Na mwandishi wetu, Ngorongoro

Watendaji Wakuu wa Taasisi za Serikali na mashirika ya Umma wametembelea Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kwa lengo la kufanya utalii wa ndani kuona vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo Ngorongoro ambayo ni kivutio bora cha utalii Africa mwaka 2023 na 2025.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo kaimu mwenyekiti wa CEOs Forum ambae pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TanTrade) Bw. Ephraim Balozi Mafuru amesema pamoja na utalii ziara hiyo imewapa nafasi ya kutumia jukwaa la wakuu wa taasisi kujadili na kuatafakari kwa pamoja namna bora ya kutekeleza dira ya taifa ya maendeleo 2050.

“Kama viongozi tumeona tuje kuhamasisha utalii wa ndani kwa kutembelea Ngorongoro ili kuongeza hamasa kwa jamii katika kuchangia kukuza sekta ya utalii, tumepata fursa ya kujadili michango ya taasisi za serikali na binafsi katika kufanikisha Dira ya 2050”. alisema Mafuru

Ziara hiyo imefanyika mara baada ya kukamilika kwa Kikao Kazi cha CEO Forum 2026, kilichofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), na kuwakutanisha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi, Mashirika ya Umma na Wakala za Serikali kujadili masuala mbalimbali yanayohusu ufanisi wa utendaji, uwajibikaji na mchango wa taasisi za umma katika kufanikisha utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Meneja uhusiano wa NCAA Hamis Dambaya ameeleza kuwa ujio wa viongozi hao umekuwa ni fursa muhimu ya kuendelea kuitangaza Ngorongoro kama eneo lenye thamani kubwa ya uhifadhi, utalii, historia na elimu huku ikiendelea kuimarisha uelewa wa wadau kuhusu kuendeleza utalii endelevu na kuhakikisha rasilimali zinazopatikana ndani ya eneo la Ngorongoro zinaendelea kutoa manufaa kwa Taifa bila kuathiri thamani yake kwa vizazi vijavyo.



-Apigia chapuo utekelezaji wa DIRA 2050


WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amesema bado kuna fursa nyingi za ushirikiano wa kiuchumi baina ya Taifa la Qatar na Tanzania ambazo zikitumiwa vizuri zitawanufaisha raia wa nchi zote mbili.

“Bado tuna fursa nyingi ambazo tunaweza tukanufaika nazo kama tutatekeleza baadhi ya shughuli za kiuzalishaji. Tanzania kama lango la Afrika Mashariki, Kusini na Kati na Qatar kama lango la Mashariki ya Kati na Umoja wa Nchi za Ghuba tulikubaliana kuwa tukichangamkia fursa zote zinazojitokeza, tutaongeza ushiriki wa wananchi wa nchi zote mbili,” alisema.

Alikuwa akizungumza na Rais na Mtendaji Mkuu wa Power International Holding (PIH), Bw. Ramez Al-Khayyat na baadhi ya viongozi wakuu wa taasisi hiyo kwenye makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo Lusail, jijini Doha.

Waziri Mkuu alimshukuru Rais na Mtendaji Mkuu wa PIH kwa kuonesha nia ya dhati ya kuwekeza katika sekta ambazo DIRA 2050 imeyaainisha kama maeneo ya kipaumbele.

“Tunashukuru kwamba hii kampuni imeonesha nia ya kuwekeza kwenye maeneo yaliyotajwa katika DIRA 2050 ambayo na sisi tumeyawekea kipaumbele. Wameonesha nia ya kushiriki DIRA yetu kupitia utekelezaji wa fursa zilizopo. Tumekubaliana kwamba mawaziri waliopo wakiongozwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mheshimiwa Kapinga wafuatilie kwa karibu ili utekelezaji uanze mara moja.”

Kwa upande wake, Rais na Mtendaji Mkuu wa PIH, Bw. Ramez Al-Khayyat alimweleza Waziri Mkuu kwamba Power International Holding ni kampuni kubwa ya kimataifa inayomilikiwa na watu binafsi ambayo inaendesha kampuni tanzu 400 zenye wafanyakazi 65,000 katika nchi 26.

Kati ya nchi 26, za Afrika ni Misri, Libya, Morocco, Algeria, Mauritania na Rwanda. Alisema wameshaingia makubaliano na Ethiopia (ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa) na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (ujenzi wa barabara yenye urefu wa km. 400).

