Timu ya madaktari bingwa 30 waliowasili mkoani Njombe wameanza kutoa huduma katika hospitali za wilaya zote mkoani humo huku wito ukitolewa kwa wananchi kujitokeza kupata matibabu ili kupunguza ghalama kwa kufuata huduma hizo katika hospital kubwa nchini.

Michuzi blog imefika katika Hospitali ya mji wa Njombe Kibena na kushuhudia huduma zikiendelea ikiwemo mama mjamzito aliyefanyiwa upasuaji kwa usalama chini ya uangalizi wa madaktari hao ambapo Erenestina Mwipopo Daktari Bingwa Mbobezi wa magonjwa ya Watoto anasema tayari ameanza kuwahudumia watoto na baadhi ya aliowahudumia ni wenye magonjwa ya Moyo,Kuzaliwa kabla ya wakati pamoja na Changamoto nyingine.

"Hapa Njombe mjini tupo madaktari bingwa watano na tumegawanyika kwenye idara tofauti lakini hapa kwenye watoto wachanga tumeshaanza kuwahudumia pia na kuna mtoto mwenye changamoto ya Moyo anapatiwa huduma na upande wa akina mama tayari upasuaji umeanza"amesema Dkt.Erenestina Mwipopo

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mji wa Njombe Kibena Dokta Ayub Mtulo amesema wateja wameendelea kujitokeza katika hospitali hiyo ambapo wengi wao wamekuwa wakifika kwa dakatari bingwa wa wanawake na uzazi "Wanaofika kwa wingi ni wateja wa daktari bingwa wa wanawake pamoja na uzazi pamoja na magonjwa ya ndani lakini pia daktari bingwa wa upasuaji amepata wateja"

Timu hiyo ya madaktari bingwa ni miongoni mwa madaktari bingwa katika mpango kabambe wa utoaji huduma za kibingwa kwenye hospitali 184 katika ngazi ya halmashauri zinazofanywa na madaktari bingwa wabobezi wa Dkt. Samia



NA VICTOR MASANGU,KIBAHA


Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mjini Mwalimu Mwajuma Nyamka amewataka viongozi wa chama kuhakikisha wanaweka misingi ya kuwaheshimu viongozi wote waliopo madarakani na kuachana kabisa na tabia ya kutengeneza safu mpya ya viongozi wapya kabla ya muda kufika.

Mwalimu Nyamka ameyasema hayo wakati wa kikao kazi ambacho kiliweza kuwakutanisha Wenyeviti pamoja na makatibu wote wa CCM ngazi ya Kata kutoka kata zote 14 za Halmashauri ya Kibaha mji lengo ikiwa kujadili mambo mbali mbali ikiwemo kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu.

Alisema kwamba viongozi wq chama wanapaswa kuwapa ushirikiano wa kutosha viongozi wote waliopo madarakani kuanzia ngazi za chini hadi za juu ili waweze kutimiza majukumu yao ipasavyo bila ya kusumbuliwa kwani bado wapo madarakani.

"Tumekutana katika kikao kazi hiki na nimewakutanisha wenyeviti wa ccm ngazi ya kata pamoja na makatibu wa Ccm ngazi ya kata lengo lake kubwa ni kuweka mikakati madhubuti ya kukijenga chama chetu kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa,"

"Pamoja na kuwa katika maandalizi ya kujiandaa na kuelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa ni lazima tukawaheshimu viongozi ambao wapo madarakani na tusianze kupanga safu za viongozi wengine kabla ya muda wake hii haitakiwi kabisa,"alibainisha Mwenyekiti Nyamka.

Kadhalika aliongeza kuwa viongozi wa chama ambao wapo madarakani wanastahili kupewa ushirikiano wa kutosha katika kutekeleza Ilani ya chama kwa vitendo na sio kuwavunja moyo pindi wakiwa bado madarakani.

Kadhlika alisema kwamba lengo lubwa la chama ni kuweka mipango madhubuti ambayo itasaidia kushiriki kikamilifu na hatimaye kushinda kwa kishindo katika chaguzi mbali mbali ikiwemo wa serikali za mitaa ambao utafanyika mwaka huu.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo aliwakumbusha viongozi hao kuweka misingi ya kuwa na umoja na mshikamano ili kuweza kukiimarisha chama kuanzia ngazi za mashina,matawi,kata hadi ngazi za juu hali ambayo itasaidia kukijenga chama.

Katika hatua nyingine Nyamka alimpongeza Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka kwa kuweza kushirikiana bega kwa bega na wananchi katika kutekeleza miradi mbali mbali ya kimaendeleo.

Pia Mwalimu Nyamka hakusita kumshukuru kwa dhati Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kutenga fedha ambazo zimeweza kusaidia kwa kiasi kukubwa katika kukamilisha miradi mbali mbali ya maendeleo.

Aliongeza kuwa Rais Samia ameweza kuteleza Ilani ya chama kwa vitendo ambayo imepelekea baadhi ya maeneo kuwaondolea adha changamoto ya wanakinamama kutembea umbari mrefu kwa ajili ya kufuata huduma maji safi na salama.

Kwa upande wake Katibu wa CCM Wilaya ya Kibaha mji Issack Kalleiya amewakumbusha viongozi kuwasajili wanachama kwa mfumo wa kisasa wa kidigitali ambao utasaidia katika kutambua wanachama wake.











