Na Janeth Raphael - MichuziTv
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Judith Suminwa Tuluka, amepongeza ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya Tanzania na nchi yake, huku akiishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kushirikiana na DRC katika masuala ya usalama na maendeleo ya kiuchumi.
Akizungumza Novemba 4, 2026, baada ya kutembelea Mji wa Serikali wa Mtumba jijini Dodoma, Tuluka amesema Tanzania na DRC zina uhusiano wa kihistoria unaotokana na undugu na ujirani mwema, hivyo ni muhimu kwa mataifa hayo kuendelea kuimarisha mshikamano na ushirikiano katika maeneo yenye maslahi ya pamoja. Ameeleza kuwa ushirikiano huo una mchango mkubwa katika kulinda usalama wa nchi hizo na kuchochea maendeleo ya kiuchumi, ikiwemo kuboresha miji na mazingira ya maisha ya wananchi.
Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi wa DRC, John Banza Lunda, amesema amevutiwa na hatua kubwa ambazo Tanzania imepiga katika sekta ya miundombinu, akibainisha kuwa ziara yake imemwezesha kujionea uwekezaji uliofanywa na Serikali katika miundombinu ya usafiri na majengo ya umma. Amesema safari yake kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma imempa nafasi ya kushuhudia maendeleo ya miundombinu, ikiwemo majengo ya Bunge na Mji wa Serikali wa Mtumba, ambayo ni sehemu ya uwekezaji unaochochea ukuaji wa uchumi na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Aidha, Banza Lunda amesema DRC inaendelea na mikakati ya kuimarisha miundombinu yake ili kukuza shughuli za kiuchumi na kijamii, huku akieleza kuwa nchi hiyo inatekeleza mradi wa ujenzi na uendelezaji wa bandari katika mwambao wa Ziwa Tanganyika, inayotarajiwa kuanza kufanya kazi Machi 2027.

Amesema bandari hiyo itarahisisha usafirishaji wa bidhaa na kukuza biashara katika maeneo yanayozunguka ziwa hilo. Ameongeza kuwa anatarajia kutumia Treni ya Reli ya Kisasa (SGR) kurejea Dar es Salaam ili kujionea zaidi uwekezaji wa Tanzania katika sekta ya usafiri wa reli, huku akiishukuru Serikali ya Tanzania na Rais Samia kwa ukarimu na mapokezi mazuri waliyoyapata.
Naye Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki, amesema Tanzania imefurahi kupokea ujumbe wa DRC katika ziara hiyo ya kindugu na kirafiki, ambayo inalenga kuendeleza uhusiano wa muda mrefu uliopo kati ya mataifa hayo mawili.

Amesema uhusiano wa Tanzania na DRC umejengwa katika misingi ya historia ya pamoja, undugu na ujirani mwema, hivyo ziara hiyo ni fursa muhimu ya kuendeleza urafiki na kuimarisha ushirikiano uliopo.
Kairuki ameongeza kuwa Tanzania inathamini uhusiano wake na DRC na itaendelea kuweka mazingira mazuri yatakayowezesha mataifa hayo kushirikiana katika sekta mbalimbali.

Amesisitiza kuwa ziara za viongozi na ujumbe wa mataifa hayo zina umuhimu mkubwa katika kuimarisha mshikamano, kufungua fursa mpya za ushirikiano na kuhakikisha wananchi wa pande zote mbili wananufaika na mahusiano hayo, hususan katika maeneo ya maendeleo ya kiuchumi, miundombinu na ustawi wa jamii.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...