Na Mwamvua Mwinyi, Mafia
MKUU wa Mkoa wa Pwani, Stanslaus Nyongo, amesema kuanzia mwezi ujao wananchi wa Wilaya ya Mafia wataanza kupata tiketi za kivuko kupitia mfumo wa mtandao ili kurahisisha huduma za usafiri na kuondoa usumbufu wa kufuata tiketi bandarini.
Nyongo ameyasema hayo Novemba 7, mwaka huu, wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kisiwani Mafia kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero zinazowakabili.
Awali, wananchi walieleza changamoto ya upatikanaji wa tiketi za kivuko, wakisema utaratibu uliopo unawalazimu kufika bandarini kuandika majina na kutafuta nafasi ya kusafiri.
Walisema hali hiyo imekuwa ikiwapa usumbufu, huku baadhi yao wakikosa nafasi ya kusafiri kutokana na kutokuwa na mfumo rahisi wa kukata tiketi wakiwa maeneo yao.
Akijibu hoja hiyo, Nyongo amesema mfumo huo wa mtandaoni utawezesha wananchi kupata tiketi kwa urahisi bila kulazimika kufika bandarini, hatua inayotarajiwa kupunguza usumbufu na kuboresha huduma za usafiri kwa wakazi wa Mafia.





.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...