-Ni waandishi waliokuja katika ziara kuangalia maandalizi ya AFCON na fursa za utalii


Na Mwandishi Wetu


MWANDISHI wa habari na mtengeneza maudhui kutoka nchini Ufaransa, Alizee Morat ameonesha mshango wake kuwa hakuwahi kufikiria kuwa Tanzania ni ya kisasa.

Ameonesha mshangao huo kibaada ya kutembelea Tanzania katika ziara inayolenga kuangazia maandalizi ya AFCON na fursa za utalii.

Alizee , ambaye amewahi kutembelea nchi mbalimbali za Afrika, ikiwemo Cameroon, amesema amevutiwa na miundombinu ya Uwanja wa Benjamin Mkapa utaokatumika kwenye mashindano, na ukarimu wa Watanzania, akisema uzoefu wake nchini umekuwa tofauti na matarajio yake.

Ziara hiyo imehususisha pia Waandishi nguli wa michezo Kitila mataita mbalimbali ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Tanzania kutumia AFCON kama jukwaa la kuitangaza nchi kimataifa, huku kundi la watu mashuhuri, waandishi wa habari na watengeneza maudhui likitembelea maeneo mbalimbali nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari, Ofisa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Nassor Garamatatu, amesema kundi hilo limekuja kujionea maandalizi ya Tanzania na kutumia vyombo vyao vya habari pamoja na majukwaa ya kidijitali kuufahamisha ulimwengu kuhusu utayari wa nchi.

Wageni hao wametembelea Uwanja wa Benjamin Mkapa na Uwanja wa Gymkhana utakaotumika kwa ajili ya mazoezi wameeleza kuridhishwa na uwekezaji uliofanyika katika miundombinu ya michezo.

Kwa mujibu wa Garamatatu, kupitia ziara hiyo Tanzania inalenga kupata matangazo ya kimataifa yatakayosaidia kuwafikia watalii na wadau wa michezo kutoka sehemu mbalimbali duniani.

“Mbali na Dar es Salaam, kundi hilo linatarajiwa kutembelea Arusha na Fumba Zanzibar, likilenga kujionea vivutio na maandalizi ya AFCON, “ amesema.

Kwa upande wake Kiongozi wa msafara huo, John Jackson, amesema Wizara ya Maliasili na Utalii imeamua kutumia umuhimu wa AFCON kuwaunganisha wageni hao na vivutio vya Tanzania ili watumie majukwaa yao kuitangaza nchi.

Jackson amesema walifurahishwa na Uwanja wa Benjamin Mkapa, wakilinganisha uwekezaji wake na viwanja vikubwa duniani.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...