Wadudu wana mchango mkubwa katika uhifadhi wa wanyamapori, ambao ni rasilimali muhimu kwa utalii endelevu. Wadudu huchavusha mimea kwa zaidi ya asilimia 75, hurutubisha udongo, hutawanya mbegu na kusaidia kuota kwake, ni viashiria vya afya ya mfumo ikolojia na chakula cha baadhi ya wanyamapori.  

TAWIRI, kupitia maabara yake ya wadudu, imekusanya zaidi ya spishi 1,000 za wadudu, ikiendeleza tafiti na elimu kuhusu kundi hili muhimu la viumbe hai ambalo limepewa kipaumbele kidogo katika tafiti, licha ya mchango wake katika uhifadhi wa bioanuai. Duniani, zaidi ya spishi milioni moja za wadudu zimegunduliwa na kurekodiwa na wanasayansi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...