Na Mwandishi wetu, Simanjiro

Wakazi wa Kata ya Ngorika wilayani Simanjiro mkoani Manyara, wamekumbwa na wakati mgumu baada ya kukumbwa na mafuriko yaliyotokana na mvua hivyo kuhitaji kivuko au daraja.

Wakazi hao hasa wa kijiji cha Nyumba ya Mungu hivi sasa wanatumia mtumbwi kuvuka eneo moja kwenda jingine kutokana na maji ya mafuriko kuzunguka maeneo yao.

Diwani wa Ngorika, Albert Msole akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro amesema wakazi wa eneo hilo wanapaswa kupatiwa msaada.

Msole amesema bwawa la Nyumba ya Mungu lililotengenezwa mwaka 1964 hadi mwaka 1968 kwa ajili ya uzalishaji wa nishati ya umeme limejaa mno na kutapika.

“Tunahitaji kivuko au daraja kwani hali ni mbaya bwawa limejaa mno, linapokea maporomo ya maji kutoka ziwa jipe, Kilimanjaro, mto Kikuletwa na bwawa la kidawashi,” amesema Msole.

Amesema hivi karibuni kuna mfugaji alizama ndani ya bwawa la Nyumba ya Nyumba, akiwa na ng’ombe wake walipokuwa wamepanda mtumbwi na hadi hivi sasa hajaonekana alipo.

“Mfugaji huyo hakuonekana hii ni siku ya nane ila ng’ombe alikufa maji baada ya mtumbwi waliokuwa wameupanda kupasuka na kuingiza maji,” amesema Msole.

Amesema hata boti ya halmashauri hiyo mashine imeharibika hivyo wananchi wa eneo hilo kuwa na wakati mgumu katika kufanya shughuli zao za kiuchumi za kila siku.

“Hali ya uchumi ni mbaya tunahitaji kivuko au daraja ili kuweza kuvuka kutoka sehemu moja au nyingine kwani hata walimu wanapanda mtumbwi ili wafike shuleni,” amesema.

Amesema awali hali hiyo ilikuwa inajitokeza kila baada ya miaka mitano au 10 ila kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, hivi sasa kila baada ya mwaka mafuriko hayo hutokea.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro, Baraka Kanunga amesema inahitajika viongozi wa wilaya kufika mara moja eneo hilo ili kujionea hali halisi ilivyo.

“Inabidi mimi, mkurugenzi wa halmashauri, kiongozi wa Tarura na diwani wa kata twende tukajionee hali halisi ili tuone namna ya kuwasaidia hao watu,” amesema Kanunga.



Serikali ya Tanzania na China zimesisitiza kuimarisha ushirikiano wa kimkakati ili kuendelea kutekeleza diplomasia ya uchumi kwa maslahi ya pande zote mbili.

Msisitizo huo umetolewa wakati Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) alipokutana kwa mazungumzo na Balozi wa China nchini, Mhe. Chen Mingjian katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam tarehe 7 Mei, 2024.

Mazungumzo ya viongozi hao yalijikita katika kujadili utekelezaji wa maazimio na maelekezo mbalimbali yaliyotolewa na wakuu wa nchi hizo mbili wakati wa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan iliyofanyika nchini China mwezi Novemba 2023.

Aidha, wameainisha maeneo mbalimbali ya kimkakati ambayo nchi hizo mbili zimedhamiria kuziendeleza na kuzisimamia kwa maenedeo ya watu wake. Maeneo hayo ni pamoja na kuanzisha na kuimarisha ushirikiano wa miji dada, kukuza ushirikiano wa biashara na uwekezaji, ujenzi wa miji ya kisasa, maendeleo ya viwanda, kilimo cha kisasa na uongezaji wa thamani ya mazao ya kilimo na mifugo na kuboresha mradi wa reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA).

Kwa upande wake Waziri Makamba ameeleza kuwa Tanzania inathamini ushirikiano wa kihistoria uliopo kati yake na China ambapo kwa uchache alitaja baadhi ya maeneo ambayo Tanzania imekuwa ikinufaika na ushirikiano huo kama vile; ushirikiano kati ya Jeshi la Ulinzi la Tanzania na China uliodumu kwa zaidi ya miaka 60.

Kuongezeka kwa muingiliano wa wananchi wa pande hizo mbili kumepelekea kukua kwa shughuli za kiuchumi hususan katika sekta ya biashara, usafirishaji na utalii.

“Tanzania imijiweka mikakati thabiti ya kuyafikia maendeleo ya viwanda, hivyo imeweka kipaumbele cha kufanikisha hilo kupitia ushirikiano wake na China” Waziri Makamba

Naye Balozi wa China nchini ameeleza kuwa China itaendeleza ushirikiano wake wa kihistoria na Tanzania ikiwa ni pamoja na kukamilisha miradi ya maendeleo inayotekelezwa nchini kwa ufanisi.

Sekta nyingine za ushirikiano kati ya Tanzania na China ni pamoja na elimu, afya, kilimo, biashara, uwekezaji, kilimo, utalii, nishati, madini, usafirishaji, mifugo na utamaduni.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) (kulia) akizungumza na Balozi wa China nchini, Mhe. Chen Mingjian alipokutana naye kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 7 Mei, 2024.

Balozi wa China nchini, Mhe. Chen Mingjian akifafanua jambo wakati alipofanya mazungumzo Mhe. Makamba katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es salaam tarehe 7 Mei, 2024.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo akichangia jambo wakati wa mazungumzo hayo, kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Asia na Australasia, Bw. Salvatory Mbilinyi.

