesha miamala inayostahili bila kulazimika kupiga simu benki au kufika tawi, hatua inayolenga kuongeza urahisi na uwezo wa mteja kupata huduma kupitia teknolojia.



.jpeg)







Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...