
Watoto wa Jah Kaya Dagna Iddi (kushoto) na Albert Mangwair wakionesha mavazi yao ambayo wameyabuni na ambayo yako chini ya lebo ya "120" ambayo inatamba sana Bongo hivi sasa. Huu ni ubunifu ambao wasanii wetu wengi wameibukia ili kuongeza taswira zao na kipato. Jana 22/12/05 walitinga Ikulu na wasanii wengine kwa mwaliko wa rais JM Kikwete aliyewaita kuwashukuru kwa tafu waliompa wakati wa kampeni. Jakaya alikunwa sana na T-shet za 'Mtoto wa Jah Kaya, na aliwasifu wasanii hawa kwa ubunifu. nao walimfagilia sana kwa kuwa rais wa kwanza kuutambua mchango wa wasanii wa kizazi kipya kiasi hata kuwaalika Ikulu.
Habari hii imenivutia sana. Ubunifu huu hasa kwa vijana unatia moyo. je wana tovuti? Anuani yao ya barua pepe au simu unayo? Ningependa kuipata.
ReplyDeleteMichuzi safi sana dalili njema hii ya huyu Mkuu wetu mpya anakumbuka nasi kuingia ikulu nadhani siku si nyingi muombeni walau kuwa na spesho day ya Watanzania kuingia hapo na kupiga vipicha, namna hii tunakuwa karibu na viongozi wetu na hofu ya wao kuwa mbali nasi inapotea na kweli wanapata kusikia shida zetu moja kwa moja. Mwambie hatutaki mahubiri ya kila mwisho wa mwezi badala yake awe na utaratibu wa kukutana na wananchi wa kariba zote. Thanks again Michuzi, nadhani hata Mwaipopo mzee wa Alabama ataipenda hii.
ReplyDeleteyahhh hii ni safi! wanasema unapotupiwa mbeleko unaikamata na wewe unajitahidi kung'ang'ania bega. la sivyo watasema unabebwa hubebeki!
ReplyDeletecheers
Ndesanjo nimekusikia.
ReplyDeleteNamba ya Dagna Iddi ambaye ni mbunifu wa lebo ya "120" ni +255 22 745 803603. yeyote aliye ughaibuni namwanikia namba hii kwani vijana wetu wanahitaji msaada wenu sana, hata wa mawazo.
Hii ndiyo ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya (sijui kama nimeziweka kwa mfuatano sahihi)
ReplyDeleteUbunifu mpya wahitajika kwa wasanii. Hapa Marekani wakina Jay Zii na Senti Hamsini wanapata mafanikio sana kwa masuala ya lebo na kuuza nguo.
Michuzi,
ReplyDeleteNadhani ulitaka kusema kuwa namba ya Dagna Iddi ni +255 745 803603.
Ahsante.
Kaka michuzi nimekupata!Kwa mara ya kwanza kukuona ilikua 2003 wakati ukiwa kwenye heka heka za kupiga picha wakuu wa nchi waliohudhria Mkutano wa SADC uliofanyika jijini Dar es salaam.
ReplyDeleteNapenda kuchukua fursa hii kwa niaba ya wanablog kukuomba mheshimiwa MICHUZI utupelekee kilio chetu kwa Mheshimiwa JK cha kutaka japo tukutane nae tubalishane mawazo na kumpa changamoto za kifikra zinazozidi kushika kasi katika mtandao wa wanablog
Ngoja tupate jina la Magazeti Tnado yetu haya na baadaye unakuja mtandao mkubwa wa wamiliki na waandishi wake kutoka Tanznaia. Sasa fikiri agenda isije ikatokea tunafika hapo Materu unaanza kupongeza kisha unataja taja majina tu kwa mistari isiyo na vina. Mwaipopo hii pi anaijua na jua hapo alipo ni ehe ehe
ReplyDeletekweli mkubwa
ReplyDeleteKaka makene mistari isiyo na vina tumeshaitupa kapuni kwani haitufai kanisani,haitufai msikitini na haitufani kwenye fani.
ReplyDeleteNadhani agenda kuu ya kusisitiza na uhuru wa mawazo katika sekta ya habari na mchango wake katika kufufua fikra za kimaendeleo.
Nilipowaangalia hawa vijana wa Jah Kaya nikawatazama kwa kufuata historia za wasanii wa namna yao kama kina Hayati Mzee Makongoro, Hayati Ramadhani Mwinamila, hadi Kapteni John Komba, na kutelemka chini kufikia kwao. Nilichoona kabla ya kusikiliza ni "vijana" na sijui kama tunaweza kuwapanga katika safu moja na kina Hayati Makongoro, Hayati Mwinamila, na Kapteni John Komba. Manojua usanii wa namna yao naomba mnipe mawazo yenu!
ReplyDeleteAsante,
F MtiMkubwa Tungaraza.
Nilipowaangalia hawa vijana wa Jah Kaya nikawatazama kwa kufuata historia za wasanii wa namna yao kama kina Hayati Mzee Makongoro, Hayati Ramadhani Mwinamila, hadi Kapteni John Komba, na kutelemka chini kufikia kwao. Nilichoona kabla ya kusikiliza ni "vijana" na sijui kama tunaweza kuwapanga katika safu moja na kina Hayati Makongoro, Hayati Mwinamila, na Kapteni John Komba. Mnaojua usanii wa namna yao naomba mnipe mawazo yenu!
ReplyDeleteAsante,
F MtiMkubwa Tungaraza.
www.120.co.tz
ReplyDeleteemail: inf@120.co.tz