“Utendaji kazi wa taasisi yetu umegawanyika katika makundi makubwa saba ya kibiashara yanayoendeshwa kimataifa na yenye kampuni tanzu 400 na wafanyakazi 65,000. Kwa sehemu kubwa, shughuli zetu zinajihusisha na madini, ujenzi wa miundombinu mikubwa, ujenzi wa majengo ya makazi pamoja na hoteli, kilimo na viwanda, utalii na utoaji huduma za mawasiliano,” alisema

Mapema, akitoa taarifa kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara, Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE, Bw. Ephraim Mafuru alisema kwa muda mrefu Tanzania ilikuwa ikisafirisha nyama ya mbuzi na kondoo kwenda nchi za Ghuba lakini kwa sasa inaweza kufanya vizuri zaidi endapo itaongeza mazao ya kilimo na madini hasa ya dhahabu.

“Tunalo soko kubwa la dhahabu ambalo kimsingi halijatumiwa. Tunajua soko liko hapa katika Ghuba. Lakini pia kuna fursa kubwa kwenye mchele ambao unaweza kutuingizia dola bilioni 3.9. Mwaka jana, tulizalisha tani milioni 3.4 za mchele na tukatumia tani milioni 1.8 tu. Maana yake ni kwamba tuna zaidi ya tani milioni 1.6 ambazo tunaweza kuzisambaza kwa watu milioni 3.4 waishio nchini Qatar.”

Akielezea kuhusu fursa za uwekezaji nchini Tanzania, Bw. Mafuru aliyataja maeneo hayo kuwa ni nishati, LNG, utalii, mbogamboga na matunda, maua, uzalishaji wa malisho ya mifugo pamoja na mazao yanayotokana na uchumi wa bluu.

Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu alifuatana na Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga; Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar; Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Ngwaru Maghembe, Katibu Wakuu (OR-Uwekezaji), Wakuu wa Mikoa ya Pwani na Dodoma, Wabunge Esther Matiko na Subira Mgallu na watendaji wengine wa Serikali.






Na Seif Mangwangi, Michuzi Tv Arusha

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, amesema mkutano wa Umoja huo unaofanyika jijini Arusha ni fursa kubwa kwa Tanzania kujitangaza kimataifa kupitia diplomasia ya kibunge, utalii na namna nchi inavyoshirikisha makundi mbalimbali katika uongozi na meza za maamuzi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo 1Oktoba 2026, Jijini Arusha alipotua kwaajili ya maandalizi ya mkutano huo unaoanza Oktoba 5 mwaka huu, Dkt. Tulia amesema mkutano huo unaowakutanisha wabunge na viongozi kutoka zaidi ya nchi 180 duniani.

Dkt Tulia amesema mkutano huo umeifanya Tanzania kuwa sehemu muhimu ya mijadala ya kimataifa, huku wajumbe hao wakipata nafasi ya kujifunza kuhusu Tanzania na Watanzania nao kupata fursa ya kujifunza kutoka kwa mataifa mbalimbali.

Amesema uwepo wa zaidi ya wageni 2,000 nchini ni fursa ambayo Tanzania inapaswa kuitumia kuwaonyesha wageni hao uwezo wa nchi katika kuandaa mikutano mikubwa ya kimataifa, pamoja na ukarimu wa Watanzania.

Kwa mujibu wa Dkt. Tulia, mkutano huo pia umeipa Tanzania nafasi ya kuonyesha namna inavyoshirikisha wanawake katika uongozi, akibainisha kuwa nchi inaongozwa na mwanamke, jambo ambalo ni sehemu ya uzoefu ambao dunia inaweza kujifunza kutoka Tanzania.

Amesema pamoja na wanawake, Tanzania imekuwa ikitoa nafasi kwa vijana na watu wenye ulemavu kushiriki katika michakato ya maamuzi, akisisitiza umuhimu wa kuhakikisha makundi mbalimbali yanapata nafasi katika uongozi.

Dkt. Tulia amesema Tanzania inapaswa kutumia uwepo wa wajumbe hao kuhakikisha wanarejea tena nchini baada ya mkutano, si kwa ajili ya mikutano pekee, bali pia kwa shughuli za utalii, biashara na maeneo mengine ya uwekezaji.

Amesema kuchaguliwa kwa Arusha kuwa mwenyeji wa mkutano huo kumeipa Tanzania nafasi ya kuwawezesha wageni kuona kwa macho yao vivutio vya utalii ambavyo awali walikuwa wakivisikia kupitia simulizi.

“Tunataka warejee tena, si kwa ajili ya mikutano pekee, bali pia kwa ajili ya utalii na shughuli nyingine,” amesema Dkt. Tulia.