Mazungumzo yakiendelea.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba (Mb.) amekutana na kuzungumza na Balozi wa Switzerland nchini Mhe. Didier Chassot leo tarehe 7 Mei 2024 katika Ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam.

Katika Mazungumzo yao viongozi hao wamejadili namna kukuza na kuimarisha ushirikiano katikaSekta ya ulinzi na usalama kwa maslahi ya pande zote mbili na Jumuiya ya Kimataifa.

Pia wamejadili jinsi ya kujenga uelewa wa pamoja kuhusu athari za migogoro inayojitokeza sehemu mbalimbali duniani na kutoa mapendekezo yenye tija kwa jumuiya ya kimataifa juu ya namna bora ya kutatua migogoro hiyo ili kupunguza adhari zake kwa jamii.

Aidha wamejadili programu mbalimbali zitakazochagiza kuimarika kwa ushirikiano huo ikiwemo ziara za mara kwa mara za viongozi wa sekta ya ulinzi na usalama na kuanda na kushiriki katika mikutano inayolenga kutatua migogoro.

Akizungumza katika mkutano huo Waziri Makamba ameeleza kuwa majadiliano ya utatuzi wa migogoro ni muhimu yakaangazia Bara la Afrika ambapo kwa muda mrefu Nchi nyingi kama vile DRC zimekuwa katika migogo na hazipewi kipaumbele katika mijadala ya kuleta amani inayojitokeza katika majukwaa mbalimbali ya Kimataifa.

Naye Balozi Chassot amesema Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika utatuzi wa migogoro na kuchangia jitihada za kuleta amani sehemu mbalimbali duniani na Switzerland inaitazama Tanzania kama mdau muhimu wa kushirikiana naye kati eneo hilo.

Balozi Chassot ametoa pole kwa Watanzania kwa hasara na uharibufu uliojitokeza kutokana na athari za mvua kubwa zilizosababisha mafuriko katika sehemu mbalimbali nchini na kusababisha vifo,majeruhi, uharibu wa makazi na mali za watu na miundombinu.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akimsikiliza Balozi wa Switzerland nchini Mhe. Didier Chassot kwenye mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam, Mei 7, 2024.




aziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akifafanua jambo wakati wa mazungumzo na Balozi wa Switzerland nchini Mhe. Didier Chassot yaliyofanyika katika Ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam, Mei 7, 2024.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba na Balozi wa Switzerland nchini Mhe. Didier Chassot wakibadilishana mawazo muda mfupi baada ya mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo yakiendelea

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano wa kiutendaji na kampuni ya SILABU APP inayotoa huduma za masomo ya ziada kwa wanafunzi majumbani na kwa njia ya mtandao. Makubaliano hayo yanalenga kushirikisha walimu wa taasisi hiyo kufikisha elimu ya fedha na huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo kwa wanafunzi wao.

Hatua hiyo inatajwa kuwa itasaidia kwa kiasi kikubwa kuwaongezea wanafunzi hao elimu na uelewa kuhusu masuala ya fedha na umuhimu wa kujiwekea akiba tangu wakiwa wadogo.

Hafla ya utiaji saini makubaliano hayo ilifanyika jana jijini Dar es Salaam ikihusisha mafunzo maalum kwa walimu wa taasisi hiyo yaliyotolewa na maafisa wa benki ya NBC kwa lengo la kuwajengea elimu ya kutosha walimu hao kuhusu huduma na program mbalimbali za benki hiyo mahususi kwa walimu na wanafunzi. Mafunzo hayo yanatarajiwa kuwasaidia vema walimu hao kufikisha elimu hiyo kwa walengwa pindi wanapotimiza majukumu yao.

Akifafanua zaidi kuhusu mpango huo Msimamizi wa Huduma za Elimu wa Benki ya NBC, Yoabu Ndanzi alisema ushirikiano huu utatoa fursa kwa benki hiyo kuweza kuwafikia wanafunzi na walimu kwa urahisi zaidi, hatua ambayo itarahisisha suala zima la kuwajengea uelewa wanafunzi hao kuhusu elimu ya fedha sambamba na kutambua huduma za benki hiyo mahususi kwao.

Huduma hizo ni pamoja na akaunti ya Chanua na akaunti ya wanafunzi (Students Account) mahususi kwa watoto na wanafunzi huku pia walimu wakifikiwa kupitia Akaunti ya Mwalimu iliyobuniwa mahususi kwa ajili yao.

“Ushikiano huu unaboresha zaidi kifurushi cha pamoja kwa maana ya kwamba wakati SILABU wanapeleka darasa nyumbani, NBC pia tunatumia fursa hiyo kuingiza uzoefu wa benki nyumbani na hivyo kuwawezesha wanafunzi kunuafaika na elimu zote mbili ambazo zina umuhimu mkubwa sana kwa maisha yao,’’ alifafanua Ndanzi.

Aliongeza kuwa kupitia mpango huo watoto watawekewa kiasi cha sh elfu 5 kila mwezi kwenye Akaunti zao za Chanua. Fedha hizi zinafadhiliwa na SILABU APP ili kuendeleza ushirikiano na wateja wao ambao ndio wanafunzi kila mwezi.

