Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) zinaendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025–2030 kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo inayolenga kuimarisha uchumi na kuboresha maisha ya wananchi.

Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 21 Novemba 2026, katika Kongamano la Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) lililofanyika Gombani, Mkoa wa Kusini Pemba, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya mwaka mmoja wa muhula wa pili wa uongozi.

Amesema Serikali zinaendelea kuimarisha miundombinu, huduma za afya, elimu, maji na nishati, sambamba na kukuza sekta za kilimo, viwanda, utalii na Uchumi wa Buluu ili kuongeza ajira na fursa za kiuchumi kwa wananchi.

Aidha, amesisitiza dhamira ya Serikali katika kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri, mifuko ya maendeleo na mafunzo ya ujasiriamali, pamoja na kuongeza ushiriki wao katika nafasi za uongozi na maamuzi.

Vilevile, amewataka wanawake wa UWT kuendelea kuwa mabalozi wa maendeleo, kudumisha amani na mshikamano wa kitaifa pamoja na kufikisha changamoto za wananchi katika vyombo husika ili zipatiwe ufumbuzi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa UWT Taifa, Ndugu Mary Chatanda, amesema Jumuiya hiyo inajivunia mafanikio yaliyopatikana katika kuwawezesha wanawake kushiriki katika uongozi na maendeleo ya Taifa kupitia uteuzi wao katika nafasi mbalimbali za maamuzi.

Amesema kuongezeka kwa nafasi za uongozi kwa wanawake kumewapa fursa ya kuonesha uwezo wao katika kusimamia majukumu na kuchangia maendeleo ya jamii.






















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...