Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linafanya uchunguzi wa kifo cha kijana Dotto Alex (19) kilichotokea baada ya kushambuliwa kwa kitu butu kichwani.
Tukio limetokea Oktoba 6, 2026 majira ya saa 7 usiku, eneo la Lwamgasa, Wilayani Geita, wakati marehemu akiwa kwenye burudani ya disko.
Kwa mujibu wa taarifa za awali, marehemu alishambuliwa na mtu ambaye alitoweka eneo la tukio. Alijeruhiwa na kukimbizwa Hospitali ya Rufaa Geita kisha kuhamishiwa Bugando Mwanza ambako alifariki Oktoba 7.
Polisi wamesema uchunguzi unaendelea na msako wa mtuhumiwa unafanyika, huku wakiomba wananchi wenye taarifa kusaidia.




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...