Na FARIDA MANGUBE, MOROGORO
Viongozi wa kampuni mbalimbali waliohitimu Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) wamekutana na uongozi wa chuo hicho katika jukwaa la kujadili fursa za ushirikiano na namna ya kuwaandaa wanafunzi na wahitimu kuwa na ujuzi unaokidhi mahitaji ya soko la ajira.
Katika jukwaa hilo, uongozi wa SUA umewataka viongozi hao kutumia nafasi zao kuwapa wanafunzi fursa za kupata uzoefu wa vitendo kupitia miradi na shughuli mbalimbali hatua inayolenga kuwaongezea uwezo wa kushindana katika soko la ajira na kujiajiri.
Akizungumza katika mjadala huo, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo anayeshughulikia Fedha, Mipango na Utawala, Profesa Mulid Mwatawala, alisema ushirikiano kati ya SUA, wahitimu wake na sekta binafsi ni muhimu katika kuhakikisha wanafunzi wanapata ujuzi unaoendana na mazingira halisi ya kazi.
Profesa Mwatawala alisema chuo kitawaunganisha wanafunzi na viongozi hao wa kampuni ili waweze kupata fursa za kujifunza na kupata uzoefu katika maeneo mbalimbali ya uzalishaji na uendeshaji wa biashara.
Aidha, aliwataka viongozi hao kutenga muda wa kuwafundisha wanafunzi namna bora ya kubuni miradi na kusimamia mawazo yao ya kibunifu hadi kuyafikisha katika hatua ya uzalishaji na hatimaye sokoni.
Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Kilimo Biashara kutoka NMB Makao Makuu, Bw. Nsolo Mlozi, alisema benki hiyo imetenga Sh bilioni 20 kwa ajili ya kuendeleza miradi anzilishi ya vijana na makundi maalum.
Alisema uwezeshaji wa miradi hiyo una umuhimu mkubwa katika kukuza uchumi wa Taifa, huku ukiwapa wahitimu fursa ya kupata uzoefu katika uzalishaji na uendeshaji wa biashara.
"Miradi anzilishi pamoja na kuchangia katika uchumi wa Taifa, pia inasaidia wahitimu kupata uzoefu katika uzalishaji na uendeshaji wa biashara," alisema Mlozi.
Kabla ya kuanza kwa jukwaa hilo, viongozi hao walifanya ziara ya kujionea shughuli na miradi mbalimbali inayotekelezwa na SUA, ikiwa ni sehemu ya kupata uelewa wa shughuli zinazofanyika chuoni hapo na kubaini maeneo ambayo wanaweza kushirikiana na chuo.
Katika ziara hiyo, viongozi hao walipata fursa ya kufuatilia maelezo kuhusu utekelezaji wa Mradi wa APOPO pia walitembelea eneo kinapojengwa kiwanda cha uzalishaji wa bidhaa mbalimbali za SUA, ikiwemo maji na sharubati (juisi), pamoja na majengo yanayotekelezwa kupitia Mradi wa Higher Education for Economic Transformation (HEET).

.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...