Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi ameagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Jeshi la Polisi kuchunguza matumizi ya fedha za mradi wa kuboresha miundombinu ya Manispaa ya Lindi, baada ya taarifa kuonesha kuwa mkandarasi amelipwa shilingi bilioni 4.22, lakini utekelezaji umefikia asilimia 24 pekee huku asilimia 80 ya muda wa mkataba ikiwa imetumika.
Akitoa maelekezo hayo leo wakati wa ziara yake mkoani Lindi, Makamu wa Rais ametaka kufahamishwa namna malipo yalivyofanyika, fedha zilivyotumika na sababu za kazi kutotekelezwa kwa kasi iliyotarajiwa. Pia ametaka taarifa ya uchunguzi imfikie yeye mwenyewe ili aiwasilishe kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Amehoji sababu za Mkandarasi kuendelea kulipwa fedha nyingine wakati Halmashauri yenyewe ilieleza kuwa hakuwa na nidhamu katika matumizi ya malipo ya awali.
Aidha, Makamu wa Rais hakuridhishwa na maelezo ya halmashauri kwamba imemwandikia mkandarasi barua 16 kuhusu kusuasua kwa kazi. Amesisitiza umuhimu wa kuchukua hatua badala ya kuendelea kuandikiana barua wakati fedha za umma zimeshalipwa.
Kwa mujibu wa taarifa ya utekelezaji iliyowasilishwa wakati wa ukaguzi, mradi huo wenye thamani ya shilingi bilioni 19.06 unatekelezwa na Hamerkop International Limited JV KIKIM Contractor’s Limited.
Mkandarasi amelipwa jumla ya shilingi bilioni 4.22, zinazojumuisha malipo ya awali ya shilingi bilioni 2.86 na malipo kupitia hati namba mbili ya shilingi bilioni 1.36.
Mkataba wa mradi huo ulisainiwa Juni 25, 2025, mjini Dodoma, na kazi kuanza rasmi Novemba 7, 2025. Mradi unatakiwa kukamilika Februari 5, 2027. Kwa mujibu wa taarifa, utekelezaji ulitarajiwa kufikia asilimia 80 katika hatua hii, hivyo kiwango cha asilimia 24 kilichofikiwa kiko nyuma kwa pointi 56 za asilimia.
Mradi huo, unaotekelezwa kupitia mpango wa TACTIC, unajumuisha Soko Kuu la Matopeni, barabara za kilomita 5.3, Stendi ya Mabasi Mitwero na Ofisi ya Uratibu wa Mradi. Unafadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia Serikali chini ya TAMISEMI, huku usimamizi wa kitaalamu ukifanywa na Inter-Consult Limited kwa kushirikiana na Tanzo Vision Engineering Limited.
Kusuasua kwa ujenzi kulimfanya Waziri anayehusika na TAMISEMI, Profesa Riziki Shemdoe, kufanya ukaguzi Septemba 14, 2026. Aliagiza mkandarasi atafute wakandarasi wadogo wenye uwezo, pamoja na kuundwa kwa timu maalumu ya ufuatiliaji. Timu hiyo ilibaini kuwa mkandarasi hana uwezo wa kukamilisha mradi kwa wakati uliopangwa. Ilipendekeza abaki na ujenzi wa soko, huku kazi nyingine tatu zikitekelezwa na wakandarasi wadogo.
Kwa mujibu wa taarifa, mkandarasi mdogo wa barabara amepatikana, lakini stendi na ofisi bado zinatafutiwa wakandarasi wengine.

.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...