Ameeleza kuwa mkutano huo pia ni sehemu ya kuimarisha diplomasia ya kibunge ya Tanzania, huku wajumbe kutoka mataifa mbalimbali wakipata nafasi ya kufahamu namna Tanzania inavyoendesha shughuli zake za kibunge na kushughulikia masuala ya kitaifa na kimataifa.

Katika hatua nyingine, Dkt. Tulia amesema Tanzania imechangia mabadiliko mbalimbali ya kanuni na taratibu za uendeshaji wa Umoja wa Mabunge Duniani katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake.

Amesema mabadiliko hayo yamewezesha Umoja huo kupata nafasi pana zaidi ya kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili dunia, tofauti na ilivyokuwa awali ambapo wakati mwingine wajumbe walilazimika kuchagua suala moja pekee kati ya masuala kadhaa yaliyokuwa yakihitaji kujadiliwa.

Dkt. Tulia ametolea mfano majanga yanayosababishwa na mabadiliko ya tabianchi katika maeneo mbalimbali duniani, akisema mfumo ulioboreshwa sasa unaruhusu mijadala kuhusu changamoto hizo kufanyika kwa upana bila kulazimika kuacha suala moja ili kujadili jingine.

Amesema mabadiliko hayo pia yameongeza nafasi ya kujadili masuala ya amani na usalama yanayoendelea katika maeneo mbalimbali duniani, ikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Sudan, Ukraine, Iran na maeneo mengine.

Kwa mujibu wa Dkt. Tulia, Tanzania inaona umuhimu wa mijadala hiyo kwa kuwa migogoro na changamoto za kiusalama katika baadhi ya maeneo zinaweza kuwa na athari kwa nchi nyingine na jamii ya kimataifa kwa ujumla.

Aidha, amesema Tanzania imechangia katika kukuza ushiriki wa wanawake ndani ya mabunge duniani, akieleza kuwa baadhi ya nchi ambazo awali hazikuwa na wanawake katika mabunge yao zimeanza kufanya mabadiliko baada ya juhudi za kuhamasisha ushiriki wao.

Dkt. Tulia amesema katika mkutano huo, ambao unatarajiwa kuwa na zaidi ya wageni 2,000, umewekwa utaratibu wa kuhakikisha wanawake na vijana wanashiriki, akieleza kuwa hatua hiyo inalenga kuhakikisha mijadala ya Umoja wa Mabunge Duniani inawakilisha makundi mbalimbali ya jamii.






•Asema maandalizi yamekamilika, washiriki zaidi ya 2,000 kuhudhuria kutoka mabunge 183

Na Vero Ignatus, Michuzi TV – Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, CPA Amos Gabriel Makalla, amemhakikishia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Balozi Anda Cristina Filip, kuwa Mkoa wa Arusha umekamilisha maandalizi ya kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani, unaotarajiwa kuanza Oktoba 5, 2026, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC).

Akizungumza leo, Alhamisi, Oktoba 1, 2026, alipokutana na Balozi Anda ofisini kwake jijini Arusha, RC Makalla amesema mkoa umejiandaa kwa muda mrefu kuhakikisha mkutano huo unafanyika kwa mafanikio ambapo Mkutano huo ni wa kihistoria kwa Tanzania kwa kuwa ni mara ya kwanza kuandaa mkutano huo wa kimataifa.

RC Makalla amesema kuwa usalama wa washiriki ni kipaumbele, akisisitiza taasisi mbalimbali zimeunganisha nguvu kuhakikisha maandalizi yote muhimu yanakamilika kwa wakati ambapo mkutano huo unatarajiwa kutoa fursa kwa wajumbe kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya kibunge na kuimarisha ushirikiano kati ya mabunge ya nchi wanachama.

Balozi Anda pia ameeleza matumaini yake kuwa mkutano huo utafanikiwa na washiriki watapata nafasi ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii nchini, hatua inayoweza kuwapa fursa ya kuifahamu Tanzania na vivutio vyake.

Kufanyika kwa mkutano huo jijini Arusha kunaipa Tanzania fursa ya kuandaa jukwaa muhimu la kidiplomasia na kibunge linalowakutanisha viongozi kutoka mataifa mbalimbali.

Kwa Arusha, maandalizi hayo yanaweka mkoa katika nafasi ya kupokea wageni wa kimataifa, huku mafanikio ya mkutano yakitarajiwa kutegemea ushirikiano wa taasisi husika, usalama na utekelezaji wa ratiba ya shughuli zilizopangwa.








Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Dkt. Zakia Mohammed Abubakar akihutubia wakati wa ufungaji wa mafunzo Mkoani Tabora leo tarehe 01 Oktoba, 2026 kwa watendaji wa uchaguzi yaliyofanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 29 Septemba hadi 01 Oktoba, 2026.

Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Dkt. Zakia Mohammed Abubakar akihutubia wakati wa ufungaji wa mafunzo Mkoani Tabora leo tarehe 01 Oktoba, 2026 kwa watendaji wa uchaguzi yaliyofanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 29 Septemba hadi 01 Oktoba, 2026. Katikati ni Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele na Kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ndg. Ramadhani Kailima.

Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Dkt. Zakia Mohammed Abubakar akihutubia wakati wa ufungaji wa mafunzo Mkoani Tabora leo tarehe 01 Oktoba, 2026 kwa watendaji wa uchaguzi yaliyofanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 29 Septemba hadi 01 Oktoba, 2026. Katikati ni Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele.

Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ndg. Ramadhani Kailima.
Mwenyekiti wa Mafunzo, Ndg Godfrey Mnyamale akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo.

*****Na. Mwandishi Wetu, Tabora
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imetoa wito kwa watendaji wa uchaguzi kuhakikisha wanafanya kazi kwa ufanisi, weledi na kujitoa ili kufanikisha zoezi la uchaguzi kwenye Jimbo la Chamwino na kata 11 za Tanzania Bara.

Wito huo umetolewa na Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Dkt. Zakia Mohammed Abubakar Mkoani Tabora leo tarehe 01 Oktoba, 2026 wakati akifunga mafunzo ya watendaji wa uchaguzi yaliyofanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 29 Septemba hadi o1 Oktoba, 2026.

“Ni matazamio ya Tume kwamba, baada ya kupatiwa mafunzo haya, mtatekeleza majukumu yenu kwa ufanisi na weledi mkizingatia ratiba ya utekelezaji ili kufanikisha uchaguzi mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Chamwino na Madiwani katika kata 11 za Tanzania Bara, unaotarajiwa kufanyika tarehe 04 Novemba, 2026,” amesema.

Dkt. Zakia amewakumbusha watendaji hao kuwa shughuli zote za uchaguzi zinaongozwa na Katiba, sheria, kanuni, maadili ya uchaguzi na maelekezo ya Tume na kuwasihi kuendelea kutenga sehemu ya muda wao kusoma Katiba, sheria na maelekezo mbalimbali yanayotolewa na Tume ili yawaongoze katika kusimamia uchaguzi utakaokuwa huru na wa haki.

Amesisitiza kuwa ili ufanisi uwepo ni muhimu watendaji hao wakazingatia sifa na uwezo wakati wa kuteua na kuajiri watendaji wa vituo vya kupigia kura kwa kuwa hao ndio watakaosimamia zoezi la kupiga kura na kuhesabu kura vituoni.

“Kuhusu utaratibu wa kupata watendaji wa vituo, tunayo imani kuwa mtateua na kuajiri watendaji wenye sifa na uwezo wa kufanya kazi hii muhimu kwa mustakbali wa Taifa letu. Jambo hili limekuwa likisisitizwa tokea siku ya kwanza ya mafunzo kwa kuwa hao ndio watakaosimamia zoezi la kupiga kura na kuhesabu kura vituoni. Kazi ambayo inahitaji umahiri, umakini na weledi katika kuitekeleza,” amesema Dkt. Zakia.

Amewataka watendaji hao kuhakikisha kuwa mafunzo ya watendaji wa vituo yanafanyika kwa ufanisi na weledi katika tarehe zilizopangwa kwenye ratiba ya utekelezaji wa shughuli za uchaguzi.

Mafunzo hayo yamewahusisha Waratibu wa Uchaguzi wa Mikoa, Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi Ngazi ya Jimbo, Wasimamizi wa Uchaguzi Ngazi ya Kata, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ununuzi na Wahasibu.

Kata 11 za Tanzania Bara zitakazofanya uchaguzi wa Udiwani ni Nonde iliyopo Halmashauri ya Jiji la Mbeya; Lugenge, Halmashauri ya Mji Njombe; Bargish, Halmashauri ya Mji Mbulu; Makole, Halmashauri ya Wilaya ya Muheza; Mwera, Halmashauri ya Wilaya ya Pangani na Oldonyosambu, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro.

