Kambi ya uchunguzi na matibabu ya kibingwa imeingia siku ya nne sasa tangu kufunguliwa kwake katika Tarafa ya Ngerengere, Halmashauri ya Morogoro.

huduma hizo kwa Sasa zimehamia katika Tarafa ya Mikese ambapo hadi sasa, idadi ya watu waliioonwa na kutibiwa imefikia 20,291 huku wagonjwa 14 kati yao wakipewa rufaa na kupelekwa katika Hospitali ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa matibabu zaidi ya kibingwa.

Kambi hiyo inayodhaminiwa na Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, Mheshimiwa Hamiss Taletale, kwa kushirikiana na Serikali na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.

Akitoa taarifa fupi ya mwendelezo wa huduma hizo katika eneo la Mikese, Kaimu Mganga Mfawidhi wa Halmashauri ya Morogoro, Dkt. Kazmil Subi amesema huduma zinaendelea kutolewa kama zilivyopangwa.

"Huduma zinaendelea vizuri kama tulivyopanga hivyo tunawasihi wakazi wa Mikese na maeneo ya jirani wajitokeze kwa wingi, kwani madaktari bingwa wapo hapa kwa ajili yao, na huduma ni zinatolewa bila malipo." Alisema

Aidha Dkt. Subi amebainisha magonjwa yanayowasumbua wananchi katika ukanda huo ni pamoja na magonjwa ya wanawake, hasa ya uzazi na saratani ya shingo ya kizazi, magonjwa ya watoto ikiwemo malaria, pamoja na magonjwa ya wanaume aina ya busha na ngiri.

Akizungumza na wananchi waliojitokeza kupata huduma hiyo, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Morogoro, Bw. Robert Mwega amesema CCM ina wajibu wa kuisimamia Serikali kuhakikisha inatoa huduma bora kwa wananchi.

Mwega amewataka wananchi kuendelea kuiamini CCM na Serikali yake kwa kuwa afya ya wananchi ndiyo kipaumbele cha kwanza.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, Mheshimiwa Hamiss Taletale, amewataka wananchi wa Mikese na maeneo ya jirani kuendelea kujitokeza kwa wingi.

 "Nawaombawananchi wangu wa Mikese na maeneo yote ya jirani, muendelee kujitokeza kwa wingi kwani huduma hizi zinatolewa kwa kila mwenye uhitaji, bila kujali kipato chake, itikadi ya chama,dini Wala kabila. hata hivyo Afya yenu ndiyo nguvu ya maendeleo ya jimbo letu. Msiogope, njooni mpimwe, mtibiwe, na mkitakiwa kwenda JKCI tutawasafirisha wenyewe." Alisema

Mhe. Taletale amesema lengo lake ni kuhakikisha hakuna mwananchi anayekosa matibabu kwa sababu ya ukosefu wa fedha.

Kambi hiyo itaendelea kwa siku zijazo katika Tarafa ya Mikese kabla ya kuhamia katika tarafa ya mkuyuni.





Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...