Akizungumzia ushirikiano huo Mwanzilishi Mwenza wa kampuni ya SILABU, Adam Duma alisema ushirikiano na NBC utahusisha walimu zaidi ya 1000, utatoa fursa pia kwa walimu hao kunufaika na huduma mbalimbali za vipaumbele zinazotolewa na benki hiyo ikiwemo akaunti ya Mwalimu huku pia kampuni hiyo ikinufaika kupitia matangazo ya huduma zake kupitia majukwaa mbalimbali ya taarifa za benki hiyo.

“Zaidi tunafarijika kuona kwamba sasa ‘package’ yetu ya mafunzo tunayoyatoa kwa wanafunzi wetu inakwenda kuongezewa kitu muhimu sana ambacho ni elimu ya fedha. Kupitia elimu hii tunakwenda kuandaa kizazi kijacho ambacho kina uelewa wa kutosha kuhusu kujiwekea akiba, kutumia taasisi za fedha kujitengenezea mitaji sambamba na matumizi sahihi ya fedha zao,’’ alisema Duma.

Wakizungumza kwa niaba ya walimu wenzao walioshiriki mafunzo hayo, Mwalimu Sixtmund Byabato na Mwalimu Hellena Mabula pamoja na kuishukuru benki hiyo kwa kuwapatia elimu hiyo ambayo waliihitaji pia, walisema mafunzo hayo yamewaongezea uelewa wa kutosha utakaowawezesha kuwafundisha wanafunzi wao. Mafunzo hayo pia yatawasaidia wao katika kufanikisha malengo yao hususani kupitia fursa mbalimbali zitolewazo na benki hiyo kupitia akaunti ya Mwalimu na akaunti ya Malengo huku pia wakitarajia kunufaika na mikopo rasmi ya taasisi hiyo.

Katika hatua nyingine, benki hiyo pia ilitumia fursa hiyo kuzindua msimu wa pili wa program yake ya kimichezo kwa watoto inayofahamika kama 'Chanua Football Kliniki' itakayofanyika kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam, Juni 1, mwaka huu.

“Kupitia Chanua Football Kliniki watoto wote wenye akaunti ya Chanua watakuwa na sifa ya kushiriki program hii ya michezo. Vigezo kwa wenye akaunti mpya ni kuwa na ingizo la awali (initial deposit) la kiasi cha Shs 100,000 na kwa wale wenye akaunti hizi tayari kigezo ni kuwa na akiba isiyopungua kiasi cha sh 200,000.’’

‘’Washiriki (Watoto na wazazi) watapata fursa ya kufurahia michezo na mafunzo mbalimbali, watapata jezi na Zawadi za jumla na za pekee, watashiriki chakula cha mchana pamoja na pia watashiriki michezo na wachezaji mashuhuri wa ligi kuu ya NBC,’’ Alisema.







Msimamizi wa Huduma za Elimu wa Benki ya NBC, Yoabu Ndanzi (Kulia) na Mwanzilishi Mwenza wa kampuni ya SILABU APP inayotoa huduma za masomo ya ziada kwa wanafunzi majumbani na kwa njia ya mtandao, Adam Duma wajipongeza mara baada ya kusaini makubaliano ya ushirikiano wa kiutendaji baina ya taasisi hizo mbili yanayotoa fursa kwa benki ya NBC kuwatumia walimu wa taasisi ya SILABU kufikisha elimu ya fedha na huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo kwa wanafunzi wao. Hafla ya utiaji saini makubaliano hayo ilifanyika jana jijini Dar es Salaam ikihusisha mafunzo maalum kwa walimu wa taasisi hiyo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo.







Msimamizi wa Huduma za Elimu wa Benki ya NBC, Yoabu Ndanzi akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo.







Mwanzilishi Mwenza wa kampuni ya SILABU APP inayotoa huduma za masomo ya ziada kwa wanafunzi majumbani na kwa njia ya mtandao, Adam Duma akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo.









Wakizungumzia mafunzo hayo walimu hao pamoja na kuishukuru benki hiyo kwa kuwapatia elimu hiyo ambayo waliihitaji pia, walisema mafunzo hayo yamewaongezea uelewa wa kutosha utakaowawezesha kuwafundisha wanafunzi wao.








Msimamizi wa Huduma za Elimu wa Benki ya NBC, Yoabu Ndanzi (wa pili kulia walioketi) na Mwanzilishi Mwenza wa kampuni ya SILABU APP inayotoa huduma za masomo ya ziada kwa wanafunzi majumbani na kwa njia ya mtandao, Adam Duma (katikati walioketi) wakiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo pamoja na baadhi ya maofisa wa benki ya NBC.






Na. Vero Ignatus, Arusha

Waziri wa Maliasili na Utalii Angela Kairuki amesema kuwa katika takwimu na tafiti za Shirika la Utalii duniani Tanzania imewekwa katila nchi ya kuigwa ambayo imekuza uchumi wake kwa kupitia mapato ya utalii na kuingia kwenye kumi Bora, kwani kwa mwaka 2022 imeweza kupokea watalii 1,456,920 mwaka 2023 1,808,205 hii ikiwa ni kwa mwaka mmoja sawa na ongezeko la asilimia 24.28.