Nyingine ni Igalula iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Uyui; Shelui, Halmashauri ya Wilaya ya Iramba; Mvumi, Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa; Nyarero, Halmashauri ya Wilaya ya Tarime na Ilolangulu, Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe.
Mkufunzi akiwasilisha mada kuhusu mapokezi na utunzaji wa vifaa vya Uchaguzi.
Mmoja wa wakufunzi akiwasilisha mada kuhusu matumizi ya fedha za Uchaguzi.



Washiriki mbalimbali wa mafunzo hayo wakifatilia mafunzo kwa umakini.

Mkufunzi wa mafunzo hayo akiwasilisha mada kuhusu usimamizi wa fedha za Uchuzi.



Washiriki mbalimbali wa mafunzo hayo wakifatilia mafunzo kwa umakini.





Washiriki mbalimbali wa mafunzo hayo wakifatilia mafunzo kwa umakini.

Kampuni ya Mkuyu Africa imewaleta karibu Watanzania wanaofanya shughuli mbalimbali nchini Dubai kwa lengo la kuwajengea uelewa kuhusu fursa za uwekezaji nchini Tanzania, hususan katika sekta ya ardhi na majengo.

Hatua hiyo imekuja wakati ambapo biashara na mahusiano ya kiuchumi kati ya Tanzania na Dubai yakiendelea kukua, huku wafanyabiashara wengi kutoka Tanzania wakifika katika nchi za Falme za Kiarabu, hasa Dubai, kutafuta bidhaa na fursa za biashara, ikiwamo nguo, bidhaa za thamani na mapambo ya ndani pamoja na kazi za viwandani

  

Katika kuunga mkono jitihada hizo, MKUYU AFRCA  iliandaa kongamano lililowakutanisha wafanyabiashara wadogo wenye asili ya Tanzania wanaoishi Dubai, ambapo walijadili namna wanavyoweza kutumia fursa wanazozipata ughaibuni kuwekeza nyumbani.

Lengo lingine la kongamano hilo lilikuwa kuwapa washiriki uelewa kuhusu fursa zilizopo katika sekta ya ujenzi na mali isiyohamishika, pamoja na namna Watanzania wanaoishi nje ya nchi wanavyoweza kumiliki mali nchini kupitia mifumo rasmi ya kifedha.

Akizungumza katika kongamano hilo, Mkurugenzi wa Mkuyu Africa, Juneid Othman, alisema Watanzania waliotoka nchini miaka 10 iliyopita wanaweza kushangazwa na kasi ya maendeleo katika sekta ya ujenzi nchini.

Alisema sekta hiyo imekua kwa kiasi kikubwa, ikiwamo ujenzi wa majengo marefu, nyumba za makazi na miradi ya nyumba za kupangisha, hasa katika maeneo ya kibiashara kama Kariakoo chini ya mradi wa Nkurumah  na maeneo ya kifahari kama Masaki.

“Ukitoka Tanzania miaka 10 iliyopita na ukarudi leo, unaweza kushangazwa na mabadiliko makubwa yaliyotokea katika sekta ya ujenzi. Kuna maendeleo makubwa katika ujenzi wa majengo ya biashara, makazi na nyumba za kupangisha,” alisema.

Juneid alisema pia mazingira ya uwekezaji yameendelea kutoa fursa kwa Watanzania kumiliki mali kupitia benki na taasisi mbalimbali za kifedha.

Alitoa mfano wa miradi ya Mkuyu Africa katika maeneo ya Kariakoo na Masaki, akisema kampuni hiyo inaendelea kushiriki katika ujenzi na uendelezaji wa majengo ya makazi na biashara.

Alisema fursa hizo zinapaswa kutumiwa na Watanzania wanaoishi nje ya nchi, akisisitiza kuwa uwekezaji katika mali nchini unaweza kuwa sehemu ya maandalizi ya maisha yao ya baadaye pamoja na kujenga urithi kwa vizazi vijavyo.

Wafanyabiashara Dubai wataka kuwekeza nyumbani

Mfanyabiashara wa bidhaa za thamani na mapambo ya ndani nchini Dubai, Ashraf Mohamud, alisema Watanzania wengi wanaoishi Dubai wanaendelea kufanya biashara na kutafuta mitaji kwa lengo la baadaye kuwekeza nchini.

Alisema ujio wa Mkuyu Africa nchini Dubai umewapa motisha na taarifa zaidi kuhusu fursa zilizopo nchini, jambo ambalo, kwa mujibu wake, linawasaidia kupanga namna ya kuanza kuwekeza nyumbani.

“Tumekuja Dubai kutafuta maisha na kufanya biashara, lakini moja ya malengo yetu ni kupata mtaji na kuja kuwekeza nyumbani. Ujio wa Mkuyu Africa umetupa hamasa na kutufanya tuanze kufikiria kwa umakini zaidi kuhusu uwekezaji nchini,” alisema.

