Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Zimbabwe, Kamishna wa Polisi (CP) Suzan Kaganda, amehitimisha mafunzo ya Lugha ya Kiswahili kwa wageni yaliyowashirikisha raia 15 wa Zimbabwe, katika kipindi cha Oktoba hadi Novemba 2026, chini ya uratibu wa Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini humo.

Mafunzo hayo ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kukuza, kueneza na kuimarisha matumizi ya Kiswahili kimataifa, kwa kutambua umuhimu wa lugha hiyo katika kuunganisha watu, kurahisisha mawasiliano, kuimarisha diplomasia na kukuza ushirikiano baina ya mataifa.

Kupitia ushirikiano na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi, Serikali imeendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha Kiswahili kinazidi kupata nafasi katika mataifa mbalimbali duniani, sambamba na hadhi yake ya kimataifa na kutambuliwa na UNESCO kama lugha yenye umuhimu mkubwa katika kukuza utamaduni, mawasiliano na mshikamano wa kimataifa.

Wahitimu wa mafunzo hayo, ambao wanatoka katika Shirika la Kikanda la Afrika la Haki Miliki (ARIPO) na Kitengo cha Diplomasia cha Jeshi la Polisi (Diplomatic Police), wamekabidhiwa vyeti vya ushiriki na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Bw. Aristides Mbwasi, ambaye yupo nchini Zimbabwe kushiriki Mkutano wa 23 wa Makatibu Wakuu wa Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA).

Hafla ya kukabidhi vyeti hivyo imefanyika katika ukumbi wa Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, mjini Harare, Zimbabwe, ikiwa ni sehemu ya kuhitimisha mafunzo hayo na kutambua ushiriki wa wahitimu katika kujifunza lugha ya Kiswahili, ambayo inaendelea kuwa nyenzo muhimu ya kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni kati ya Tanzania na mataifa mengine.







Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...