Kairuki amesema hayo katika mikutano mkuu wa mwaka wa Taasisi ya waongoza watalii nchini mei 4,2024 Jijini Arusha, kuwa mapato ya utalii kwa mwaka 2022 waliweza kuwa dola za kimarekani bil 2.5 ambapo mwaka 2023 waliweza kufunga mwaka kwa dola za kimarekani bil. 3.3
Malengo ya serikali ifikapo 2025 unapaswa kuwa na mapato ya utalio yasiyopungua bil 6

" Rais Dkt Samia amekuwa ni mwongoza watalii namba moja kwenye kutangaza utalii haswa kupitia program yake ya Royal tour ambapo wameweza kuona matokeo makubwa,ya kuongezeka kwa watalii nchini,sambamba na juhudi nyingine za kuboresha miundombinu ya utalii ambapo aliweza kutoa mafunzo kwa waongoza utalii zaidi ya 1000 kipindi cha covid 19. "

Aidha amewapongeza waongoza watalii Hao kwa kusema kuwa eneo hilo ni nyeti ambalo ni la kukuza Utalii ni la muhimu na kuwa taka kuendelea kuwa mabalozi wazuri katika ulinzi wa mazingira katika hifadhi , sambamba na kulinda utamaduni na Mila za Mtanzania.

Akijibu changamoto za waongoza utalii amesema kuwa suala la bima ya Afya siyo kwamba iliyokuwa awali ya kicurishi vha 100,000 imefutwa la hasha badala yake ni kwamba taarifa za awali alizonazo kupitia kwamba imeongezeka na kufikia 192000 kwa mwaka amewataka wao wenyewe kijuridhisha na kiwango hicho

"Kwa upande wa barabara ya londware kupitia karate kwa sasa inaendelea kufanyia kazi kwani serikali imeweza.kupitia Baheti yetu ya 2023-24 Kutenga shilingi Bil 16 , pia serikali kwa Baheti ya mwaka 2024-25 serikali imetenga shilingi Bil. 40 ambazo zitatumiks. Line. Ga barabara za londware kwa aina ya tabaka gumu".

"Changamoto ya leseni za waongoza utalii na tozo zake maslahi mbalimbali, gharama za malazi kwa waongoza watalii tauari tumeshaanza kufanyia kazi Malalamiko yote ili kuyapatia suluhu kwsajili ya kuboresha na kukuza biashara ya utalii, ni Bornora mokajiwekea viwango vya ubora, hivyo 2024 -2025 serikali itatoa tena mafunzo ya utalii kwenu kwani ninyi ndio taswira ya nchi yetu.'alisema

"Suala la mikataba ya Ajira 6 april nilishamueleza Afisa kazi mkoa wa Arushana tayari alishaitisha kikao 25 April 2024 ambacho kilihudhiriwa na wadau kutoka TTGA, Wizaara ya kazi na niliwaambia lazima wataalam kutoka Wizara ya maliasili na utalii wawepo maana ndio walezi wenu na washauri wenu na waliweza kupeana eliminate juu ya mikataba ya Ajira.

Awali akisoma risala Katibu Mkuu wa Taasisi ya waongoza watalii Tanzania Robert Max Asilimia 70% ya waongoza utalii nchini hawana mikataba ya ajira 30% tu ndiyo wameajiriwa wengi mbali na sekta hiyo kuliingizia Taifa 25℅ya pesa za kigeni na inachangia Pato la Taifa 15% ambapo muda mwingi wanakaa na wageni kwa muda mrefu Hadi wanaondoka nchini

Max ameeleza kuwa zipo changamoto wanazokutana nazo ni pamoja na kutokuwa na mikataba na mishahara kutoka kwa waajiri wao , bima ya Afya imekuwa changamoto kubwa kwao kwani hapo awali wali kuwa wanaipata kwa kifurushi kwa tsh 100,000 Ila kwa sasa kimefutwa

Tunakuomba utusaidie kwani hadi tunapozungumza wakati huu waongoza watalii wengi wamelala Vitandani hawana matibabu ,tunaomba suala la miundombinu ndani ya hifadhi kutoka Lodware getini hadi Karatu kuelekea Serengeti barabara hiyo imekuwa changamoto,pia hakuna huduma ya (picnic site)kwaajili ya huduma ya choo kwa wageni Jambo ambalo tunalazimika kuwashusha wageni porini kwani ni hatari kwajili ya wanyama na nyoka.

Dkt. Christopher Nzella Red Cross MKT wa Bodi ya TTGA:nimefika kilele cha mlima Kilimanjaro Mara 43 hawa waongoza watalii mhe.Waziri wanachangamoto nyingi haswa za kimaslahi, wanaweza kuharibi nchi au kuijenga nchi kutoka na na kile wanachokifanya, tunaomba uyaunganishe MAKUNDI haha wanashida wanapunjwa maslahi yao, na waajiri wao.

Vilevile Dkt. Nzella aliweza kuwasihi waongoza utalii Hao kuwa na Tania ya kujiwekea akiba akiba kwani uzee una kuja kesho kutwa huku akimsihi mhe. Waziri was Kara hiyoasiwasahau Bali awe anawatvelea Mara kwa Mara kwa Mara ili watoe changamoto zao.

Kwa upande wake mwenyekiti mstaafu wa TTGA 2012-2018 ndugu Alifa Msangi alisema kuwa mkutano huo umewela Historia kwenye taasisi hiyo tangia kimeanzishwa kwa Waziri kuwa morning rasmi na yupo tayari kufanyabkazi na waongoza watalii nchini kwa karibu zaidi.

