Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, leo Novemba 18, 2026 ameongoza kikao cha Kamati ya Maandalizi ya Hafla ya Ugawaji Tuzo za World Travel Awards (WTA) zinazotarajiwa kufanyika Desemba 12, 2026 katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Akizungumza katika kikao hicho, Dkt. Abbasi amesisitiza kuwa tukio hilo ni la kimataifa na lenye hadhi kubwa, hivyo maandalizi yote yanapaswa kuzingatia ukubwa na umuhimu wake ili kuhakikisha linafanyika kwa viwango vya kimataifa.
Amesema Tanzania inapata fursa adhimu ya kuitangaza zaidi nchi kimataifa kupitia tukio hilo, huku Serengeti ikiwa mwenyeji wa wageni na wadau mbalimbali wa sekta ya utalii kutoka sehemu tofauti duniani.
Serengeti, inayotambulika kimataifa kwa tukio la kipekee la uhamaji wa mamilioni ya Nyumbu (Wildebeest Migration), inatarajiwa kuwa jukwaa la kuonesha uzuri wa vivutio vya Tanzania na ubora wa huduma za utalii.







.jpeg)




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...