MSANII wa muziki wa kizazi kipya,. Ferooza usiku wa kuamkia jana alipagawisha mashabiki wa muziki visiwani hapa na kibao chake cha starehe.Ferooz alianza kulishambulia jukwaa majira ya saa sita usiku, akiwa na kundi zima la Daz Nundaz lenye maskani yake Sinza jijini Dar es Salaam.Msanii huyo anayetamba na kibao chake cha Starehe alizikonga nyoyo za mashabiki waliokuwa wamefurika visiwani hapa kwenye ukumbi wa Ngome Kongwe kushuhudia tamasha la tatu la Sauti za Busara linaloendelea visiwani hapa.Kabla ya kuwapagawisha mashabiki na kibao cha Starehe Ferooz na kundi zima la Daz Nundaz ni waliwapagawisha na vibao vyao kama ‘Nafsi’, Nipe Tano, Jirushe, Boss na Kamanda.Wakiongozwa na mkongwe wa Bongo Fleva Mr II maarufu ‘Sugu’ wasanii haoa wa Daz Nundaz walifunika bovu na kusababisha vurugu kubwa kwenye tamasha hilo linaloanza kila siku saa kumi jioni hadi majogoo.Mbali na kundi hilo la Daz Nundaz linaloongozwa na Ferooz Mr II naye hakubaki nyuma pale alipopagawisha mashabiki kwa kibao chake cha Sugu ambacho kilichengua mashabiki ambao walimtaka kuendelea kuimba.Wasanii wawili ambao unaweza kudhani ni mapacha, Mandojo na Domokaya pia walizikonga nyoyo za mashabikiwa kwa vibao vya ‘Taswira’, ‘Wanafki nafki’ ambao wamemshirikisha Lady Jay Dee, Nikupe, ‘Leke Lekee’ na Usiponisikia.Wasanii wengine ambao hawakubaki nyuma kuzikonga nyoyo za mashabiki wa visiwani hapa usiku wa kuamkia jana ni `Black Root (Zanzibar), Taffetas (Guinea Bissau, Bukina Faso, Mali, Swatzerlad), New Sound Band (Burundi), Ukoo Flani Mau Mau (Kenya), The Shrine Synchrosystem (Ghana, Uk, Nigeria)Vikundi vilivyotarajiwa kutumbuiza jana jioni ni African Ngoma, Kyandu Music, Tamarind Band, Mkalimala group, Black Roses, Wagosi wa Kaya na Jangwa Music.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Michuzi,
    Taarifa na picha za tamasha la Sauti za Busara sizipati kwingine kama ninavyozipata hapa kwako.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...