Benet na JMK ndo hiyo tena. Picha ingine chini inahusu siku tuliyokwenda naye kuangalia madhara ya mafuriko huko jimboni kwake Chalinze. Maji yalijaa kibao kila sehemu ikabidi tukodi mtumbwi, madereva sie waandishi. Picha hiyo ya chini ilitoka jana 24/12/05 ukarasa wa mbele gazeti la Majira. Jamaa alinipigia simu kuhoji kama nimeiona. nikavunga nami pia nilitaka kupiga ila sina namba yake. tukacheka sana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Mh, michuzi nawe si haba.

    ReplyDelete
  2. Michuzi, safi sana.

    Mbona huyu dada hapo kwa pembeni umemkata!

    Tunashukuru sana mkuu kwa picha na habari motomoto.

    Nakutakia kila lakheri na maandalizi mema ya kukaribisha mwaka mpya wa 2006.

    Mwenyezi Mungu akulinde na akujalie neema zaidi wewe pamoja na familia yako na marafiki zako pamoja na mahasimu wako!

    ReplyDelete
  3. Hi Michuzi,

    Naona umetoka kwenye picha uliyopiga na Rais Kikwete. Msalimie sana.

    Napenda sana kutazama picha zako! Endelea na kazi nzuri, best wishes!

    ReplyDelete
  4. Michuzi,

    Mwambie Rais awe anapitia na huku kwenye blogu zetu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...