Na Mwamvua Mwinyi, Pwani

Halmashauri ya Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, imepokea Sh bilioni 1.3 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/2027.

Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Leon Mgweno, amesema fedha hizo zimeelekezwa katika kata mbalimbali kwa ajili ya kutekeleza miradi ikiwemo ya elimu, inayolenga kuboresha huduma na kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika eneo hilo.

Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani, Mgweno alisema baadhi ya miradi iliyoelekezwa kutekelezwa ni pamoja na ujenzi wa eneo la maegesho ya malori na soko la wajasiriamali.

Mlawa aliwataka wataalamu wa Halmashauri kukutana na wawekezaji na kuwaelekeza namna ya kushiriki katika kuchangia maendeleo ya jamii, huku akiwataka madiwani kuwafuata wananchi katika maeneo yao, kusikiliza kero na kutafuta ufumbuzi badala ya kusubiri viongozi wa ngazi za juu kufika.

Katika kikao hicho, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Ramadhani Possi, ameombwa kusaidia ukarabati wa barabara inayoelekea katika chuo cha ufundi ili iweze kupitika wakati wote.

Wakati huo huo, Diwani wa Miono, Fransis Kilo, aliiomba RUWASA kuimarisha upatikanaji wa huduma ya maji katika eneo la Kweikonje ili kuwaondolea wakazi wake changamoto ya upatikanaji wa maji.






Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...