"Yupo tayari kupokea changamoto zetu Sisi waongoza watalii ambao tunaonekana watu wa chini Sana Ila yeye ameonyesha anamaono kwenye sekta hiyo" Alisema Msangi

Nae Mwenyekiti wa TTGA Lembrice Loipuko mkutano huo ni mkutano wa kawaida wa mwaka ambao unalenga kuwasomea maps to na matumizi pamoja na kuangalia malengo mikakati waliyokuwa wamejiwekea kama imetekelezwa na kutaka kuwa na mbinu mbadala kwaajili ya kuendeleza ukuaji wa Utalii nchini kwa kupitia waongoza watalii
Katikati ni Mwenyekiti wa TTGA Tanzania Lebrice Loipoku kushoto kwake ni Karibu wa TTGA Tanzania Robert Max wakiteta jambo kabla ya kuanza kikao cha mkutano mkuu wa mwaka uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha Sauti Jijini Arusha




Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Angela Kairuki akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Taasisi ya waongoza Utalii Jijini Arusha alipowasili kwaajili ya mkutano mkuu wa mwaka



Hakuna hadithi nyingine zaidi ya Wewe kupata haki yako, Muhimu Njoo na Nyaraka zako zote na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda yupo tayari kukuhudumia na kupambana kwaajili yako dhidi ya wanaozuia haki yako kwa muda mrefu.

Mkuu wa Mkoa Mhe. Paul Christian Makonda anakualika na kukusihi usiwe mnyonge kwasababu haki yao inakwenda kupatikana kupitia Mawakili na Wanasheria wabobezi walioandaliwa kukusikiliza na kuhakikisha unaipata haki yako kikamilifu.

Ni fahari na Heshima kwa Mkuu wa Mkoa wetu Mhe. Paul Christian Makonda kukuhudumia na kupambana kuhakikisha unaipata Haki yakl na kuyafuta Machozi yako.Ni Kheri pia kukuhudumia wewe Mkazi wa Arusha Popote Pale Ulipo.

Karibu Kwenye Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuanzia majira ya saa Mbili asubuhi ili uhudumiwe na kufutwa Machozi kutokana na Haki unayoistahili na kwa bahati mbaya ilifichwa, kukandamizwa na kupokwa na watu wasiokutakia mema.

Kazi ni Moja tu kwa siku tatu mfululizo, kukusikiliza na kurejesha Haki yako iliyopotea.


  Picha ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Christian Makonda

07 Mei 2024, Dar es Salaam

Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) kimesema kuwa kimefurahishwa na Uamuzi wa Serikali wa kukubali ombi lililokuwa likiwasilishwa na Chama hicho la kuongeza Siku ya Likizo ya uzazi kwa Wafanyakazi Wanawake wanaojifungua watoto njiti kama ilivyotangazwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango alipokuwa Mgeni Rasmi wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani-Mei Mosi Kitaifa jijini Arusha.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo katika Tawi la TUGHE Hospitali ya Rufaa ya Temeke Jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa TUGHE Taifa, Dkt. Jane Madete amesema kuwa Wafanyakazi wanawake wanaojifungua watoto njiti wanapitia changamoto mbalimbali ikiwemo za kiafya, hivyo wanahitaji kupata muda mwingi wa kupumzika na pia kumuhudumia mtoto toka katika kipindi cha uangalizi hadi wanaporuhusiwa kutoka hospitalini ndiyo maana Chama cha TUGHE kwa kutambua hilo kiliamua kubeba ajenda hiyo na kuiomba Serikali iweze kuongeza siku za likizo ya uzazi ili kuleta tija sehemu za kazi.

“Kufuatia uamuzi huu tunaiomba serikali sasa ianze mchakato wa kufanya marekebisho katika Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini ambayo kwa sasa imekuwa ikitoa siku 84 kwa wanawake wanaojifungua mtoto mmoja na pia siku 100 kwa wanaojifungua zaidi ya mtoto mmoja. TUGHE tupo tayari kushiriki kikamilifu katika hatua zote za kuhakikisha uamuzi huu unaingia katika sheria hii” Alieleza Dkt. Madete

Kwa upande wa Sekta Binafsi, TUGHE imewaomba Waajiri nchini katika mikataba yao ya hali bora kuweka kipingele cha kuongeza muda kwa siku za likizo ya uzazi kwa wanaojifungua watoto njiti kama ambavyo mwishoni mwa mwaka jana 2023 Chama cha TUGHE waliweka kipengele hicho katika Mkataba wake wa Hali Bora na kuwa Chama cha kwanza cha Wafanyakazi Nchini kufanya hivyo katika Mkataba wake wa hali bora.

IMETOLEWA NA

IDARA YA HABARI NA UHUSIANO KWA UMMA

TUGHE MAKAO MAKUU






 

 

Kaimu Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bi. Martha Makala akizungumza na wazazi, wanafunzi na viongozi na wadau wa elimu katika mkutano wa majumuisho mara baada ya washiriki wa juma la elimu kutembelea shule za msingi Mgusu na Mshikamano pamoja na Shule ya Sekondari Mgusu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayoendelea mkoani Geita.

Kaimu Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Mji wa Geita, Bi. Linda Marandu akizungumza
na wazazi, wanafunzi na viongozi na wadau wa elimu katika mkutano wa majumuisho mara baada ya washiriki wa juma la elimu kutembelea shule za msingi Mgusu na Mshikamano pamoja na Shule ya Sekondari Mgusu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayoendelea mkoani Geita.


