BENKI ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imetunukiwa tuzo ya Ubora katika Suluhisho za Ufadhili wa Kilimo Tanzania katika tuzo za Global Brand Awards, zilizofanyika Dubai hivi karibuni

Tuzo hiyo inatambua juhudi za TADB katika kuendeleza suluhisho bunifu za kifedha kwa sekta ya kilimo, ikiwemo ufadhili wa kijani, unaolenga kukuza uwekezaji endelevu na kuimarisha uwezo wa sekta ya kilimo kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Frank Nyabundege, alisema tuzo hiyo itaendelea kuhamasisha benki kubuni na kutoa suluhisho za kifedha endelevu zinazochochea mageuzi ya kilimo na kuchangia utekelezaji wa malengo ya Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2050.

Tuzo hiyo ilipokelewa kwa niaba ya TADB na Frank Nyabundege, Mkurugenzi Mtendaji; Mkani Waziri, Mkurugenzi wa Mipango, Ushauri na Mahusiano ya Taasisi; na Irene John, Meneja wa Masoko, Huduma kwa Wateja na Mahusiano ya Taasisi.



Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...