Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Dkt.Abdul-Razaq Badru, amewataka waongoza watalii nchini kuendelea kujiongezea maarifa kuhusu vivutio na bidhaa za utalii ili kuboresha huduma kwa wageni.

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Chama cha Waongoza Watalii wa Kanda ya Kaskazini (NTSGS) Dkt.Badru alisema mtu anayetafuta maarifa hachoki hasa ikizingatiwa kuwa waongoza watalii ni kiungo muhimu kati ya vivutio vya utalii na wageni hivyo wanapaswa kuwa na uelewa wa kina wa maeneo wanayoyaeleza.

Alisema mtalii anayefika nchini anatarajia kupata taarifa sahihi na za kutosha kuhusu vivutio anavyotembelea, jambo ambalo huongeza thamani ya huduma anayolipia na kumhamasisha kurejea tena nchini.

Dkt.Badru aliongeza kuwa utalii ni miongoni mwa sekta zinazochangia kwa kiwango kikubwa uchumi wa taifa, huku akisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa wadau wote, wakiwemo waongoza watalii, katika kuendeleza sekta hiyo.

Amewahakikishia waongoza watalii kuwa Ngorongoro kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii itaendelea kuandaa mafunzo ya kujengea uwezo, ikiwemo mafunzo maalum ya kuwaboresha kitaaluma kabla ya msimu mkubwa wa utalii na tukio kubwa na la muhimu kabisa la Michezo ya AFCON.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa NTSGS, Angelbert Aloyce Qorro, alisema chama hicho tangu kuanzishwa mwaka 2019 kimekuwa mstari wa mbele katika kuimarisha taaluma ya uongozaji watalii na kujenga ushirikiano na taasisi za uhifadhi.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...