Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
Manispaa ya Kibaha, mkoani Pwani, imepokea vifaa maalumu 14 kutoka Kiwanda cha Tanzania Biotech Products Limited (TBPL), kwa ajili ya kuimarisha mapambano dhidi ya malaria kwa kuangamiza mazalia ya mbu wanaoeneza ugonjwa huo.
Akizungumza wakati wa kupokea vifaa hivyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kibaha, Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo, Dkt. Catherine Saguti, ameeleza kuwa, vifaa hivyo vitatumika kupulizia dawa kwenye mabwawa yenye mazalia ya mbu ili kudhibiti ongezeko la wadudu hao.
Dkt. Saguti amesema Manispaa inatambua mchango wa TBPL katika mapambano dhidi ya malaria na kutoa shukrani kwa uongozi wa kiwanda hicho kwa kuendelea kushirikiana na Halmashauri katika kulinda afya za wananchi.
Kwa upande wake, Mratibu wa Malaria wa Manispaa ya Kibaha, Ally Bakari Shaha, amesema vifaa hivyo vitaongeza ufanisi wa shughuli za udhibiti wa mazalia ya mbu, huku akiwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii wanapofika kwenye maeneo yao kutekeleza zoezi la upuliziaji dawa.
Amefafanua utaratibu wa kupulizia dawa kwenye mabwawa yenye mazalia ya mbu na matundu ya vyoo umesaidia kupunguza kiwango cha malaria kutoka asilimia 35 hadi asilimia moja, huku akibainisha kuwa dawa zinazotumika katika zoezi hilo hutolewa bure.
Akikabidhi vifaa hivyo, Kaimu Masoko wa TBPL, Pilly Abbas, ameeleza vifaa 14 vimetolewa kwa ajili ya kata zote za Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano pale utakapohitajika.
Msaada huo unatarajiwa kuimarisha juhudi za Manispaa ya Kibaha katika kudhibiti mazalia ya mbu na kuendeleza mapambano dhidi ya malaria na magonjwa mengine yanayoenezwa na mbu.

.jpeg)

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...