Na Seif Mangwangi, Michuzi TV, Arusha
MAHAKAMA ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR), imeyatupilia mbali maombi manne yaliyowasilishwa na walalamikaji dhidi ya nchi za Malawi, Burkina Faso, Mali na Benin, baada ya kubaini kuwa hayakukidhi baadhi ya masharti ya kisheria yanayotakiwa ili kesi zisikilizwe na Mahakama hiyo.
Hukumu hizo zilisomwa Novemba 13, 2026, na majaji watatu tofauti wa Mahakama hiyo, wakiongozwa na Rais wa Mahakama, Jaji Blaise Chikaya, kesi hizo zilihusu madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu, ikiwamo haki ya kumiliki mali, usawa mbele ya sheria, haki ya kusikilizwa na haki za kisiasa.
Katika shauri la kwanza namba 007/2022, lililowasilishwa na Mlalamikaji Patroklos Tsaperas dhidi ya Jamhuri ya Malawi, mwombaji ambaye ni raia wa Afrika Kusini na mkurugenzi wa kampuni ya Malawi Mobile Limited (MML), aliituhumu Serikali ya Malawi kukiuka haki zake za msingi, ikiwamo haki ya kumiliki mali, kutobaguliwa, usawa mbele ya sheria na haki ya kusikilizwa kwa mujibu wa sheria.
Serikali ya Malawi iliwasilisha pingamizi la awali ikidai kuwa mwombaji hakumaliza kutumia njia za ndani za kisheria kabla ya kuifikisha kesi hiyo Mahakamani hapo pamoja na kuchelewa kuwasilisha maombi yake.
Baada ya kupitia hoja za pande zote, Mahakama ilibaini kuwa suala la haki ya kumiliki mali lilikuwa limefikia hatua ya kukamilisha taratibu za ndani za kisheria.
Hata hivyo, Mahakama ilibaini kuwa Tsaperas aliwasilisha maombi yake Oktoba 17, 2022, takribani miaka saba, miezi saba na siku saba baada ya Mahakama Kuu ya Rufaa ya Malawi kutoa uamuzi wake Machi 10, 2015 na kwa kuwa hakutoa maelezo ya kuridhisha kuhusu sababu za kuchelewa kuwasilisha maombi hayo, Mahakama iliamua kuwa maombi yake hayakuwasilishwa ndani ya muda unaokubalika kisheria na hivyo kuyatupilia mbali.
Aidha katika uamuzi huo, Mahakama ilielekeza kila upande kubeba gharama zake za shauri.
Katika shauri la pili, Jean Roger M’BA dhidi ya Burkina Faso, namba 015/2019, mwombaji aliomba Mahakama itoe nafuu mbalimbali, zikiwamo msamaha au kupunguziwa adhabu ya kifo, kuhamishiwa katika nchi alikozaliwa pamoja na kulipwa fidia.
Mahakama ilibaini kuwa mwombaji aliwasilisha maombi yake Aprili 23, 2019, ikiwa ni miaka sita, miezi miwili na siku 29 tangu kukamilika kwa taratibu za ndani za kisheria.
Hata hivyo, hakutoa sababu zilizothibitishwa kueleza kwa nini alichukua muda mrefu kuifikisha kesi hiyo mbele ya Mahakama ya Afrika.Katika kufafanua uamuzi wake, Mahakama ilisisitiza kuwa ukweli kwamba mtu amefungwa jela pekee hautoshi kuwa sababu ya kuhalalisha kuchelewa kuwasilisha maombi.
Aidha mahakama hiyo Ilieleza kuwa mwombaji anapaswa kutoa maelezo na ushahidi unaoonyesha kuwa muda alioutumia kuwasilisha shauri ulikuwa wa kuridhisha hivyo kutokana na kutokuwepo kwa maelezo hayo, Mahakama ilitangaza maombi hayo kutokubalika na kuelekeza kila upande kubeba gharama zake.
Shauri la tatu lililotolewa hukumu ni namba 023/2020 la mlalamikaji Babarou Bocoum dhidi ya Jamhuri ya Mali, ambapo mwombaji alidai kukiukwa kwa haki zake za usawa mbele ya sheria na kushiriki katika shughuli za uongozi wa nchi, kufuatia kuondolewa kwa jina lake katika daftari la wapiga kura na mchakato wa uchaguzi wa wabunge uliofanyika Machi 29, 2020.
