Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) imeendelea kutoa elimu kwa wakulima kuhusu umuhimu wa kutumia mbegu bora, ikieleza kuwa hatua hiyo ni msingi wa kuongeza uzalishaji wa mazao na kuimarisha usalama wa chakula nchini.
Akizungumza Oktoba 12, katika Maonesho ya Siku ya Chakula Duniani yanayofanyika kuanzia Oktoba 10 hadi 16, 2026, mkoani Tanga, Aleti Kibalazo, Mtafiti na Mkaguzi wa Mbegu kutoka TOSCI, amesema matumizi ya mbegu bora ni hatua muhimu katika kuhakikisha wakulima wanazalisha chakula cha kutosha na chenye ubora.
Kibalazo amesema usalama wa chakula unaanzia kwenye mbegu bora, akieleza kuwa bila kuhakikisha wakulima wanatumia mbegu zinazokidhi viwango, jitihada za kuongeza uzalishaji wa chakula haziwezi kufikia matokeo yanayotarajiwa.
Amesema Serikali imewekeza katika tasnia ya mbegu, huku TOSCI ikiendelea na mikakati ya kuhakikisha mbegu bora zinapatikana kwa wingi, zinawafikia wakulima kwa urahisi na zinakuwa na gharama nafuu.
Ameeleza kuwa mikakati hiyo inazingatia mambo matatu muhimu yanayojulikana kama A3, ambayo ni Availability (upatikanaji wa mbegu), Accessibility (urahisi wa kuzipata) na Affordability (uwezo wa wakulima kumudu gharama zake).
Kwa mujibu wa Kibalazo, upatikanaji wa mbegu pekee hautoshi iwapo wakulima wanashindwa kuzifikia kutokana na umbali au gharama za usafiri. Hivyo, TOSCI inaendelea kusajili mawakala wa kusambaza mbegu hadi vijijini ili kurahisisha upatikanaji wake na kupunguza muda na gharama ambazo wakulima hutumia kuzitafuta.
Amesema kuongezeka kwa upatikanaji wa mbegu bora kunatarajiwa kusaidia wakulima kuzipata kwa urahisi zaidi, huku ongezeko la upatikanaji na matumizi yake likitarajiwa kuchangia kupunguza gharama kulingana na hali ya soko na mahitaji.
Kibalazo amesema TOSCI inaendelea kutoa elimu moja kwa moja kwa wakulima kupitia maonesho na kampeni mbalimbali ili kuwajengea uelewa kuhusu umuhimu wa kutumia mbegu zinazokidhi viwango, amesisitiza kuwa elimu hiyo haihusu mbegu za zao moja pekee, bali inajumuisha mazao mbalimbali, pamoja na miche na vipando.
Amesema kwa mwaka 2026, TOSCI imeweka makadirio ya matumizi ya mbegu bora kufikia tani 120,000, na hadi sasa kiwango kilichofikiwa tayari kimevuka nusu ya lengo hilo. Kwa muda mrefu, taasisi hiyo inalenga matumizi ya mbegu bora kufikia tani 250,000 ifikapo mwaka 2030.
Ameeleza kuwa maendeleo hayo yanahusishwa na kampeni zinazoendelea za kuhamasisha matumizi ya mbegu bora, huku ushiriki wa TOSCI katika Maonesho ya Siku ya Chakula Duniani ukiwa sehemu ya juhudi za kukutana na wakulima moja kwa moja, kuwapatia elimu na kuwahamasisha kutumia mbegu bora katika shughuli zao za kilimo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...