huyu ndiye zakaria ndabameye aliekuwa mmiliki wa bendi ya dar international orchestra chini ya jabali la muziki marijani rajabu. bw. zakaria hivi sasa anaishi kijijini kwake mjesani nnia ya kuelekea maramba huko tanga, akiwa hoi bin taabani, pamoja na kwamba bendi yake ilikuwa na nyimbo zipatazo 695 na albamu lukuki. ishukuriwe sheria butu ya hakimili ya tanzania ambapo mtu unaweza kuibiwa kweupeeee. enyi mlio ughaibuni, dili hili. ukiweza kuja na 'fomyula' ya kupambana na wizi wa hakimiliki umeula! muziki bongo sasa unashindana na unga! unaambiwa juma nature anaendesha benzi la dola 45,000, ana jumba la kifahari la milioni 150 na mapene kibao. na hapo anaibiwa!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. niliwahi kumuomba raisi mpya wa jamuhuri wa muungano (rejea barua kwa raisi mpya kwenye blogo langu) kuunga juhudi za kulinda haki za watu wanaofanya kazi zao kwa bidii kama hawa. kilichobaki hapa ni nia tu ya utawala, jambo ambalo nahisi kikwete ana uwezo wa kulifanya. kwa mfano, sitaelewa kwa nini polisi na TRA wasifanye kazi bega kwa bega kudhibiti uhalifu wa kazi za wenzao? kwani pia pato la taifa si linapotea hapo? au watasema kuwa bado hawajatambua muziki kuwa kazi kama nyingine? huo mwanya ni kwa faida ya nani? si ni mazingira ya rushwa tu? pia kuna formula ya scorpion hapa SA inatumika, unachotakiwa ni kuwa member na utacheka vihela vyake ni kiduchhuuuu kweli, wanafuatilia kazi za wanachama....hii lakini yawezekana kama utawala utakiri nia yake bila kigugumizi!!

    hili pia ni suala ninaloniumiza sana nadhani kuna haja ya kutafuta gear mpya...asante sana michuzi, nimeona ujumbe ndio kwanza umeuweka, nasubiri picha!

    ReplyDelete
  2. Mark Msaki amesema yoote kwa kweli. Maono yangu huyu Prez Jakaya atafanikiwa katika hili maana amekwishatambua kazi za wasanii (pale alipowaita 'White House'). Cha muhimu ni kumu-ignite tu. Wezi wote watakoma kuringa.

    Michuzi kapicha vipi?

    ReplyDelete
  3. kikwete naye anacopy sana cd, naye mwizi tu.

    ReplyDelete
  4. Tafadhali kama unazo naomba uzibandike namba ya simu, anuani ya posta, e-mail, jina la mtaa au kijiji anapoishi ya Ndugu Zakaria Ndabameye na pia kama utaweza kunisaidia namba ya simu, anuani ya posta, na e-mail ya Mzee david Musa aliyekuwa mmiliki wa bendi ya Safari Trippers ambayo pia ilikuwa mwajiri wa Hayati Marijani Rajabu.



    Ninaomba ushirikiano wako kwa sababu ninajaribu kutafuta makampuni ya rekodi na watu binafsi ambao wataweza kuhifadhi kazi za Hayati Marijani Rajabu katika teknolojia ya kisasa na kuyaminika hali kadhalika kuwapatia vipato wamiliki, familia ya marehemu na wanamuziki wenzake walioshirikiana katika kazi zake za kimuziki.

    ReplyDelete
  5. we michuzi utakuwa na million dolla, unapiga picha siku nyingi sana.hata watu wa ughaibuni tunajua hivyo.

    ReplyDelete
  6. tuletee picha ya crib ya huyu selebriti j-necha,na na hiyo cedes yake, tafadhali sana mzee michuzi.

    ReplyDelete
  7. michuzi mzushi

    ReplyDelete
  8. mark msaki maelezo mengi sanaaaaaaa, si uweke website yako tu bwana.

    ReplyDelete
  9. ndesanjo, bw. alama, jeff,baragumu, ida, semkae n.k naomba ulinzi! jamaa kaniita mzushi,halafu anajificha, nimfanyeje?

    ReplyDelete
  10. michuzi tusaidie kwa kweli, kazi yako yaweza leta mabadiliko makubwa kwa jamii, huyo anony hapo aliyeomba anuani za mzee wa safari trippers anaweza sana kuhifadhi utamaduni kwa kuziweka kwenye mambo za sasa.

    nilikuwa pia nawaza. hawa watu kama msondo, je kazi zao za tokea awali teyari zipo kwa digital?

    anony, ukienda pale kwa jina langu, ukiclick basi utapelekwa kasisini mwangu....

    michuzi nakuhakikishia usalama!

    ReplyDelete
  11. Michuzi Ida ni nani? Isijekuwa Idya Nkya unamwita Ida.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...