Na Farida Mangube Dodona
PAZIA la Ligi ya Taifa ya Mpira wa Kikapu (NBL) limefunguliwa rasmi jijini Dodoma, likiwakutanisha jumla ya timu 28, zikiwemo timu 16 za wanaume na 12 za wanawake, zinazowania ubingwa wa msimu huu.
Miongoni mwa timu zinazoshiriki ni mabingwa watetezi pamoja na timu nyingine zilizojiandaa kupambana kuwania mataji ya michuano hiyo inayotarajiwa kutamatika Desemba 8 mwaka huu.
Michuano hiyo iliyoanza Novemba 28, imefunguliwa rasmi katika viwanja vya Chinangali jijini Dodoma, huku wadau mbalimbali wakieleza matumaini yao ya kuona ushindani mkubwa na maendeleo zaidi ya mchezo wa kikapu nchini.
Akizungumza katika hafla ya ufunguzi, Kamishna wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Robert Nyerere, amesisitiza umuhimu wa michuano hiyo katika kukuza na kuendeleza mchezo wa kikapu nchini.
Kwa upande wake, mwakilishi wa kampuni ya Bet Power, Rose Kishimba, ameeleza dhamira ya kampuni hiyo ya kuendelea kuunga mkono maendeleo ya michezo nchini kupitia ushirikiano wake na TBF.
Nae Rais wa Fox Divas ya mkoani Mara, Esther Matiko, amesema wamejipanga kuhakikisha wanaendelea kutetea ubingwa wao wa wanawake baada ya kutwaa taji hilo mara mbili mfululizo.
Aidha, Matiko ametoa wito kwa Serikali na wadau mbalimbali kuongeza uwekezaji katika mchezo wa kikapu ili kuimarisha ushindani na kuinua viwango vya timu nchini.



.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...