Malipo kwa awamu

Ashraf alisema Watanzania wengi wanaoishi Dubai wana hamu ya kuwekeza Tanzania, lakini baadhi yao wamekuwa wakikumbana na changamoto pale wanapowatumia ndugu fedha kwa ajili ya kununua ardhi au kujenga nyumba.

Alisema hali hiyo imewafanya baadhi yao kutafuta njia mbadala zitakazowawezesha kufanya uwekezaji moja kwa moja na kwa utaratibu unaoeleweka.

“Watanzania wengi wanaoishi huku wanatamani kuja kuwekeza nchini, lakini hapo awali kumekuwa na changamoto na wakati mwingine urasimu, hasa pale tunapowatuma ndugu zetu fedha kwa ajili ya uwekezaji,” alisema.

Aliongeza kuwa fursa zinazotolewa na kampuni kama Mkuyu Africa, ikiwamo uwezekano wa kumiliki mali kupitia taasisi za kifedha na kulipa kwa awamu kulingana na masharti yaliyowekwa, zinaweza kuwasaidia Watanzania waishio nje ya nchi kuwekeza kwa utaratibu rasmi.

Kwa mujibu wa washiriki wa kongamano hilo, uwekezaji nchini Tanzania unapaswa kuonekana kama sehemu ya kujenga maisha ya baadaye, kuongeza thamani ya mitaji na kuweka msingi wa mali kwa ajili ya familia na vizazi vijavyo.

Mkurugenzi wa kampuni ya MKUYU AFRICA ,Juneid Othmani akizungumza wakati wa kongamano la wafanyabiashara wenye asili ya Tanzania  waishio Duba


Na Mwandishi wetu, Geita

NAIBU Waziri wa Madini, Dkt Steven Lemomo Kiruswa ameitaka kampuni ya Waja General LTD inayomilikiwa na Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini, mhandisi Chacha Wambura kusambaza huduma ya vifaa vya uchimbaji nchi nzima ili wachimbaji wote waweze kupata vifaa hivyo kwa urahisi.

Naibu Waziri Dkt Kiruswa ameeleza hayo alipotembelea banda la Waja General Company LTD kwenye maonyesho ya tisa ya kitaifa ya teknolojia ya madini yanayofanyika katika viwanja vya Dkt Samia Suluhu Hassan, manispaa ya Geita.

Amesema Wambura ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, anapaswa kusambaza huduma hiyo nchi nzima ili wachimbaji waweze kupata vifaa bora vya uchimbaji kwa urahisi.

"Mheshimiwa mhandisi Chacha wewe ni mjumbe wa Kamati yangu ya Nishati na Madini nakuomba usambaze vifaa hivyo nchi nzima ili wachimbaji waweze kunufaika kwa wingi," amesema Dkt Kiruswa.

Hata hivyo, mhandisi Wambura ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kupitia Mkoa wa Geita alikubali ombi hilo la Naibu Waziri wa Madini.

"Hakuna shaka mheshimiwa Naibu Waziri kwa sababu sisi ndiyo watu wa kwanza kusambaza huduma hizo hapa Geita, tunaweza kusambaza pia kwa wachimbaji wengine," amesema mhandisi Wambura.

Kwa upande wake, Afisa wa kampuni tanzu ya Waja General LTD, Juline Ngowi akizungunza mbele ya mgeni rasmi Naibu Waziri wa Madini DKt Kiruswa amesema kampuni hiyo inajihusisha na kutoa huduma mbalimbali kwa jamii.

Ngowi ametaja baadhi ya huduma hizo ni shule ya sekondari Waja, Waja General michofines, bima za nyumba na makazi, uhandisi, maisha na afya.



  


VIWANJA mbalimbali kuwaka moto siku ya leo kushuhudia mitanange ya moto kwelikweli. Pointi 3 zinawaniwa na timu tofauti tofauti. Unasubiri nini kutengeneza jamvi lako la ushindi?

Mechi za Kimataifa zinaendelea ambapo kule Ulaya michuano ya UEFA Nations League inaendelea ambapo Ujerumani atakuwa nyumbani kumenyana vikali dhidi ya Serbia ambapo kwenye kundi lao wao ndio wapo nafasi ya mwisho huku tofauti yao ikiwa ni pointi 1.