Katika maombi yake, Bocoum aliiomba Mahakama kufuta matokeo ya uchaguzi husika, kurejesha jina lake katika daftari la wapiga kura, kufanya mageuzi ya mfumo wa uchaguzi ikiwamo kuanzishwa kwa tume huru ya uchaguzi, pamoja na kumlipa fidia ya faranga kiasincha CFA milioni 100.
Hata hivyo, Mahakama ilibaini kuwa sheria za Mali zilikuwa zimeweka njia za kiutawala na kimahakama ambazo mwombaji angeweza kuzitumia kupinga kuondolewa kwa jina lake katika daftari la wapiga kura lakini hakuwasilisha ushahidi unaoonyesha kuwa alitumia au hata kujaribu kutumia njia hizo kabla ya kuifikisha kesi yake katika Mahakama ya Afrika ya Watu na haki za binaadam.
Kutokana na hali hiyo, Mahakama hiyo ilisema kuwa Bocoum hakutimiza sharti la kumaliza kutumia njia za ndani za kisheria kabla ya kuwasilisha maombi yake katika Mahakama hiyo, hivyo, ilitangaza maombi yake kutokubalika na kuamuru kila upande kubeba gharama zake.
Katika shauri la nne namba 063/2019 lililofunguliwa na ,mlalamikaji, Ida Afiavi Ajavon (née Goudjo) na wenzake dhidi ya Jamhuri ya Benin, waombaji walikuwa ni raia wa Benin wanaoishi Paris, Ufaransa, kama wakimbizi wa kisiasa.
Walalamikaji hao ni Ida Afiavi Ajavon, Ludmila Isis Ayelé Ajavon, Evaëlle Jonella Noémie Ajavon na Ronald K. Steeven Karen Ayité Ajavon.
Waombaji waliwasilisha shauri hilo Novemba 29, 2019, wakidai kukiukwa kwa haki zao za kumiliki mali na kusikilizwa kwa haki, kufuatia hatua zilizochukuliwa dhidi ya kampuni ya COMON SA pamoja na kutaifishwa au kuzuiwa kwa akaunti zao binafsi za benki.
Ilidaiwa na walalamikaji kuwa hatua hizo zilihusishwa na hukumu iliyotolewa dhidi ya Sébastien Germain Marie Aïkoué Ajavon, aliyekuwa mkurugenzi mkuu na mwanahisa wa kampuni hiyo.
Katika maombi yao, walalamikaji waliomba kulipwa fidia ya faranga za CFA milioni 170 kila mmoja, pamoja na fidia nyingine kwa hasara walizodai kupata na gharama za kesi.
Hata hivyo, Mahakama ilibaini kuwa sheria za kiraia za Benin zilitoa njia za kisheria ambazo wanahisa wangeweza kuzitumia kwa kuwasilisha madai yao, huku Sheria inayojulikana kama OHADA inayotumika nchini humo ikiwa na utaratibu wa kupinga hatua za kukamatwa au kuzuiwa kwa akaunti za benki.
Mahakama ilieleza kuwa waombaji hawakuwasilisha ushahidi unaoonyesha kuwa walitumia au kujaribu kutumia njia hizo za kisheria zilizokuwepo nchini Benin. Kwa msingi huo, ilihitimisha kuwa hawakutimiza sharti la kumaliza kutumia njia za ndani za kisheria kabla ya kuwasilisha shauri lao.
Aidha, Mahakama ilikataa pingamizi nyingine zilizowasilishwa na Serikali ya Benin, zikiwamo hoja zilizohusu suala la shauri hilo kuwa tayari limeamuliwa na kutokuwepo kwa madai mahususi.
Mahakama ilifafanua kuwa fidia iliyowahi kutolewa kwa Sébastien Ajavon ilikuwa inamhusu yeye binafsi na haikumaanisha moja kwa moja kuwa wanahisa wengine wa kampuni hiyo nao walikuwa wamefidiwa.
Katika kuhitimisha hukumu yake Mahakama ilitangaza maombi ya Ida Afiavi Ajavon na wenzake kutokubalika kutokana na kushindwa kutumia njia za ndani za kisheria, na kuelekeza kila upande kubeba gharama zake za shauri
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...