Mama Anna Mkapa akimuamkia Mzee Rashidi Mfaume Kawawa huku Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na aliyekuwa Mshauri wa Siasa wa Rais Mzee Kingunge Ngombale Mwiru na mkewe kawawa wakiangalia Ikulu Dar. Kuna uvumi uliosema Mzee Kawawa amefariki na hii ni picha ya karibuni (21/12/05) mara baada ya kutoka India kwa matibabu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. samahani ndugu wanablogu! hivi ni kitu gani kilimfanya mzee kawawa aitwe simba wa vita? - ni kulimiliki vizuri lile igizo la mwalimu kujiuzulu na kumkabidhi na kisha kumrudishia tena ukuu? - maana sasa inabidi kuanza kuchuja haya masimulizi isije ikawa yale yale ya kila mzazi kudanganya watoto wake etri alikuwa anakuwa wa kwanza darasani kila mara! je nani alikuwa anakuwa wa mwisho?

    ninaombeni maelezo wanablogu!

    cheers

    ReplyDelete
  2. Mimi nimesahau asili ya jina hili lakini kwa leo "Long live Simba wa Vita"

    ReplyDelete
  3. Hivi mna habari Mzee ruksa ni mkubwa kiumri zaidi ya Mzee Kawawa?

    ReplyDelete
  4. Duh!
    Sasa anonymous unazua mjadala mpya! lakini nadhani mtu wa kutusaidia katika kupata ufumbuzi ni MICHUZI anayejigamba kugongana nao mabega kila mara IKULU. ni bora awatafute afanye nao mahojiano atuondoe gizani.

    ReplyDelete
  5. Mbona mzee kingunge anamuangalia sana mke wa kawawa???????

    ReplyDelete
  6. we mwache aende ovyo! na hawa wazee walizoea....makiambiwa....hawaelewi somo!!

    ReplyDelete
  7. "Simba wa nyika'ni jina lilo toka na uchezaji wa cinema,(Hollywood ya bongo) kabla ya kukutana na Mwl,Nyerere

    ReplyDelete
  8. sasa ma'mkapa anamwamkia mzee kawawa, na je ma'kawawa atamwamkia ma'mkapa?????

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 16, 2006

    Katika CInema Rashidi Kawawa alitumia jina la Muhogo Mchungu mie sijawahi kusikia alitumia "Simba wa Vita" labda hili lina asili yake ambayo labda Michuzi anaijua

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...