Timu hiyo ya Ujerumani chini ya Klopp inaingia kwenye mchezo huu ikiwa katika kipindi cha mpito. Jürgen Klopp amechukua timu hiyo baada ya Kombe la Dunia la 2026 na anajaribu kujenga timu yenye nguvu zaidi kuelekea Euro 2028. Katika michezo yake ya mwanzo, Klopp amekuwa akitafuta namna bora ya kuchanganya wachezaji wenye uzoefu na vipaji vipya. Suka jamvi mechi hii.

Kwa upande wa Serbia ni timu yenye nguvu kimwili na inaweza kuwa hatari kupitia mashambulizi ya kushtukiza. Wanahitaji kuwa na nidhamu katika ulinzi na kutumia vizuri mipira ya mwisho wanapopata nafasi. Kiungo kitakuwa eneo muhimu kwa sababu timu itakayolitawala eneo hilo inaweza kupata udhibiti mkubwa wa mchezo.

Kila timu inahitaji kupata ushindi siku ya leo, kwani pointi 3 ni muhimu sana kwa pande zote mbili. Je nani kushinda?. Jisajili hapa.

Mkwanja mnono upo kupitia michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Mtanange mwingine ni huu wa Ugiriki dhidi ya Uholanzi ambapo hawa wote wapo kwenye Kundi A na kila timu leo hii inahitaji kupata ushindi kwenye mchezo huu ili iweze kujiweka kwenye nafasi nzuri kundini.

Ugiriki ni timu ambayo inaweza kuingia mchezoni kinidhamu zaidi, na kufanya mashambulizi ya kushtukiza pale inapopata nafasi. Ufanisi wao mbele ya lango utakuwa muhimu, kwa sababu huenda wasipate nafasi nyingi za kufunga kutokana na mpinzani ambaye wanaenda kukutana naye.

Kwa upande wa Uholanzi wao chini ya kocha mkuu Xavi Hernandezi, nguvu yao kubwa iko kwenye kasi ya kushambulia, ubunifu wa viungo na uwezo wa kutumia nafasi kwenye maeneo ya pembeni. Wanatarajiwa kujaribu kuutawala mchezo mapema na kuilazimisha Ugiriki kujilinda kwa muda mrefu.

Hata hivyo, wakishindwa kutumia nafasi zao, Ugiriki inaweza kuwaadhibu kupitia counter-attacks. Hivyo, mchezo huu unaweza kuamuliwa zaidi na umakini wa ulinzi na ubora wa kumalizia nafasi.

Tofauti yao mpaka sasa ni 2 pekee huku takwimu zikionesha kuwa mechi mbili mara ya mwisho kukutana Uholanzi ameondoka na ushindi meci zote mbili, hivyo huenda hii ndio mechi ya kisasi kwa Ugiriki. Beti hapa.

Lakini pia mechi nyingine ambao unaweza kukupatia pesa ni Denmark dhidi ya Ureno ya Cristiano Ronaldo ambao kwenye mechi mbili wameshinda zote hivyo wameanza vyema kabisa kwenye michuano hii.

Denmark inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na faida ya kucheza nyumbani, hivyo itahitaji kutumia nguvu na kasi ya wachezaji wake wa pembeni kuiwekea Ureno presha kwani wana wachezaji wengi wazuri wakiwemo Højlund na wengine.

Ureno ina ubora mkubwa katika eneo la kiungo kupitia Bruno Fernandes, Vitinha na Joao Felix, pamoja na uzoefu wa Cristiano Ronaldo katika safu ya ushambuliaji hivyo inawafanya kuwapa faidi zaidi.

Hata hivyo, kucheza ugenini dhidi ya Denmark kutahitaji umakini mkubwa katika ulinzi na matumizi mazuri ya nafasi. Kwa ujumla, tunatarajia mchezo wenye ushindani mkubwa ambao unaweza kuamuliwa na ubora wa timu katika dakika za mwisho. Nani kushinda leo?. Jisajili hapa.
Na, Mwandishi wetu – Ankara, Uturuki

SERIKALI ya Tanzania imesema itaendelea kuimarisha ushirikiano na Mamlaka ya Usimamizi wa Maafa na Dharura ya Uturuki (AFAD), kwa lengo la kuimarisha uwezo wa nchi katika kuzuia na kupunguza athari za maafa, kujiandaa, kukabiliana na dharura na kurejesha hali baada ya maafa kutokea.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Watu Wenye Ulemavu), Dkt. Jim Yonazi, wakati wa kikao cha pamoja kati ya ujumbe wa Serikali ya Tanzania na uongozi wa AFAD kilichofanyika katika ofisi za taasisi hiyo mjini Ankara, Uturuki ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi nchini humo iliyolenga kuongeza ujuzi na maarifa ya kiufundi, kuimarisha uwezo wa kitaasisi, kujifunza uzoefu wa Uturuki katika kupunguza vihatarishi vya maafa, kujiandaa na kukabiliana na dharura, pamoja na kurejesha hali baada ya maafa kwa kutumia mbinu, mifumo na teknolojia za kisasa.

