Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi ameweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kongani la Viwanda katika Kijiji cha Maranje, Halmashauri ya Nanyamba, akiwa ziarani mkoani Mtwara leo tarehe 13 Novemba 2026.

Katika hafla hiyo, Makamu wa Rais amekabidhi mashine 100 zinazotumia umeme kwaajili kubangulia korosho kwa Vikundi mbalimbali Wilayani humo, na kuagiza kuimarishwa kwa huduma za gesi, umeme na barabara ili kuchochea uzalishaji na ajira.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania, Francis Alfred, kongani hiyo ina ekari 1,500, zikiwemo 350 zinazotumika kwa sasa, na wawekezaji tisa wako tayari kuwekeza.

Lengo ni kufikia mwaka 2030, korosho zote zinazozalishwa nchini zibanguliwe na viwanda vya ndani kuongeza thamani, ajira na manufaa kwa uchumi wa Tanzania.
















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...