Baadhi ya wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) na wadau wa elimu wanaoshiriki Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayoendelea mkoani Geita wakiwa katika majadiliano na wanafunzi.

Afisa Elimu Watu Wazima Mkoa wa Geita, Bi. Salome Cherehani akizungumza na wazazi, wanafunzi na viongozi na wadau wa elimu katika mkutano wa majumuisho mara baada ya washiriki wa juma la elimu kutembelea shule za msingi Mgusu na Mshikamano pamoja na Shule ya Sekondari Mgusu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayoendelea mkoani Geita.

Baadhi ya wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) na wadau wa elimu wanaoshiriki Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayoendelea mkoani Geita wakiwa katika majadiliano na wanafunzi.


Kaimu Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bi. Martha Makala akisisitiza jambo alipokuwa kwenye mkutano na wazazi, wanafunzi na viongozi na wadau wa elimu katika mkutano wa majumuisho mara baada ya washiriki wa juma la elimu kutembelea shule za msingi Mgusu na Mshikamano pamoja na Shule ya Sekondari Mgusu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayoendelea mkoani Geita.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Juma la Elimu Kitaifa, ambaye pia ni Meneja Mawasiliano wa Shirika la Uwezo Tanzania, Bw. Greyson Mgoi (kulia) akizungumza kuwatambulisha wadau wa elimu walipotembelea baadhi ya shule ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yaliofanyika Mkoani Geita.

KAIMU Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bi. Martha Makala amewataka wazazi na walezi wa wanafunzi katika shule za msingi Mgusu na Mshikamano pamoja na Shule ya Sekondari Mgusu kuhakikisha wanafunzi katika shule hizo wanapata chakula wawapo shuleni.

Kauli hiyo, imetolewa leo mkoani Geita katika ziara ya wadau wa elimu wanaoshitiki Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayoendelea mkoani Geita, walipokuwa wakizitembelea shule hizo na kuzungumza na wazazi, wanafunzi, walimu pamoja na viongozi na wadau wa elimu. 

Alisema haki ya mtoto kupata chakula ni ya msingi hivyo ni jukumu la wazazi na walezi kuhakikisha wanakula ili waweze kusoma vizuri na hata kufaulu katika masomo yao, kwani mtoto akiwa na njaa hawezi kusoma na kuelewa kwa urahisi anachofundishwa na walimu.

"Naomba sana wazazi na walezi tuhakikishe kwamba watoto wetu wanakula wakiwa shuleni kwani watoto hawa muda mwingi wanautumia wakiwa shuleni tukiwaacha watoto hawa wakakaa na njaa wakiwa shuleni tunatengeneza matatizo ya kiafya kwao kama vidonda vya tumbo naomba tuchangie ili tuwanusuru," alisema Kaimu Mratibu wa TEN/MET, Bi. Makala akizungumza.

Aliongeza kuwa kiasi kinachotakiwa kuchangiwa kwa kila mzazi ni kilo moja ya mahindi na shilingi mia tano (500) tu kwa mwezi kiwango ambacho kinaweza kuchangiwa kwa kila mzazi kama amedhamiria kufanya hivyo. Kuna watoto 687 wanashinda na njaa kila siku wawapo shuleni huku wenzao 813 wanapata huduma ya uji shuleni kila siku. 

"...Ni vizuri mtoto asome akiwa ameshiba hapa anaweza kumsikiliza mwalimu vizuri, lakini tumboni akiwa hana kitu hawezi kumsikiliza mwalimu na kuelewa kirahisi...kwa hili nawasihi wazazi tusaidiane, Serikali inajitahidi kufanya kwa sehemu yake lakini wazazi na wadau wengine tuna kila sababu ya kuunga mkono juhudi hizo za Serikali"

Aidha aliongeza kuwa ushirikiano kati ya wazazi, walimu na viongozi wa elimu ndio njia pekee inayoweza kuchochea maendeleo ya elimu katika eneo hilo. 

Kwa upande wake, Kaimu Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Mji wa Geita, Bi. Linda Marandu alisema licha ya uwepo wa changamoto hiyo ya baadhi ya wazazi kutoitikia uchangiaji wa chakula eneo hilo, lakini bado Kata ya Mgusu inaongoza kufanya vizuri katika uchangiaji chakula ukilinganisha na kata zingine eneo hilo. 

Baadhi ya walimu wakizungumza na wadau wa elimu walipofanya ziara katika shule hizo.

Baadhi ya wazazi na wanafunzi wakiwa katika vikao na wadau wa elimu.

Baadhi ya wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) na wadau wa elimu wanaoshiriki Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayoendelea mkoani Geita wakiwa katika majadiliano na walimu.

Baadhi ya wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) na wadau wa elimu wanaoshiriki Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanayoendelea mkoani Geita wakiwa katika majadiliano na wanafunzi wa shule za msingi.

Kwa muda mrefu kinamama waliokuwa wanajifungua watoto kabla ya wakati (njiti) wamekuwa wakipatwa na hofu na mashaka kuhusu mustakabali wa maisha ya watoto wao kwakuwa inaelezwa wengi wa watoto hao walikuwa wakipoteza maisha kutokana na kukosa huduma bora za uangalizi kwa mama na mtoto.