Dkt. Yonazi amesema Tanzania inathamini uzoefu na utaalamu wa AFAD katika usimamizi jumuishi wa maafa na kwamba Serikali itaendelea kuimarisha ushirikiano huo kwa manufaa ya Tanzania na Uturuki, hususan katika kuendeleza mifumo ya kisasa ya usimamizi wa maafa, teknolojia, mafunzo ya wataalam, utafutaji na uokoaji pamoja na uratibu wa hatua za mwitikio wakati wa dharura.

“Tanzania itaendelea kujifunza na kushirikiana na taasisi mbalimbali zenye uzoefu katika usimamizi wa maafa, ikiwemo AFAD, ili kuimarisha uwezo wa kitaifa wa kuzuia na kupunguza athari za maafa, kujiandaa, kukabiliana na kurejesha hali pindi yanapotokea,” amesema Dkt. Yonazi.

Kwa upande wake, Mkuu wa AFAD nchini humo, Gavana Ali Hamza Pehlivan, ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendeleza ushirikiano na Uturuki katika eneo la usimamizi wa maafa na kueleza kuwa AFAD ipo tayari kuendelea kushirikiana na Tanzania katika maeneo mbalimbali ya kitaalamu.

Gavana Pehlivan amesema maeneo hayo ni pamoja na matumizi ya teknolojia za kisasa katika usimamizi wa maafa, mifumo ya ufuatiliaji na tathmini ya vihatarishi na madhara ya maafa, maandalizi na mwitikio wa dharura, pamoja na uanzishaji, mafunzo na uendelevu wa timu maalumu za utafutaji na uokoaji na upatikanaji wa vifaa vinavyohitajika wakati wa maafa.

Ameeleza kuwa AFAD inatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia dhana ya usimamizi jumuishi wa maafa, inayolenga kushughulikia hatua zote za mzingo wa usimamizi wa maafa, kuanzia katika kutambua na kutathmini vihatarishi, kuzuia na kupunguza uwezekano na athari za maafa, kujiandaa, kukabiliana na dharura hadi kurejesha hali pindi maafa yanapotokea.

Vilevile, AFAD imejenga uwezo wa kuratibu timu za wataalam na vikosi vya utafutaji na uokoaji vinavyoshughulikia majanga mbalimbali, yakiwemo matetemeko ya ardhi, mafuriko na dharura nyingine, kwa lengo la kuokoa maisha na kulinda mali. Taasisi hiyo pia hushiriki katika uratibu wa utoaji wa misaada ya kibinadamu kwa waathirika wa maafa na kusaidia shughuli za kurejesha hali na makazi katika maeneo yaliyoathirika.

Katika eneo la kujenga uwezo wa rasilimali watu, AFAD inaendesha mafunzo na mazoezi ya vitendo kwa wataalam na timu za mwitikio wa maafa kupitia miundombinu yake ya mafunzo, ikiwemo Disaster and Emergency Training Centre (AFADEM). Mafunzo hayo yanalenga kuongeza ujuzi wa kitaalamu, uwezo wa kufanya kazi kwa pamoja na utayari wa kukabiliana na matukio ya dharura.

Gavana Pehlivan ameongeza kuwa AFAD pia hushiriki katika ushirikiano wa kimataifa wa usimamizi wa maafa kupitia Timu ya Kimataifa cha Utafutaji na Uokoaji (The International Search and Rescue Advisory Group - INSARAG) ambayo inasimamiwa na Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (UN-OCHA) katika kupeleka timu maalumu za utafutaji na uokoaji na kutoa msaada wa kibinadamu katika nchi mbalimbali pale kunapojitokeza maafa makubwa.

Tanzania na Uturuki zimeendelea kuwa na fursa ya kubadilishana uzoefu na utaalamu katika eneo la usimamizi wa maafa, hususan katika teknolojia, mifumo ya taarifa na tahadhari za mapema, mafunzo, utafutaji na uokoaji, uratibu wa mwitikio wa kukabili na urejeshaji wa hali, kwa lengo la kujenga jamii na taasisi zenye uwezo mkubwa wa usimamizi wa maafa.