Mkuu wa Mkoa wa Mara, Brigedia Jenerali Evans Mtambi, akifungua semina ya mafunzo kwa Maafisa Rasilimaliwatu na Utumishi wa Mkoa huo iliyoandaliwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Mjini Musoma Novemba 6, 2026.

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Brigedia Jenerali Evans Mtambi, akifungua semina ya mafunzo kwa Maafisa Rasilimaliwatu na Utumishi wa Mkoa huo iliyoandaliwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Mjini Musoma Novemba 6, 2026.

Meneja wa Mfuko wa PSSSF Kanda ya Ziwa Mashariki, Bw. Rajabu Kinande (kulia), akizungumza kwenye semina ya mafunzo kwa Maafisa Rasilimaliwatu na Utawala wa Mkoa wa Mara. Semina hiyo imefunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Brigedia Jenerali Evans Mtambi mjini Musoma, Novemba 6, 2026.
Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Mhe. Juma Chikoka, akitoa salamu kwenye semina kwa Maafisa Utumishi mkoani Mara. Semina hiyo iliandaliwa na PSSSF na kufanyika Mjini Musoma Novemba 6, 2026
Baadhi ya washiriki wa semina ya mafunzo kwa Maafisa Rasilimaliwatu na Utawala wakifiatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa na wataalamu wa Mfuko wa PSSSF mjini Musoma Novemba 6, 2026.




Novemba 6, 2026 Musoma.


Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umeendesha semina kwa Maafisa Utumishi Mkoa wa Mara, ili kuwajengea uelewa wa kushughulikia kwa weledi masuala ya wanachama wa mfuko huo.

Semina hiyo imefanyika Ijumaa Novemba 06, 2026 katika Wilaya ya Musoma, Mkoani Mara ambapo washiriki wa semina hiyo wamehimizwa kuwasaidia wanachama wa PSSSF kupata huduma bora na kwa wakati.

Akifungua semina hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mara Brigedia Jenerali Evans A. Mtambi amesema semina hiyo pia itasaidia kuongeza ufanisi katika upatikanaji wa huduma za PSSSF hususani matumizi ya huduma za kidigitali kwa wanachama.

“Zamani mtu alikuwa anafunga safari kwenda Dar es salaam, Dodoma au makao makuu ya Mkoa, lakini sasa hivi anawasha tu bando kwenye simu yake, anawasilisha hitaji lake na anahudumiwa akiwa nyumbani” amesema RC Mtambi.

Naye Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa Mashariki, CPA. Rajabu Kinande amesema ili kuhakikisha Mfuko huo unatoa huduma bora na ya haraka, umejikita kuwafikia wanachama wake kwa njia ya kidigitali.

“Sasa hivi mteja anaweza kupata huduma kupitia simu yake ya mkononi hivyo ili kuhakikisha huduma hiyo inaenda vizuri tukaona ni vyema

kukutana na maafisa Utumishi ambao wana wajibu wa kutusaidia kutoa huduma bora kwa wanachama” amesema CPA. Kinande.

Akitoa shukurani kwa niaba ya Maafisa Utumishi mkoani Mara, Jumanne Obogo ambaye ni Afisa Utumishi Halmashauri ya Musoma Vijijini amesema semina hiyo itawasaidia kuwahudumia kwa ufanisi watumishi kupitia mfumo wa kidigitali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...