Hata hivyo jambo hilo kwa sasa linaonekana kuwa historia kutokana na maboresho ya mifumo ya kitaalamu na uwepo wa Madaktari Bingwa wabobezi kwenye Hospitali mbalimbali za umma hapa nchini ambapo uangalizi dhidi ya watoto hao umekuwa ukifanywa kitaalamu zaidi.

Hilda Msigwa mkazi wa mkoa wa Songwe na Rose Masebo mkazi wa mtaa wa Mabatini Mbeya ni miongoni mwa kinamama mashuhuda, ambapo wawili hao kwa sasa wamelazwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya wakipatiwa uangalizi maalumu wa huduma ya Kangaroo baada ya kujifungua watoto wao kabla ya wakati (njiti) .

Katika maelezo yao wamesema kuwa watoto wao wamezaliwa wakiwa na gramu tano (5) ndani ya kipindi cha miezi miwili (2) pekee watoto hao wamefikisha kg 1.5 jambo ambalo limewapa faraja kubwa.

Wametumia nafasi hiyo kutoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna alivyofanikisha mageuzi makubwa kwenye sekta ya afya nchini ambayo yameokoa maisha ya watoto wengi waliozaliwa kabla ya wakati (njiti)




 

Na Mwandishi Wetu,Dodoma.


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amepokea msaada wa 13.7m/- kutoka kwa wanachama wa kundi sogozi(WhatsApp) liitwalo Viongozi Tanzania.

Akipokea msaada huo katika hafla hiyo iliyofanyika jana ofisini kwake Mei 6,2024,mjini Dodoma ,Dkt Yonazi amewashukuru wanachama wa kundi hilo kwa kujitoa kwao kwenda kwa waathirika hao wa maporomoko ya udongo, tope, mawe na magogo kutoka mlima Hanang mkoani Manyara yaliyotokea mwishoni mwa mwaka 2023.
Dkt.Yonazi amesema msaada huo,pamoja na misaada ya wasamalia wengine inaunga mkono jitihada za serikali zinazoendelelea katika kurejesha hali ya kawaida kwa waathirika hao ikiwemo kujengea nyumba 108, ili wanaendelee kujitafutia riziki na kujiletea maendeleo yao.

Aidha, Dkt. Yonazi ametoa wito kwa Watanzania wote kuendelea kuwa na desturi ya kuwakimbilia wahitaji pale ambapo wanapata athari za majanga mbalimbali.

"Tunawashukuru wenzetu wa kundi la Viongozi Tanzania kwa uzalendo waliouonesha kwa ajili ya mchango huu mkubwa walioutoa, niwaombe Watanzania wenzangu tuzidi kushikana mkono hasa nyakati hizi ambapo sehemu nyingi nchini yametokea majanga mbalimbali,hivyo ni  jambo jema kuendelea kushirikiana kuwasaidia ndugu zetu, "alisema Dkt. Yonazi

Wajumbe wawili wa kundi hilo ambao ni Ndg.Benjamin Thompson, ambaye ndiye Mratibu Mkuu wa kundi hilo, pamoja na Mhandisi Archard Kato,ambaye ni mmoja wa Wanachama wa kundi hilo, waliwawakilisha wanachama wengine zaidi ya 600 walioko kwenye kundi hilo, ambao ni viongozi mbalimbali wa serikali,viongozi wa taasisi za umma,viongozi wa sekta binafsi,wahadhiri na viongozi wa vyuo vikuu,viongozi wa vyama vya siasa,viongozi wadiaspora n.k

Bw.Thompson alisema michango hiyo ilikusanywa kutoka kwa wanachama 145 tu kati ya wote walioko kwenye wa kundi hilo, ambao ndio waliweza kuchangia kwa wakati huo.
"Mkusanyaji wetu alikuwa ni Zamaradi Kawawa,ambaye alifanya kazi nzuri sana na kwa uaminifu mkubwa.Baada ya kumaliza kazi hiyo,tulikubaliana kwamba aweke pesa hizo kwenye akaunti ya maafa iliyopo chini ya ofisi ya Waziri Mkuu,na aliweka pesa hizo Desema 27,2023.Sasa hili lililofanyika hapa leo lilikuwa ni kukabidhi tu karatasi ya malipo yaani pay in slip",alisema Bw Thompson.

Naye Mhandisi Kato,  ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya kutengeneza mvinyo ya Alko Vintages iliyopo Dodoma, alisema wanachama wa kundi hilo wameguswa na janga hilo la Hanang na hivyo kuona umuhimu wa kutoa michango hiyo katika kuunga mkono juhudi za serikali za kukabiliana na majanga kama hayo.
"Tunakuahidi kwamba tutaendelea kuisaidia serikali kwa kidogo tulicho nacho katika kukabiliana na athari za majanga kama haya,na tungependa kuona hili jambo linaenea kwa watanzania wengi,yaani hata kabla ofisi yako haijafika au serikali haijafika, angalau watanzania wenyewe wawe wanafanya jambo la mwanzo kwa uzalendo wao katika kukabiliana na mambo hayo hasa ya dharula ambayo hakuna mtu ambaye amepanga yatokee hasa hasa mafuriko,"alisema Mhandisi Kato.

Janga la Hanang lilitokea Desemba 3, mwaka jana mkoani Manyara na kusababisha vifo ya watu zaidi ya 80, huku mamia wengine wakiachwa bila makazi, uharibifu mkubwa wa miundombinu.




 


Top News