Na Seif Mangwangi, Michuzi TV, Arusha

Msanii wa muziki wa bongo flava nchini Raymond Mwakyusa maarufu kama ‘Rayvanny’ anatarajiwa kutumbuiza wajumbe wa mkutano wa 153 wa kimataifa wa Mabunge Duniani ulioanza Leo Oktoba5, 2026 Jijini Arusha.

Akizungumza mara baada ya kutua katika uwanja mdogo wa ndege wa Arusha uliopo kisongo, Msanii huyo amesema amekuja kuwaonyesha wageni wanaoshiriki mkutano huo utajiri ambao Tanzania inao kupitia muziki.

Amesema ni fursa na heshima kubwa ambayo amepewa kuwa mmoja wa watumbuizaji katika mkutano huo pamoja na uwepo wa wasanii wengi nchini lakini yeye ndio kapewa nafasi hiyo.

“ Nina furaha sana ya kupata nafasi ya kutumbuiza wageni katika mkutano wa kimataifa wa Mabunge Duniani, niwaahidi tu kuwa burudani nitakayoitoa itaacha historia Tanzania,” ameahidi Rayvanny.

Mkutano wa 153 wa umoja wa Mabunge Duniani umeanza Leo Oktoba 5 , 2026 Jijini Arusha ukiwa ni mara ya kwanza tangu kuanzishwa Kwa umoja huo Duniani.

Katika mkutano huo ambapo masuala mbalimbali yatajadiliwa ikiwemo ajenda za watoto, wanawake, vijana na makundi maalum aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Tulia Ackson atamaliza muda wake kama Rais wa Jumuiya ya Mabunge Duniani.

Spika Dkt Tulia Ackson allichaguliwa kuwa Rais wa 31 wa IPU, Oktoba 27, 2023 katika Mkutano wa 147 wa IPU, uliofanyika katika mji wa Luanda nchini Angola na hivyo kuongoza Jumuiya hiyo Kwa miaka mitatu.

Aidha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mkutano huo wa kimataifa.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...